Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...

Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

Hilo neno la huyo mama hali justify huo upuuzi uliofanyika, nenda shule Mr
 
Mimi bado nawashauri wale wanaosema kijana huyu wa miaka 14 ni mkubwa sawa tuwakubalie ni mkubwa. hoja ni je kwa hiyo kuna uhusiano gani kati ya kijana aliyekojolea qur an na pamoja na majibu ya mama wa mtoto na kuchoma makanisa. Hapa ndipo tulitegemea waislam hawa wanojiita wanaharakati wafikiri kwamba ni nani adui yao. Yani Shekhe ponda jina kubwa anashidwa kutofautisha kosa la mtu binafsi anashawishi waislam kuchoma makanisa. Ndio maana mnawapa credit wacristu waonekane wana akili, busara na hekima kwa jambo rahisi. Kosa la Mkristo haliwezi kuwa la wakristo vivyo hivyo kosa la muislam haliwezi kuwa la waislam wote. Tujifunze kufikiri sio kufuata upepo wa Ponda ambae hana shule, tufuate watu wenye uelewa mkubwa kama Shekhe wa Mkoa wa DSM.
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!
yule Kijana kuwa na akili Timamu au Kutokuwa nayo si tayari alikuwa mikononi mwa dola?. adhabu siingetolewa na mahakama? kwanini watu ambao hawakushuhudia wala kuwepo kwenye mazingira ya tukio watake kuhukumu?

tatizo hili ni kubwa na limejikita Kwa waislamu wenyewe (siyo uislamu). waislamu wa Tanzania kuonewa inawezekana. Lakini tujiulize maswali. wale wa Mombasa wanotaka Mombasa ijitenge na Kenya nao wanaonewa? Bokoharamu huko Nigeria nao wanonewa? huko Mali nako wanaonewa? Alshabab nao wanonewa? kwanini Vikundi vikundi vya uhalifu vingi vihusiane na waislamu?
 
hapa sasa nimeanza kupata picha kwamba si Waislamu wote ni waumini wa hizi fujo. na hata mafundisho ya kiislamu hayapendekezi fujo na ghasia. ni kweli ni tatizo la ajira na elimu
Karibu JF,nimependa post ya kwanza tu na imekwenda shule ama ni mzoefu?
 
Nadhani Mdondoaji unapoint hapa, binafsi sipendezwi na yanayoendelea huko Dar/Tz, hata hivyo ni ukweli kwamba serikali inabidi iingilie kati. Iingilie kati kutokana na yafuatayo:-

1. Nguvu za ki-ushindani wa nyanja zote(uchumi, siasa, utamaduni, ajira nk) duniani leo hii zinasimamiwa na Elimu. Ni elimu hiyo hiyo ndiyo inayoweza kutoa ishara ya Taifa/jamii flani itakavyokuwa katika kipindi flan kijacho. Sasa, tusirejee historia, tuanze hapa tulipo; turejee katika hali halisi kwa Tanzania, tuna shule (naomba niziweke katika namna tano) ; 1. Seminari za Kikiristo, Seminari za Kiislamu, Shule za Binafsi zisizo Seminari, shule za Serikali zenye performance afadhali( Mzumbe, Ilboru, Kibaha, nk) na shule za Serikali za Kata. katika matokeo yoyote ya Sekondari(O na A level, matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimi 90 ya shule za seminari za kikristo zinapata matokeo ya kuendelea hatua inayofuata ya masomo ilhali asilimia zaidi ya 90 ya seminari za kiislamu wanapata matokeo ya jumla yasiyo yenye kuendelea na hatua inayofuata. Vile kutokana na "historia" watoto wengi wa jamii za kiislam wanajiunga na shule za Kata au wazazi wao ima hawana uwezo wa kuwapeleka katika shule za binafsi kutokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya jamii ya kii-islam wana maisha yasiyowezesha kuwapeleka shule hizo,au wanahitaji government intervention ya kuwapeleka katika shule binafsi; most likely ratio ya <10:90> inaendelea. Kwa kuwa mfumo wa elimu wa sasa, ni market based system na wazi kuwa jamii moja imeshindwa kucheza na market-based system hii, kanuni za kiuchumi zinabainisha government intervention inapotokea market failure imetokea. (Naomba niseme kuwa kuna market failure katika mfumo wa elimu uliopo baina ya waislam na wakristo hivyo si suala tena la kusema 'wenyewe hawataki kusoma' bali Serikali iingilie kati kwa kukusudia kuiondoa hii 10% ya wakristo wanaobaki uraiani na kuipunguza hatimaye kuiondoa hii 90% ya waislam wanaobaki uraiani. Serikali pamoja jamii ya kikristo ifanye yafuatayo ili kusawazisha tofauti hizi.
1.Kuanzishwe "Islamic Society enhancement programme" inayolenga kuongeza idadi ya watoto wa jamii ya kiislam kupata elimu kwa kuimarisha uwezo wa Shule zao, maabara, na waalimu hata ikibidi kuongeza idadi ya shule hizo na kulipa mishahara ili kupata waalimu watakao-stabilize katika shule hizo.(nimesema jamii ya kikristo inabidi ikubaliane na hili kama intervention kwa market force imefail, hivyo wasomi wa kikristo walielewe hili).
2. Ufanyike utambuzi wa uwezo wa kitaaluma kwa watoto wote ambao ni kweli wako katika mazingira magumu then serikali i-subdize waweze kusoma katika shule either za seminari, binafsi au serikali zenye viwango vinavyoendana na uelewa wao
3. Serikali ipige marufuku tamaduni za kucheza ngoma na sherehe za kipuuzi za namna hiyo.
Nitaendelea.....

Ndgu mchango wako umekosa mashiko kidogo kuna baadhi ya mambo ilipaswa uyaangalie kwa undani kidogo,
Moja ni malezi ya familia kwa muislam yakoje kwani hili limesabisha kwa watoto wengi wa familia za kiisalam kukosa haki za msingi kama hiyo elimu na familia chache zilizo staarabika na kuelimika ndizo zinafikia mafanikio na watoto wao kuwa na maisha mazuri

Hili mara nyingi linasabishwa na Mzazi mmoja kuwa na familia kubwa pasipokuwa na uwezo wa kuimudu kwani kwa maisha ya sasa kila kitu ni gharama katika kugharimikia familia na watoto kupata elimu bora na utofauti katka hili ni kama ulivyoeleza katika kipengele kimoja hapo juu ni kuhsu uchumi kwani nchi za kiarabu ambazo zina waislamu wengi serekari huwa wanatoa huduma zote kama elimu,afya na mitaji bure kitu ambacho hapa kwetu hatuna na kuna chama kilikuja na sera za elimu bure kikapandkiziwa udini nakusema haiwezekani kutoa elimu bure na hili la uchumi na elimu bure ni tatizo la kila mtu sio la waislam tu.

La pili ni kujiuliza kwanini hizi islamic seminary zinshindwa kufanya vizuri kwni kwenye usahihishaji mitihani inasahihishwa kwa namba na sio jina na wasahihishaji ni wa Dini zote,hebu tujaribu kuangalia wenzentu wanafanyaje kama ni walimu bora na mishahara nasisi tuweke na kama kutafuta cream kwa kujiwekea percentage kwa mwanafunzi anaefikisha alama zilizowekwa anaendelea a asiefikia anashauriwa atafute vyuo vya ufundi au kitu kingine mbadala na sisi tufanye hivyo ila tukumbuke kuwa katika yote msingi mzuri unaanzia shule za awali,pia ya tupasa kujua katika katika baadhi ya hizo seminary za wasiokua waislam na waislam wanaruhusiwa kusoma

La mwisho kwa mtazamo wangu waislam tujishughulishe na kuacha kulalamika tunaonewa na kama kuna haki inayopindishwa kwa sababu ya uislamu wetu mbona vyombo vya sheria vipo, na kama ukihitaji kila mali kwenye utawala awepo muislam hebu tujiulize lengo letu ni nini? Kumbukeni asili yetu hatukua na dini haya yote yameletwa na wazungu na waarabu, ndugu zangu waislam tudumishe mshikamano wetu tuachane na mambo yanayotaka kuvunja mshikamano wetu
 
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

Mkuu free world.

Kwanza kabisa kwa heshima na taadhima naomba nikuambie kuwa hakuna kundi/kikundi kilicho nimezesha propaganda ambazo unasema "zina enezwa na maadui juu ya lile tukio" hapa umeamua kuwa msemaji wangu kwa kujiwekea maneno mdomoni na kuyatapika mwenyewe.

Lakini pili, umesema "maadui juu ya lile tukio" hapa sijakuelewa kabisa kuwa adui wa tukio unaye msema wewe ni nani? Hujawa muwazi kueleza kuwa maadui ni wapi maana umetoa lawama za jumla.

Kwangu mimi mpaka kadhia ile inatokea naweza kuitafsiri hivi.

1. Mtoto wa kiislamu ni mtuhimiwa namba moja.
Kwa nini?
. Yeye amempa mwenzake vitisho vya kumshawishi akojolee qu-ran (asinge ongea mambo yaliyo mjengea mwenzake ujasiri wa kukojolea qu-ran nina uhakika tusingekuwa tunaongea haya leo. Mtoto wa kiislamu alikosa hekima na busara za kuto kukitia kitabu kitukufu kwenye majaribio. Huyu adhabu yake ilipaswa awaelimishe watoto wenzake wasirudie tena na watambue umuhimu wa kuheshimu vitabu vya dini.

Lakini pia anapaswa afunge siku kumi kwa kuihusisha qu-ran na ushirikina (rejea kauli yake kuwa 'ukikojolea qu-ran una geuka mjusi).

2. Mtuhumiwa namba mbili angekuwa aliye kojolea Qu-ran huyu kwa namna moja au nyingine hakupaswa kabisa kukojolea kitabu kitukufu maana tayari alisha jua kuwa ni kitabu kitukufu. Adhabu yake huyu ni kumfuunza asiwe mjeuri siku nyingine na anatakiwa kuheshimu vitabu vya dini nyingine kama anavyo heshimu vitabu vya dini yake.

Hata hivyo, niungane na wewe kwa haki kabisa kama ulivyo sema "waislamu si wajinga" lakini lazima ukubali kuwa miongoni mwa waislamu werevu kuna idadi chache ya wajinga wasio kuwa na hekima na busara za kiislamu (mfano kuvunja makanisa na kuiba kompyuta au sadaka)huu hauwezi kuwa werevu kwa muislamu wa haki.

Mkuu. Wanaodharau dini yetu dawa yao sio kuwachomea makanisa au kuwakata kwa majambia! Hawa wanahitaji kuelimishwa kwa hekima na busara ili waone upande wa pili wa makosa yao ya kudharau dini ya wengine, lakini pia wanatakiwa wajifunze kupitia matendo mema miongoni mwetu sisi waislamu ambayo matendo hayo yana dhati ya utamaduni wa kiislamu na imani ya matendo yaliyo jaa mshikamano wa upendo, subra na hekima za kiislamu.

Wabilaah tawfiq.
Salaam alykum.
 
kama wewe ungekuwa Pilato na jambo hili limeletwa kwako ungebariki liwe kama lilivyotokea?
 
Asante Maggid, lakini unapaswa uelewe kuwa tatizo halikuwa mkojo...kuna kitu kilichofichika zaidi ya mkojo wanachodai ndugu zetu. Mkojo ni kisingizio tu! Hebu tuambiane ukweli kuwa kinachotakiwa pale ni utawala wa dola.
 
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'

Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!

Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!

Mngempuuza huyo mama na huyo dogo Mngepengukiwa nini? Mungu wenu asingebaki kuwa Mungu? Mtume wenu asingebaki kuwa mtume? Swala zenu zisingesikilizwa? Tumieni akili sometimes
 
Mkuu free world.

Kwanza kabisa kwa heshima na taadhima naomba nikuambie kuwa hakuna kundi/kikundi kilicho nimezesha propaganda ambazo unasema "zina enezwa na maadui juu ya lile tukio" hapa umeamua kuwa msemaji wangu kwa kujiwekea maneno mdomoni na kuyatapika mwenyewe.

Lakini pili, umesema "maadui juu ya lile tukio" hapa sijakuelewa kabisa kuwa adui wa tukio unaye msema wewe ni nani? Hujawa muwazi kueleza kuwa maadui ni wapi maana umetoa lawama za jumla.

Kwangu mimi mpaka kadhia ile inatokea naweza kuitafsiri hivi.

1. Mtoto wa kiislamu ni mtuhimiwa namba moja.
Kwa nini?
. Yeye amempa mwenzake vitisho vya kumshawishi akojolee qu-ran (asinge ongea mambo yaliyo mjengea mwenzake ujasiri wa kukojolea qu-ran nina uhakika tusingekuwa tunaongea haya leo. Mtoto wa kiislamu alikosa hekima na busara za kuto kukitia kitabu kitukufu kwenye majaribio. Huyu adhabu yake ilipaswa awaelimishe watoto wenzake wasirudie tena na watambue umuhimu wa kuheshimu vitabu vya dini.

Lakini pia anapaswa afunge siku kumi kwa kuihusisha qu-ran na ushirikina (rejea kauli yake kuwa 'ukikojolea qu-ran una geuka mjusi).

2. Mtuhumiwa namba mbili angekuwa aliye kojolea Qu-ran huyu kwa namna moja au nyingine hakupaswa kabisa kukojolea kitabu kitukufu maana tayari alisha jua kuwa ni kitabu kitukufu. Adhabu yake huyu ni kumfuunza asiwe mjeuri siku nyingine na anatakiwa kuheshimu vitabu vya dini nyingine kama anavyo heshimu vitabu vya dini yake.

Hata hivyo, niungane na wewe kwa haki kabisa kama ulivyo sema "waislamu si wajinga" lakini lazima ukubali kuwa miongoni mwa waislamu werevu kuna idadi chache ya wajinga wasio kuwa na hekima na busara za kiislamu (mfano kuvunja makanisa na kuiba kompyuta au sadaka)huu hauwezi kuwa werevu kwa muislamu wa haki.

Mkuu. Wanaodharau dini yetu dawa yao sio kuwachomea makanisa au kuwakata kwa majambia! Hawa wanahitaji kuelimishwa kwa hekima na busara ili waone upande wa pili wa makosa yao ya kudharau dini ya wengine, lakini pia wanatakiwa wajifunze kupitia matendo mema miongoni mwetu sisi waislamu ambayo matendo hayo yana dhati ya utamaduni wa kiislamu na imani ya matendo yaliyo jaa mshikamano wa upendo, subra na hekima za kiislamu.

Wabilaah tawfiq.
Salaam alykum.

Mkuu kwanini usitenge muda wako ukawa unawaelimisha wenzio? Nina hakika utapata thawabu kubwa sana kwa mola wako
 
Maggid,

As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.

Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.

Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!

Nilikuwapo!!!!

Mdondoaji,
Katika kisa cha Bedui aliyekojoa msikitini alichoeleza Maggid umeweza kufafanua zaidi kuwa alikuwa amelewa. hii inamaanisha Mtume Muhammad alipowazuia maswahiba wake na kwenda kumhoji bedui yule aliweza kugundua kua alikua amelewa, maana yake ni kwamba Mtume Muhammad alimpa BENEFIT OF DOUBT kabla ya kumhukumu, na akamsamehe baada ya kugundua alikua amelewa. Ajabu ni kwamba unapokuja kulinganisha kisa hiki na tukio la Mbagala unasahau kutoa BENEFIT OF DOUBT, ambayo hata Mtume aliitoa kwa bedui, badala yake unaamua KUHUKUMU moja kwa moja kuwa mtoto yule wa miaka 14 alikuwa na akili zake timamu (hajafanyiwa vipimo vyovyote) wakati akifanya kitendo kile, na pia hutoi mawazo yako juu ya nini kilipelekea mtoto yule kufanya kitendo kile. Nadhani ungekubaliana na Maggid, kwa maoni yangu analiangalia suala hili kwa jicho la tatu.
 
Duuuu yaani kumbe thamani ya Qurani ni sawasawa na Makalio? nilikuwa sujui nilifikiri Qurani ina hadhi kubwa zaidi kumbe nilikuwa najidanga thanks for clarification
Ndio tatizo la makafiri! Sasa kama mtu unaweza pigana kwa ajili ya makalio ya mkeo, kwa nini usipgane kwa ajili ya neno la Mungu?
 
Ndio tatizo la makafiri! Sasa kama mtu unaweza pigana kwa ajili ya makalio ya mkeo, kwa nini usipgane kwa ajili ya neno la Mungu?

Mungu wenu kama yupo hai na ananguvu haitaji umpiganie anao uwezo wa kujipigania mwenyewe lakini mke ni dhaifu lazima umpiganie asidhalilishwe vp na Mungu wenu ni dhaifu kama Mke????????? Ndo tatizo la kuishia madrasa tu ungekuwa walau umefika darasa la saba tu ungeweza kuiona hii tofauti!!!!!!!!!!
 
Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.

Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.

Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.

Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.
Nilidhani utaanza kumuelimishaira aliyochafua majjid then ndio umalize na majjid juu ya hadhithi yake aliyoileta then kaitafsiri anavyojua yeye!!!kumbe na wewe ni walewale tu.Anza kwanza kusafisha mazingira then ndi umalizie na hayo unayoyasema.
 
Ndugu zangu,

Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765

Maggid I cant believe unaweza fanya kazi sawa na hawa waliochoma kupiti akalamu yako.Hiyo hadith inasaidia nini kama kuna hadith nyingi zaidi zinazoweza mpa kiburi kijana wa kiislam anapofaya huu uovu?

Maggid ulichoandika hakina conclusion wala ukemeaji, wala kuwajibika wewe au kuiwajibisha jamii yako.Kwanini utumia hadith moja ambayo waislam wanaweza kuuliza kwanini unataka wao wachague hiyo hapo juu wakati wana nyingi na nziro kwa nia yao?Kwanini upindishe ukweli ili kuficha makosa ya dini yako na si kujiuliza maswali ya msingi?Kwa tunaolewa mambo tunaona wazi kwamba unapunzuga makali ili kuwanusuru walio wako kwa hasara ya makafir.Kwa kiasi fulani umetimiza kile walichofanya watawala wa kiislam ktk serikali kwa kusema kuwa wale ni wauni, wengine ni issue ya Muungano, na wengine kuwa uislam haufundishi hayo.MItaani humu kila muislam anacheka kirohoroho.Tunjaua uongo unarudhurisiwa ktk uislam ili kumpotosha adui,lakini kw aufahamu wako wa universala values hujaweza jiuliza maswali ya msingi kuhusu dini yako na mahusiano yake na dunia?Hujaweza chambua mistari na kutambua vitu ambavyo logically si true.Sasa kama huajaweza ona hayo yote ya nini sasa unapoteza muda na elimu dunia kiasi hiki?Utamshauri nani sasa kitu chenye maana kama uandishi wako haujakuwasaidia ona mambo yasiyo sawia ktk dini yako?

Kama unafiki ndio sehemu ya maisha yako,kwanini basi tusiamini wachangiaji humu wanayosema linapokuja suala la siasa na uzalendo wa nchi?

Nadhani unahitaji kwenda mbali sana ktk hoja zako, na kujenga maridhiano dhaifu kama haya.Waislama wanachoma na kuendelea choma na kutamani sana kuingia ktk ugaidi kabisa.Sasa unatuletea sijui vijana wa dini zote wasio na kazi na blah blah nyingine...Kwani umesikia lini wasio na kazi ktk Ukristu wanchoma misikiti?Ongea issue halisi ndugu yangu na si haya matapishi.Umefanya kazi yako kuupamba uislam, sasa wenyewe unajichafua,badala ya kujiuliza msuala ya msingi unaleta uzembe wa fikra kiasi hichi.Unatama umaarufu wa amani kwa wale wanachukua amani ya wengine.
 
Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.

Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.

Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.

Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.
Nilidhani utaanza kumuelimishaira aliyochafua majjid then ndio umalize na majjid juu ya hadhithi yake aliyoileta then kaitafsiri anavyojua yeye!!!kumbe na wewe ni walewale tu.Anza kwanza kusafisha mazingira then ndi umalizie na hayo unayoyasema.
 
Nilidhani utaanza kumuelimishaira aliyochafua majjid then ndio umalize na majjid juu ya hadhithi yake aliyoileta then kaitafsiri anavyojua yeye!!!kumbe na wewe ni walewale tu.Anza kwanza kusafisha mazingira then ndi umalizie na hayo unayoyasema.

Mr Mzumbe.
Unadhani kwa mchango wako ume-add value kwenye hii hoja?! Kama kuna mapungufu kwenye michango yangu kwa nini wewe usije na kasha la nyama ili wiiongezee i-none kama ulivyo dhani kuwa ikiwa namna unavyo taka wewe ingekuwa mujarabu?!

Umeshindwa kuutumia u-great thinker wako ukaamua kupiga msele na kusepa.

Karibu tena.
 
Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.

Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.

Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.

Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.

kwani haya mahubiri huwa hamyatoi miskitini? Au ni kwa ajili ya kutuliza makafiri tuu wanapochafuliwa hali ya hewa na hao watu wachache wenu?mbona wanatosha sana kufanya sizable distructions ya nini sasa na wengine waingie?Kwanini mara nyingine msiwe watu kwa dkk chache nyugu yangu?Mkiwa watu kidogo mtaona hizi blah blah zinapunguza nguvu ya watu kuwawajibisha hawa hooligans.Sasa ni Jukumu lenu waislam nyie mnaodai kuwa wachache wanaoichafua dini , muache kutumia wingi mnaotuzuga nao kuisafisha hiyo dini huko huko kwenu na si kwa wengine.Nyie ndio mkawakamate hao wanaochafua dini kama mnavyokuwa busy kuwaua na kuchoma makanisa na bendera za wengine ili kumaliza hasara za wanaoudhalilisha uislam.Sasa inakuweje hamuwezi wawajibisha hao wanaouchafua uislam wakati nyi emnautakatisha.Mkifanikiwa hili bil aunafiki mwingine kuwa mnagombanishwa na makafir basi naahidi kuwa muislam.
 
63 Reactions
Reply
Back
Top Bottom