Ya Manyara yahamia Ngara!

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
14
Wajameni, salamu kwenu. Ni imani yangu kuwa wote tumeamka salama.

Kuna tetesi kuwa jana kulizuka ugomvi kati ya mkuu wa wilaya ya ngara vs mwandishi wa ITV hali iliyosababisha wananchi kuondoka kikaoni baada ya wananchi kuomba mwandishi wa ITV asitolewe nje na OCD kama agizo la mkuu wa wilaya. Lakini mkuu huyo alikataa na kuwaambia wanaomtaka mwandishi waondoke nae na wengine wabaki!

Mamaa weeeee, watu wote wakaamka na kuondoka kikao kikafikia mwisho kwa style ya ngumi za tyson ....knok-out!

Wenye habari watuhabarishe!

Source: Itv news jana usiku 20:00EAT
 
Hawa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa mara nyingine wana ubabe usiokuwa na tija
 
Hawa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa mara nyingine wana ubabe usiokuwa na tija

.
Sina uhakika sana kama huyu mkuu wa wilaya nae mwanajeshi. Ila ninachofahamu wingi wa wakuu wa wilaya na mikoa ni kijjiwe cha mapumziko ya mwisho ya wastaafu hasa wanajeshi. Na kwa wingi wao . elimu haikuwa kipaumbela ktk zama zao. Sasa unaweza ukaona hatari ya wazi inayolikabili taifa ya matumizi ya nguvu badala ya akili na busara. Unaweza ukamlazimisha ngombe kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Hii ni sawa na kuwalazimishia watu madaraka lakini hawana uwezo wa kukabiliana na changamoto za teknolojia ya wakati. Tukubaliane kwamba hilo halilazimishwi.
 
Back
Top Bottom