Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,455
Wanabodi,

Kumekuwepo kwa thread mbali mbali za kumshutumu, kumbeza hadi kumkebehi Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Phillip Mulugo kwa kauli yake ya Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba!.

Naomba kujitokeza kumtetea huyu jamaa "It was only a slip of a tongue!. Yaani aliteleza tuu ulimi kunakosababishwa na adrenalin inayoleta first time panic, hii ndio mara yake ya kwanza katika maisha yake, kuhutubia mkutano mkubwa kana ule
.
Ukiangalia hii video kwenye U-Tube utaona ni PPT Presentation kupitia Over Head Projector kila neno alilotamka pia limeandikwa na kuonyeshwa na ile projector screen.

Japo ni kweli aliitamka neno Zimbabwe lakini screen ya projector ilionyesha neno Zanzibar!. Hivyo hilo neno Zimbabwe, was a slip of a tongue tuu yaani aliteleza ulimi kwa panic tuu ni kosa la kawaida la kibinaadamu!.

Kufuatia kosa hilo dogo tuu, kitendo cha Clouds Redio kumkomalia jana nzima sio cha kistaarabu na sio kumtendea haki!.

Watu sasa wameanza hata kuhoji elimu yake!. Watanzania sasa tumekuwa wagonjwa wa "paper qualifications" na ni kufuatia kosa hilo dogo, watu humu sasa ndio wanamkomalia kuhusu elimu yake!. Kwa watu wanaomfahamu vizuri Mulugo kwa utendaji wake, Kikosa hicho "It doesn't matter" kwa vile jamaa ni jembe kweli!. Nimemshuhudia akipiga mzigo wa kufa mtu!. Akifanya ziara za kikazi popote, hufanya 'surprize visit" kwenye mashule au vyuo na kuibua madudu kibao!.

Tumhukumu mtu kwa utendaji wake na sio kwa "Slip of a tongue"!.

Paskali.
NB. Kitendo cha Mhe. Mulugo kuzungumza na Clouds Radio, na kuzunguzia hili, hakina uhusiano wowote na thread hii, it was a mere coincidence!.
 
Mi hata ukiniamsha usingizini siwezi kuchanganya Zanzibar na Zimbabwe. Labda kama ningekuwa sijasoma.
 
Hapa sijui tuseme nini sasa!! sleep of brain?
 

Attachments

  • 167541_1390032369824_1802575517_750317_699599_n.jpg
    167541_1390032369824_1802575517_750317_699599_n.jpg
    21.3 KB · Views: 644
Watu sasa wameanza hata kuhoji elimu yake!. Watanzania sasa tumekuwa wagonjwa wa "paper qualifications" watu humu sasa wanamkomalia kuhusu elimu yake!. I doesn't matter jamaa ni jembe kweli!. Nimemshuhudia akipiga mzigo wa kufa mtu!. Akifanya ziara za kikazi popote, hufanya 'surprize visit" kwenye mashule au vyuo na kuibua madudu!.

Nadhani hii nayo ni "slip of a keyboard" lol. Na issue ya 11964(one nineteen sixty four) mbona haujaizungumzia Pasco?
 
Jamani hii lugha ni kigeni, hata mbuzi wana lugha yao. Wakati mowing inte ni bora tutumie Kiswahili kwenye mikutano hiyo.
 
hahah Pasco huyu naibu kasoma thread yako kabla hajaongea clouds nini? Kwani naye kasema aliteleza.. But huyu naona hafai aondoke(japo hatoondoka)
 
Mashambulizi ya wadau katika jamii kwa kushindwa kutumia lugha ngeni ya Kiingereza ndio sababu inayofanya Watanzania wengi washindwe kujifunza hio lugha kwa ufasaha kwa woga wa kuchekwa, kebehiwa na hata kusanifiwa ukikosea (mara nyingi hata wakosoaji unakuta pia lugha hawaielewi ila tu bado amcheka mwenzie). Ile sio lugha yake na wala hata makosa katika kukosea... Na ilibidi tu aweke wazi kuwa hio lugha inampiga chenga sababu makosa ni mengi kafanya katika hotuba yake yote.

Hata hivyo hii slip of the tongue ni acceptable kabisa, kosa kubwa lipo kuwa anawakilisha entity ambayo Kimssingi, hairuhusiwi na ni kosa kubwa kutoelewa lugha ya Kiingereza hasa ukizingatia ndio lugha kuu ya maofisini ukiacha Kiswahili. Naamini kwenye 'vipengele husika' vya sifa ya mtu wa ku cover hio nafasi LAZIMA kuna kipengele kinasema mtu awe fluent in English. Sasa sababu serkali yetu inatowa kazi kwa vigezo vya kujuana, connections na upendeleo ndio madhara yake haya...

Katika aibu kwenye conference, katia aibu serkali yake then akatutia aibu na sisi hali tuna watu ni wanastahili hata wangeenda pale wangewakilisha vilivyo.
 
Back
Top Bottom