Ya Nishati Na Madini, Ni Kioja Kingine

makerubi

Member
Apr 11, 2011
81
3
Na Maggid Mjengwa,
PTOLEMY, mwanafalsafa wa Kiyunani alipata kuandika: ”Ex Africa simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika."

Naandika makala haya nikiwa nchini Sweden. Katika kufuatilia yanayoandikwa na kusemwa na wanahabari wa Sweden kutuhusu sisi, basi, nimekutana na kashfa ambayo kimsingi ni kioja chenye kutuhusu.

Hapa Sweden kuna Shirika la Misaada limeishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey, inavuna gesi ya Songosongo nchini Tanzania; huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli , TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid, iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 10. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabini na tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi uliotamalaki unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Unatuacha tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na mkataba wa kifisadi usiotanguliza maslahi ya Taifa. Taarifa hii niliweka mtandaoni majuma mawili yaliyopita na hakika wengi wameshiriki kuitolea maoni yao.

Ni jambo la faraja na kutia moyo kuwa hata waheshimiwa wabunge, bila kujali itikadi zao za vyama, wameanza kuamka na kuwa wakali kutetea rasilimali zetu. Na hakika, huu ni wakati wa waheshimimiwa wabunge wetu kumweka kikaangoni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na Waziri Ngeleja atwambie ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii, na hivyo basi kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

Naamini kuwa nchi yetu ni nchi tajiri sana, lakini wananchi wake wengi wamo katika lindi la umasikini unaotokana na ufisadi wa wachache tuliowapa dhamana za uongozi.

Haiyumkini mtu mwenye akili zake na anayeipenda nchi yake akakubali kuingia mkataba wa miaka 25, kwa maana ya robo karne, na kampuni ya kigeni kuruhusu wageni hao wavune gesi yetu asilia iliyo kwenye visima vyetu kule Songo Songo.

Na kioja katika mkataba huo ni mgeni mwekezaji anayevuna gesi yetu tunakubali asitozwe kodi kwa faida anayopata kwa kutuuzia umeme unaotokana na gesi ya kwetu wenyewe! Kwa mwanadamu, ni heri uwe mwendawazimu kuliko kuwa limbukeni. Watanzania tumefanywa kuwa malimbukeni.

Na majuzi hapa tumemsikia Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo, akimtuhumu Bungeni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia Shiolingi bilioni moja kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge. Nacho ni kioja kingine kwa wizara ya serikali kutumia fedha kuwahonga wawakilishi wa wananchi ili bajeti ipite, na wawakilishi hao wakapokea hongo hiyo.

Ni jambo jema kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufikia busara ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini. Na itakaporudi tena bungeni, ni wakati wa wabunge wetu kusimammia maslahi ya umma na kuibana Wizara kufafanua baadhi ya mikataba yenye kashfa kama huu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli, TANESCO na kampuni ya Pan African Energy.

Na kauli ifuatayo ya Mbunge wa Nzega, Mheshimiwa Hamisi Kingwangwalah inatia matumaini kuwa bado tuna wabunge walio tayari kupambana kutetea maslahi ya umma.

Mbunge Kingwangwalah aliyasema haya bungeni:

"Nataka nianze kwa kusema siungi mkono hoja ya kupitishwa kwa bajeti hii na nawaomba wabunge wenzangu msipitishe bajeti hii kwa sababu tupo gizani". Mbali na tatizo la umeme, alitaja sababu nyingine za kutaka bajeti hiyo isipitishwe kuwa ni mikataba mibovu ya sekta ya madini na nishati ambayo imesababisha rasilimali za nchi kuibwa na wageni huku Watanzania walio wengi wakiendelea kuogelea kwenye umasikini.

Mbunge Kingwangwala anasema: "Waliosababisha hayo wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua. Wengine wapo hapa bungeni na wengine wako serikalini. Hii ni mikataba kandamizi. Watu hao wapo kwenye 'system' (mfumo wa Serikali). Nchi inauzwa, wachache wanashibisha matumbo yao. Watu hawa wamelifikisha taifa kwenye mazingira haya ya kifisadi kwa sababu ya kutumia nafasi zao kujinufaisha na kuweka kando maslahi ya umma wa Watanzania...Hawa watu kama hawafikirii kwa matumbo wanafikiria kwa kutumia 'spinal cord' (uti wa mgongo) badala ya ubongo."

Mbunge huyo akaongeza kusema; “ Watendaji walioliingiza taifa kwenye mikataba hiyo mibovu wanapokwenda kuisaini wanajali kile watakachopata ili kufanikisha malengo yao binafsi kama vile kujenga majumba ya kifahari. Wanaruhusu ardhi ya Watanzania kuuzwa nao wanafaidi kwa kwenda kujenga Mbezi Beach (Dar es Salaam),"

Akaongeza kusema: “Miongoni mwa mikataba ya kifisadi ni kati ya Pan African na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusiana na uzalishaji na usafirishaji wa gesi asilia.” Mwisho wa kumnukuu.

Ndio, kuna baadhi ya viongozi wetu wameigeuza nchi yetu kuwa Banana Republic. Katika Banana Republic, wanasiasa wachache hutumia siasa kufanya biashara na uchumi wa nchi. Wako tayari kuuza rasilimali za nchi kwa faida yao.

Watanzania tuna lazima ya kukataa kugeuzwa malimbukeni na kuruhusu nchi yetu kuwa Banana Republic’- Jamhuri ya Migomba. Nahitimisha.
 
Mod usifute kwa niaba ya watanzania wengi ambao hatukuisoma hii kashfa. Uuiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, nakufa,nchi yangu inaisha. Kikwete utauwa generation inayokuja after you. watoto wako na wajukuu watarithi nini kama unauza nchi namna hii. Mlaaniwe wote mnaohujumu nchi. Tutafukua makaburi yenu hata mkifa na tutaisagasga kwa hasira dhidi ya dhuluma zenu. Usalama wa Taifa mko wapi wakati nchi inateketea? Mlaaniwe na nyie kwa kuifanyia ccm ujasusi huku wananchi wazalendo wakiumia na dhuluma za watawala za kuifilisi nchi. Nchi hakuna usalama wa Taifa. Ni usalama wa marais na mawaziri. Laana iwe juu yenu pamoja na wabunge wa kama makinda, ndugai, simba chawene, etc
 
Mod futa hii ,,, ishawekwa tangu wiki iliyopita humu.

Wewe kaka kweli ni jambazi kama jina lako! Hii thread sio ya kufuta hata kidogo! Unaogopa nini? Acha ambao hawajaisoma hii habari waisome (Mkataba wa PAE). Uwiiiiiiiiiiiiii! Masikini Tanzania! Naona aibu kujitambulisha taaluma yangu! Eti mwanasheria! Mie nadhani mikataba huko serikalini huwa inaandaliwa na madaktari wa meno na sio wanasheria!
 
Mod usifute. Kama ungefuta nisingeona hii. Huyo anayesema ifutwe ana matatizo kwenye ubongo wake hata kama ilishaletwa hapa 2 yrs ago. Nahisi kulia haki ya Mungu. Jamani kampuni inavuna gesi kwa miaka 25 bila kutozwa kodi??jamani jamani jamani....halafu eti tunajivunia miaka 50 ya uhuru?uhuru gani?wa giza na umaskini uliokithiri?kila kona ya nchii hii ni malalamiko tu hata watoto wadogo walio under 18 wanaona jinsi mambo yanavyokwenda holela. Halafu najiulizaga hivi hawa wenye dhamana huwa wanapitaga huku jamvini kusoma hizi taarifa zinazoletwa na wazawa? Ni ubadhirifu uliokithiri na rushwa ya hali ya juu.
 
jamani jamani!!! jamani naumia mie, nashindwa kulia,kunyamaza, kucheka hata sijui nifanye nini miye mtoto wa mkulima!
 
Back
Top Bottom