Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Wewe acha kutetea bila msingi huwa kuna neno "kumradhi"alipoteleza alirekebisha?Na kuseme zile in 1 19..?Embu tusipotoshe Ukweli hapa Mh.alionesha udhaifu.Kwa mtazamo wangu hapaswi kuwa kiongozi wa wizara nyeti ya elimu wakati elimu inamsumbua.
 
HUYU "MWALIMU MZOEFU" wa somo la historia kama alivyojiita mwenyewe hajateleza ulimi wala nini.
Kakubali kuwa hana umahiri wa kutumia PPT... kwanini basi alikubali kwenda kufanya presentation kwenye hadhira ya kimataifa huku akijua ni maamuma kwenye hilo eneo? Uzoefu wake kama mwalimu hatujauona popote kwenye ile presentation na hata hapa radioni kwenye kujitetea.
AKUBALI YAISHE KUWA HANA SIFA ZA KUWA WAZIRI WIZARA YA ELIMU BAAAS!
Hili ni fundisho kuwa MAWAZIRI WANATAKIWA AMA KUWA MAHIRI SANA KWENYE MAMBO MENGI, AU BASI WABAKIE KUPIGIA DEBE TU SERA ZA CHAMA BILA KUINGILIA MAMBO YA TAALUMA ZENYE WENYEWE.
 
huyu si mbunge wa Songwe kule Mbeya mpakani na Malawi nahisi jamaa si raia wa Tanzania na pia jamaa alikua anataka kuuaminisha ulimwengu kwamba Tanzania ina tamani ardhi ya nchi nyingine hivyo
 
Pasco,

Kabla hatujakusaidia kubadili title, nawe 'umetelaza' :)

Naona naye kajitetea kuwa aliteleza tu.


Hapa bwana ni ngumu kujitetea akaeleweka...

Ndani ya dakika 10, mtu anaweza kuteleza mara ngapi ikabaki within normal (not exceeding elasticity limits)??

Hata hivyo, huku site wanatoa ushuhuda kwa huyo ndiye yeye (Mulugo).....sifa za kitaaluma tunazooneshwa kwenye makaratasi siyo zake....Sifa zake kamili ni hizo alizotuenesha live...

Bahati nzuri...kilema hakifichiki...na uwezo wa mtu hauwezi kufanyiwa maigizo/usanii....Mifano ni mingi hapa bongo...kuanzia ofisi kuu hadi kwa balozi wa nyumba kumi kumi!

Bora wanyamaze tu!!
 
Vipi na ile one nineteen sixty four? Na yenyewe ni kuteleza kwa ulimi?

Huyo ni KIHIYO. Waziri wa Wasomi utasomaje "speech" neno kwa neno kama mtoto wa Primary school? kwa mfano kusoma maneno"INTRODUCTION" Pili: Je una-"conclude" halafu unatoa "The way Forward" au unatoa "the way Forward" halafu Conclusion? Msikilize tena kabla ya kumtetea. TAFAKARI
 
Wanabodi,

Kumekuwepo kwa thread mbali mbali za kumshutumu, kumbeza hadi kumkebehi Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Phillip Mulugo kwa kauli yake ya Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba!.

Naomba kujitokeza kumtetea huyu jamaa "It was only a slip of a tongue!. Yaani aliteleza tuu ulimi!.

Ukiangalia ile video kwenye U-Tube utaona ni PPT Presentation kupitia Over Head Projector kila neno alilotamka pia limeandikwa na kuonyeshwa na ile projector screen.

Japo ni kweli aliitamka neno Zimbabwe lakini screen ya projector ilionyesha neno Zanzibar!. Hivyo hilo neno Zimbabwe, was a sleep of a tongue tuu yaani aliteleza ulimi ni kosa la kawaida la kibinaadamu!.

Kufuatia kosa hilo dogo tuu, kitendo cha Clouds Redio kumkomalia hana nzima sio cha kistaarabu na sio kumtendea haki!.

Watu sasa wameanza hata kuhoji elimu yake!. Watanzania sasa tumekuwa wagonjwa wa "paper qualifications" watu humu sasa wanamkomalia kuhusu elimu yake!. I doesn't matter jamaa ni jembe kweli!. Nimemshuhudia akipiga mzigo wa kufa mtu!. Akifanya ziara za kikazi popote, hufanya 'surprize visit" kwenye mashule au vyuo na kuibua madudu!.

Tumhukumu mtu kwa utendaji wake na sio kwa "Sleep of a tongue"!.
Pasco.

Ni kama kipofu mwenye miguu mizima kambeba kilema bubu ili amwongoze na kumwonyesha njia
 
HUYU "MWALIMU MZOEFU" wa somo la historia kama alivyojiita mwenyewe hajateleza ulimi wala nini.
Kakubali kuwa hana umahiri wa kutumia PPT... kwanini basi alikubali kwenda kufanya presentation kwenye hadhira ya kimataifa huku akijua ni maamuma kwenye hilo eneo? Uzoefu wake kama mwalimu hatujauona popote kwenye ile presentation na hata hapa radioni kwenye kujitetea.
AKUBALI YAISHE KUWA HANA SIFA ZA KUWA WAZIRI WIZARA YA ELIMU BAAAS!
Hili ni fundisho kuwa MAWAZIRI WANATAKIWA AMA KUWA MAHIRI SANA KWENYE MAMBO MENGI, AU BASI WABAKIE KUPIGIA DEBE TU SERA ZA CHAMA BILA KUINGILIA MAMBO YA TAALUMA ZENYE WENYEWE.

TausiMzalendo: Hapo kwennye RED: Ni uroho wa POSHO (DSA) ulimponza. Ni sawa na "Nzi kufia Kidondani"
 
Pasco said:
Naomba kujitokeza kumtetea huyu
jamaa "It was only a slip of a
tongue!. Yaani aliteleza tuu ulimi!.
Japo ni kweli aliitamka neno
Zimbabwe lakini screen ya projector ilionyesha neno Zanzibar!. Hivyo hilo
neno Zimbabwe, was a sleep of a
tongue tuu yaani aliteleza ulimi ni
kosa la kawaida la kibinaadamu!... I
doesn't matter.
Tumhukumu mtu kwa utendaji wake
na sio kwa Sleep of a tongue"!.

Lugha sahihi hapo ni ipi slip of a tongue au sleep of a tongue?
 
Mashambulizi ya wadau katika jamii kwa kushindwa kutumia lugha ngeni ya Kiingereza ndio sababu inayofanya Watanzania wengi washindwe kujifunza hio lugha kwa ufasaha kwa woga wa kuchekwa, kebehiwa na hata kusanifiwa ukikosea (mara nyingi hata wakosoaji unakuta pia lugha hawaielewi ila tu bado amcheka mwenzie). Ile sio lugha yake na wala hata makosa katika kukosea... Na ilibidi tu aweke wazi kuwa hio lugha inampiga chenga sababu makosa ni mengi kafanya katika hotuba yake yote.

Hata hivyo hii slip of the tongue ni acceptable kabisa, kosa kubwa lipo kuwa anawakilisha entity ambayo Kimssingi, hairuhusiwi na ni kosa kubwa kutoelewa lugha ya Kiingereza hasa ukizingatia ndio lugha kuu ya maofisini ukiacha Kiswahili. Naamini kwenye 'vipengele husika' vya sifa ya mtu wa ku cover hio nafasi LAZIMA kuna kipengele kinasema mtu awe fluent in English. Sasa sababu serkali yetu inatowa kazi kwa vigezo vya kujuana, connections na upendeleo ndio madhara yake haya...

Katika aibu kwenye conference, katia aibu serkali yake then akatutia aibu na sisi hali tuna watu ni wanastahili hata wangeenda pale wangewakilisha vilivyo.

Usinichekeshe wewe AshaDii,

Nasikia enzi zile, Dr Remmy alikuwa na gari bovu bovu, basi akaandika nyuma..."Eti unacheka, baba yako analo?"

Ni ukweli ila kama kila mwanajamii angesubiri kumiliki gari ali amtoe makosa mwenye mkangafu basi ingekuwa hatari...

Lugha ya watu kweli hatuijui, hata hivyo tuna tatizo la umakini na kujiamini...Ukifuatilia sana utakuta watu wengi tunakuwa na ujuzi wa kuegesha engesha hata tukiambiwa tujieleze kwa kiswahili tunaishia kujikanyaga kanyaga....Mifano ni mingi sana na naamini unaijua!!

Lakini pia kama unavyosema....Mulugo ni kiongozi wa juu wa wizara nyeti inayoshughulika na elimu ya watoto wetu na wajukuu zetu. Kama uwezo wake kielimu unatia shaka, basi hataona shida kuvumilia wanafunzi wababaishaji na kutujanzia makanjanja mitaani.

Tabia ya kuvumilia mizaha mizaha kama hii kwenye mambo ya msingi katika hili taifa ndiyo inayotuwahisha kwenye kifo..!

Watu kama hawa, hatutakiwi kuwavumilia ukizingatia kuwa wanajaza nafasi za watu makini wenye uwezo wao ambao wanabaguliwa kwa sababu za kipuuzi kabisa (ukabila, ukanda, ufisadi, ukada n.k)!!
 
Last edited by a moderator:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom