YA "TBC" na miaka 35 ya CCM

buhange

JF-Expert Member
Oct 23, 2011
505
110
Ndugu wana JF,

Ni wakati mwingine wa kujadili na kuweka sawa maswala tata yanayoendana na maslahi ya taifa.
Kwa tukio la leo wakati TBC wakijaribu kurusha maadhimisho ya miaka 35 ya magamba kule Mwanza ndo hasa yamenisukuma nitupie uzi huu.
Hivi TBC inaonyesha sura gani kwa mwenendo wa utendaji wake kwa sasa?, hii ni televisheni ya taifa au? maana utendaji wa shirika hili unaweza kufanishwa kabisa na mwenendo wa Magamba, kila kitu kufanywa kwa uzoefu, habari inagoma kuruka hewani mpaka mara mbili?
 
acha hzo bana, sasa si imegoma kuruka we unafikiri wametaka igome kuruka, mbona mnataka kuleta mambo yasiyo na maana! anywai unafikiri labda nini wewe???
 
Kwani Tbc bado ipo? Me huwa naangalia television ya taifa ITV
 
CCM wamelipia matangazo yote ya Star TV na TBC........Hata CUF,CHADEMA,NCCR-Mageuzi,TLP et al wanaweza kulipia na kurushiwa mikutano/vikao vyao ama shughuli yao yoyote Live kama ilivyokuwa kwa CCM leo....
 
nina sababu ya kuuliza mkuu, maana mambo ya serikali hii kupenda kutuletea vyuma chakavu ndo matokeo yake haya tunaaibika worldwide maana kama ATC kumejaa ndege chakavu itashindikanaje TBC kujaza vyuma chakavu? kumbuka siyo leo tuu, imekuwa mazoea yao. Leo, imegoma taarifa toka ktkt ya jiji la mwanza, Je! ingekuwa Basanza huko Kigoma si tusingeona kitu kabisa. Fikiria vema kuhusu sera ya manunuzi ktk taifa hili halafu rudi tena hapa mkuu, inawezekana sana hoja yako imejengeka kimantiki, karibu uwanjani...
 
pyaaaaa!!! kama bata kanya.
 
Back
Top Bottom