Kama maneno hayo hayo yangesemwa na Mgombea mkristo na akashinda tusingekuwa na khadithi za kutengana na kunyanganywa ukristo kwa baadhi ya wauminiHTML:Huyo mgombea wa ccm Rukwa alisema yeye ni Yesu, mgombea urais ni Mungu baba na diwani ni Roho Mtakatifu. Kanisa lililaani na kuwakataza waumini kumshabikia mtu nayekufuru
Sina hakika kuna maana gani iliyojificha kwa hayo maneno ya kujifananisha na Yesu, Mungu na Roho Mtakatifu lakini naamini si maneno mazuri kutumiwa kwa mzaha na mwanasiasa.
Kwanini?
kwasababu tunajua kuongelea au kufanya utani katika imani za watu kunaweza kusababisha madhara makubwa sana. Hata hapa Tanzania tuna mfano; Kumbuka yule aliyesema Yesu si Mungu, je tumesahau sakata lililofuatia. Je yule aliyechora katuni ya Mtume Mohamed kule Denmark. Je yule Mchungaji aliyekuwa anataka kuchoma Koran wakati wa maadhimisho ya 11/9. Na je vita ya kidini nchini Nigeria iliyoanzia kwa mchoma mishikaki! Mifano ni mingi, lakini nia nikujaribu kuona jinsi gani kitu kidogo kwenye mambo ya dini kinaweza kusababisha matafaruku mkubwa na hata vita!
Mwisho
Kwa vitu vinavyohusu dini ni bora wote tukajaribu kuviepuka, si rahisi mtu kujua matokeo ya kufanya utani kwenye dini za watu. Nafikiri kwa mifano ya hapo juu tunaweza ku-imagine reaction za watu dini zikihusishwa! Ni vyema dini nyingine na vyama vimeamua kujitenga na malumbano hayo ya Sumbawanga kwasababu hiyo inaweza kuchochea mzozo na kuhusisha hata maeneo mengine!
Mungu ibariki Tanzania!