Tausi Mzalendo
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 1,471
- 722
Mashambulizi ya wadau katika jamii kwa kushindwa kutumia lugha ngeni ya Kiingereza ndio sababu inayofanya Watanzania wengi washindwe kujifunza hio lugha kwa ufasaha kwa woga wa kuchekwa, kebehiwa na hata kusanifiwa ukikosea (mara nyingi hata wakosoaji unakuta pia lugha hawaielewi ila tu bado amcheka mwenzie). Ile sio lugha yake na wala hata makosa katika kukosea... Na ilibidi tu aweke wazi kuwa hio lugha inampiga chenga sababu makosa ni mengi kafanya katika hotuba yake yote.
Hata hivyo hii slip of the tongue ni acceptable kabisa, kosa kubwa lipo kuwa anawakilisha entity ambayo Kimssingi, hairuhusiwi na ni kosa kubwa kutoelewa lugha ya Kiingereza hasa ukizingatia ndio lugha kuu ya maofisini ukiacha Kiswahili. Naamini kwenye 'vipengele husika' vya sifa ya mtu wa ku cover hio nafasi LAZIMA kuna kipengele kinasema mtu awe fluent in English. Sasa sababu serkali yetu inatowa kazi kwa vigezo vya kujuana, connections na upendeleo ndio madhara yake haya...
Katika aibu kwenye conference, katia aibu serkali yake then akatutia aibu na sisi hali tuna watu ni wanastahili hata wangeenda pale wangewakilisha vilivyo.
Da AshaDii,
Heshima yako kwanza kabla sijachangia. Nakuunga mkono kabisa kuwa wziri huyu asilaumiwe sana kwenye lugha. Ila pia nadhani tukiangalia maelekezi ya criticism tutaona kuwa kinachozungumzwa kwenye hili sakata, kimsingi siyo umahiri wa lugha.Tunaangalia kwa mapana dhana ya kuwakilishwa na kiongozi wa level ya juu kama Waziri kwenye international conferences. Kuna makosa ya kawaida ya slip of the tongue na haya hayakwepeki huwa yapo lakini mtelezaji hutarajiwa mara moja kujisahihisha.Kuchanganya Zimbabwe ba Zanzibar siyo kiingereza bali ni kosa dogo but with far reaching implications.Kuchanganya tarakimu kwenye mwaka nalo siyo kosa la lugha.
Binafsi nimeweza kuona kuwa kuna makundi mawili ya critics kwenye hii ishu.Kuna watu wanaolalamikia maswala ya kimsingi na pia kuna kundi linalojadili umahiri wa lugha. Kwenye lugha nako kuna vitu vya msingi ambavyo kiongozi wa level ya juu kabisa ya uongozi hatarajiwi kuyafanya.Kwenye mikutano ya kimataifa tunarajia " HIGH QUALITY PARTICIPATION( CONTENT WISE) NA HIGH LEVEL OF REPRESENTATION ( BOTH CONTENT AND TRIMMINGS SUCH AS GOOD COMMAND OF LANGUAGE, PRESENTATION SKILLS, PERSONAL APPEARANCE ETC).Hatupaswi kujali sana swagga na kutema yai kwa maana ya lafudhi kwa maana kwenye hadhira za kimataifa utakutana na lafudhi zote - za kihindi, za kiarabu, za kinaijeria, za kikenya,Kisenegali, kihabeshi, za kiganda, kispaniola, kiitaliano nk).Waziri huyu kwa kweli atuombe radhi watanzania kwa kutokutuwakilisha kwa ufanisi na siku nyingine asing'ang'anie kupanda ndege kabla ya maandalizi.