ya kipara na DARUSO aibu kubwaaaaaa.... WANAHARAKATI washindwa kutetea ukweli

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Huyu Kipara aka Kipara aka Kipara ndio aibu kubwa ya mwaka huu kwa UDSM...

Chuo hiki kinafahamika kwa mihemuko ya kisiasa hapa nchini lakin mamluki lukuki wameamua ku-dilute ile DARUSO tunayoijua...

Madai ya wanafunzi ni mengi tuu lakini pale UDSM kumekuwa chuo cha kata kuliko hata UDOM ilivyo... Mimi nitaelezea machache niliyohabarishwa na wadau wenzangu..

1. Madai ya msingi ya upungufu ya malazi na wanafunzi wanatetseka lakini DARUSO haijatambua wala kushughulikia hilo...
2. Madai ya msingi kuwa "BOOM" Halitoshi na gharama nyingine
3. madai ya kuandikishwa na NHI na utambulisho wao mwka wa 2009/2010.. wengi hwakupewa kitambulisho lakini hela zao hawajapata kabisa... licha ya wengi kulalamika...
4. Madai ya ufisadi na wizi ndani ya DARUSO kutokana na mapato na matumizi ya DARUSO kutokuwa wazi siku zote toka kipara na yule mtangulizi wake waingie madarakani... Kuna ombwe kubwa lauwajibikaji na ukuzaji wa mafisadi watoto
5. Masikitiko yangu ni DARUSO kujiunga TAHLISO wakati watangulizi waliona fika jinsi gani TAHLISO iliweza kuiba haki za wanafunzi na kukumbatia ufisadi wa watoto ambao tunapiga vita kabla hatuajaunda akiana EL na RA wapya... Inaaminika KIPARA alijiunga bila baraka hata ya rafiki zake ambao woote wamenukuliwa wakikana kushiriki huku wakishangaa kwa KIPARA kuwa mwenyekiti wa TAHLISO kwa kuwa wanaamini hiyo ndio rushwa waliyompa ili alainike kirahisi...
6. Uongozi mbovu ambapo inaaaminika kuwa mawaziri watatu walidisko kwa sababu ya ulevi na uchu wa kutumia bila idhini ya wanafunzi na "laana" ya Mungu.. Mimi pia natoa laana zangu binafsi kwa kuwa hii sio DARUSO ya kina-wanaharakati tunaowafahamu
7 .Kuna tetesi mtaani na chuoni pale kuwa KIPARA aliingia madarakani kwa gharama kubwa ya zaidi ya mil 5... ikiwa message special kupitia ZAIN na picha kibao, rushwa, CCM, wizi wa kura na ushabiki mamluki na msaada kutoka kwa kina OWAWA na SILINDE ambao walipigwa danganya toto wakampigia chapuo bila kugundua kuwa mwenzao ni mamluki...

Haya yooote yamelelewa na KIPARA pamoja na serikali yake mamluki ambayo ndio sindano ya maumivu na uchungu mkubwa...
TAHADHARI:
Wabunge wa DARUSO wapige kura ya kutomwamini Raisi ili uchaguzi ufanyike upya...

Nawasilisha!!!
Baadae
 
Najua kuna wanafunzi wa UDSM hapa jamvini ngoja waje watupe ukweli wa madai yako kwani na wewe unaonekana huna uhakika na ulichokiandika kama ni kweli!!!!

Tiba
 
Japo sipo UDSM lakini kwa kiasi kikubwa matatizo hayo hapo na ni madai ya msingi kabisa,lakini hayakifanyi chuo hicho kuwa cha kata.Tatizo kubwa liko upande wa wanafunzi wenyewe,utawala wa chuo na serikali kwa ujumla.

Kwa upande wa wanafunzi;wanafunzi wengi wa UDSM ni waoga na wanaojali zaidi madesa kuliko haki zao za kimsingi kama vile kupata sehemu za kuishi.Unaweza kuona jinsi mtoa mada anavyolalamika bila kuchukua hatua,matatizo hayo yapo chini ya wanafunzi wenyewe.Kwa uzoefu wangu katika chuo hicho,uongozi wa chuo hauwezi kuwasaidia wanafunzi bila shinikizo na hiyo imekuwa desturi.

Pili,inasikitisha kwamba na ninyi wanachuo mnaingia kwenye mkumbo wa ushabiki wakati wa uchaguzi,badala ya kuchagua wanaharakati,watu wenye misimamo isiyoyumba,mnawachagua viongozi kwa sababu ya kuwa na poster za picha nyingi na mambo mengi ya kipuzi.Kama wanachuo mnafanya makosa kama hayo,vipi wananchi wa kawaida huku mtaani?Mnatia mashaka na hizo elimu zenu.

Tatu,kwa mara nyingi zaidi,uongozi wa chuo umekuwa ikiingilia michakato ya uchaguzi kwa kuwaweka mamluki ambao watakuwa na misimamo dhaifu,mifano ni mingi sana tangu enzi na enzi.Kama mnafuatilia,uchaguzi wa kumtafuta rais 2008,uongozi wa chuo walihakikisha mgombea urais ODONG raia wa Uganda hapati nafasi,mwisho wa siku hata serikali ikaingilia kati na kusema mgombea huo hakuwa na kibali ha kuishi hapa nchini.Tumeona jinsi akina OWAWA walivyotendewa na uongozi wa chuo na kuwafungulia kesi hewa,ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni shinikizo kutoka serikalini.

Serikali inakiona UDSM kama chama cha upinzani,wamekuwa wakitumia kina aina ya vitisho,manyanyaso na mambo mengi yasiyo na utu.Kwa makusudi kabisa serikali imeamua kupoteza historia kabambe ya chuo hicho,ndio maana badala ya kujenga hostel za kuishi wanafunzi,wanajenga mashoprites na mambo mengi ya kishenzi.Na serikali inahakikisha inaweka mkuu wa chuo (vice councillor) ambae ni mtu wao kama vile Mukandala,hawataki kuwaweka watu wenye msimamo usioyumba kama vile Luhanga.

Nihitimishe kwa kusema,pamoja na matatizo yanayowakumwa Udsm,ni lazima wajisaidie wenyewe.Wawe na movement za uhakika za kudai haki zao.Huo rais kibaraka ambaye mie namfahamu vizuri sana,hawezi kuwashindwa kumng'oa.Kwanza ni kutumia njia ya kidemokrasia ikiwemo bunge kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kama ambavyo katiba ya DARUSO inavyosema.Hilo likishindikana lazima nguvu ya umma itumike.Wasiojua ugumu wa vyuo vyetu,wanaweza kuona ushauri huu hauna maana,lakini bila nguvu ya umma watawala hawasikii wala kuona.Wewe uliyepost htread hii,jitahidi ku-organise wenzio mfanye vitu vya maana kuliko kukimbilia JF,ACHENI UOGA,UREMBO NA MAMBO MENGI YA KITOZI YA KUSHINDA ROOM KUSIKILIZA MUZIKI BADALA YA KUWA NA MUDA WA KUTOSHA WA KUSOMA NA KU-ACT
 
kwa hiyo unaleta huku ili sisi tufanye nini? Ulitakiwa uandae kunji kisha kisha wakati kunji linapamba moto ndo utuandikie haya kutueleza kwa nini mmeanzisha kunji. Pumbafu kweli wewe, halafu unauliza wanaharakati wako wapi? Wewe unafanya nini?
 
kwa hiyo unaleta huku ili sisi tufanye nini? Ulitakiwa uandae kunji kisha kisha wakati kunji linapamba moto ndo utuandikie haya kutueleza kwa nini mmeanzisha kunji. Pumbafu kweli wewe, halafu unauliza wanaharakati wako wapi? Wewe unafanya nini?

Hapa tumeandika haya kama mambo ya msingi kabisa... Kunji tulishatayarisha kabisa(mojawapo ya mada ni kumng'oa raisi aliye madarakani) lakini watu kama KIPARA na wenzake wamekuwa wakiweka kigugumizi hatari na woga... Sasa naona madai yamekuwa nuksi kabisa!! Watu walitaka kudai malazi mapya kwa nguvu lakini DARUSO imekuwa kikwazo kikubwa... Tayari kuna wanaharakati wamewekwa katika kitimoto si na UTAWALA bali ni "kautawala" uchala cha DARUSO... Ambao wamewatangazia wanafunzi wasije REV SQUARE for any how... Wale wanaharakati wamekuwa wakimpinga saaana huyu raisi wa DARUSO lakini movement bila REV SQUARE haiwezekani kabisa... Thread kibao za kuamsha hisia tumeweka katika kuta za madarasa karibia college zote lakini DARUSO na vibaraka wachache wamekuwa waoga wa wivu na wapenda starehe lukuki... Madaraka dawa jamani sio kulala na kusikiliza ndomboro...
Wengine tuko pembeni sasa tunawaaachia madogo wakae na vibaraka vyao ili mradi wanateseka zaidi wao nasi tunakipa zetu kwa mbaaaali....

Nawasilisha
 
sasa ndo hapo mkubali kila taasisi ya govt kuna mamluki wanaokwamisha movement za maendeleo.
 
Back
Top Bottom