Ya Kandoro inatisha... Ajiuzia gari la TZS milioni 300 kwa milioni 2 tu!

atabadilishaje kadi asipolipa kodi au akimuuzia mtu mwingine si lazima alipe hizo kodi?

siku moja nilishuhudia jamaa wa polis intepol, walikamata gari walipohoji kadi yake walibewa kuangalia chesis no. Kwenye kadi ilikuwa ni tofauti na kwenye gari enyewe. Aliambiwa ni la wizi, akanza kujitambulisha nilinunua serikalini na kadi hii ndiyo niliyopewa. Sina kadi nyingine. Alipelekwa polisi lakini aliachiwa na gari lake akaondoka nalo.
 
TZ inajengwa na wenye MOYO na kuliwa na wenye MENO.

Poleni sana, jikusanyeni kupinga ufusadi huo kama ni kweli na wala si majungu.
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mteule wa JK mh. ABASI KANDORO, amefanya kufuru ya mwaka kwa kujiuzia gari la kifalme lililogarimu wavuja jasho zaidi ya milion 300/= ambalo wanaharakati tumekuwa tukiyapigia kelele kwa pesa za kitanzania Tsh. 2,000,000 tu.

Gari hilo ni VX TOYOTA LANDCRUISER, LENYE SPEED MITA 240, namba za usajili STK 3643 lililonunuliwa na mtangulizi wake kwa matummizi ya OFISI YA MKUU WA MKOA wa Mwanza.

Gari hilo lililonuliwa na mkuu wa mkoa kabla ya Kandoro bado ni mpya na hali yake ni nzuri sana, wala halijamaliza hata miaka 10 likitumika.

Baada ya kandoro kufika mwanza, alilikataa kulitumia na kusema kuwa halifai kuwa la mkuu wa mkoa na hivyo alitenga fedha la kununua gari lingine la kifahari zaidi LANDCRUISER V8, BEI MILLION 400/= speed mita 260 ambalo ndilo analolitumia mpaka sasa.

Baada ya kununua gari hilo la kifalme, gari la awali lilipewa namba za serikali STK 3643 na kupaki kwenye ofisi za mkoa na mara chache sana kutumika mkoani.

Ndipo Mh. Abasi kandoro akaunda mbinu za kujiuzia gari hilo alilolikataa kwa madai kwamba halifai kuwa la mkuu wa mkoa, akijiuzia kwa Tsh. 2,000,000/= milion mbili pesa za kitanzania.

Kwa sasa yuko kwemnye hatua za mwisho za kupata kibali, ili aondoe hiyo STK, na kubandika namba za kiraia anze kula maisha na gari hilo la kifahari lililogarimu pesa za walipa kodi karibu au zaid ya 300,000,000/= na kuuzwa kwa bei ya kifisadi 2,000,000 tu.

Nawasilisha tafadhali.




unaelewa maana ya Depreciation?
 
Bwana Nhengolo weka mambo hadharani, je hakukuwa na taratibu zilizofuatwa katika mauziano haya. kama sivyo weka mabo hapa jamvini mimi nianze kazi kesho.
 
mtoto wa mama ..... Wewe unajua nini zaidi ya kula na kulala bure ...... Ha haaa haaaaa

jibu lako saizi yake mtoto wa mama. Hafikirii kesho. Akila leo yeye kamaliza mchezo, hawazi kuwa atakuja kuwa na familia yake mwenyewe na wanawe watadai kula kama yeye anavyokula kwa mama yake.
 
OK MIU.MI NI MJASILIA MALI NAJITOLEA KUREJESHA HIYO MILIONI MBILI NA LAKI TANO KAMA FIDIA KWA MUHESHIMIWA KANDORO ILI TUWEZE LITUMIA KWA SHUGHULI ZA AFYA.HIVI NI KWELI SHANGINGI KUUZWA BEI HIYO HATA KAMA CHAKAVU?NA KILOMETER 250000 NI UCHAKAVU KWELI?GALI LINATUNZWA NA SERIKALI KWA GARAM ZA JUU LEO LISIFAE?NA HIYO DISPOSOR POLICY INATAKIWA KWA MAGALI YA VITENGO AMBAYO UTUMIKA KWA MATUMIZI MENGI NA PENGINE BILA MATENGENEZO YAKINIFU.HAPO NAOMBA MWONGOZO WA Ngd SPK.
 
Watanzania tupunguze majungu tufanye kazi. Kila taasisi ina kitu kinaitwa "Disposal Policy" kwamba gari likifikisha Kilometer/miaka flani linauzwa linanunuliwa lingine. Wengi hutumia Kilometer 250,000 au miaka mitano. Hata kama gari lilinunuliwa kwa 300 million baada ya kutumika miaka mitano thamani yake haitabaki kuwa 300 milion tena kutokana na uchakavu ambao utakuwa umekadiriwa kuwa 60 million kwa mwaka kama Policy yao ni miaka mitano.

Ila kwa swala la kuuzwa 2 million, kama ndio bei iliyopatikana kwa ushindani "Tender process" bado mtu hawezi kuhoji. Ila kabla ya kutangaza tender ilitakiwa gari hili lifanyie "valuation" kujua market value na hivyo lisingeweza kuuzwa chini ya "market value

Hayo usemayo sidhani kama kuna mwanafunzi wa primary school humu ndani wa kumfundisha; process za disposal ya mali ya UMMA zinajulikana. Sasas wewe Kandoro hebu wajuze watanzania ni lini Tenda ya Kuuzwa gari hilo ilitangazwa watu waka place bid na wewe ukashinda tenda kwa Millioni Mbili? Mweka mada hajaweka details na hali ya hiyo gari wakati inauzwa, lakn kwa imani yangu hiyo gari haizidi miaka kumi, na kwa kuwa ni ya serikali naamini pia service record zote ziko safi; hivyo pia uwa garagaza hiyo gari hata mimi mlalahoi ningejipigapiga na kukopa hata milioni 20! WEZI WAKUBWA NYIE!
 
Kandoro si wa kwanza kufanya hivyo huo ni utaratibu wa kawaida tu kwa viongozi wengi hasa wa serikali kuu na Taasisi mbalimbali kujiuuzia magari ya thamani kubwa kwa bei sawa na bure.

Tena hizo milioni 2 za kandoro ni nyingi sana kuna watu wananunua GX kwa laki tisa (900,000/=) tu, yaani ufisadi ni mkubwa sana serikali kuu na kwenye taasisi za serikali ila chakushangaza watu wanapiga kelele kuwa halmashauri zinaongoza wakati sio kweli, asilimia kubwa ya wizi kwenye halmashauri ni chini ya milioni 10 tu.

Taratibu hizo zisizo za kawaida tunatakiwa kuzipigia kelele na kuhakikisha zinakoma, Hata tuhuma za Jairo, Luhanjo anasema ni kawaida Tukomeshe hiyo Kandoro awajibishwe au awajibike
 
Nyambala, hakika tuko pamoja! Huyo mtoa taarifa atujuze hilo Landcruiser la 300m ni toleo la mwaka gani? Maana taarifa inadai kuwa halijafikisha hata miaka 10 likitembea, kwa maana kwamba angalau limetembea miaka zaidi ya 5. Ikumbukwe kuwa kwa viwango vya magari hususani Toyota, gari likitembea miaka 5 be it in Tanzania or elsewhere, thamani yake inashuka almost to 0.
Sina nia ya kumtetea Mhe. Kandoro, ila lazima nasi tujaribu kuwa makini na baadhi ya habari zinazowekwa hapa jamvini na tuchangie bila ushabiki wa kiitikadi....
Mkuu, fafanua hapo kweye red, onesha formula unayotumia kukokotoa! au unaongea tu kama mtoto mdogo? SHAME ON YOU!
 
Hao ndio watawala wetu Ma-Kada CCM na tabia za KIFISADI zinazowapanda ghafla kama wanga. Hiyo ndio CCM tafuna nchi!!!!!!!!!!!!
 
How could a car when new costing 300mil and at disposal 2m, just after five years, Ni ukweli kwamba huu utaratibu ni wa kawida sana serikalini, unasema mambo ya tender wakati hata wafanyakazi wa chini huwa hawajui ni lini hayo magari huuzwa? Iweje kila siku wakubwa tu ndo wawe wanayanunua? Hata kama kuna ubovu wa barabara lakini unajua magari ya minadani toka japan yanauzwaje tusitaniane? Priority ingekuwa kwa wadogo ningekubali lakini walewale wenye uwezo wa kununua ma brand new ndo kila siku wanashinda hizo tender????!!! kuna dereva mmoja alipata bahati ya kununua mkonga kwa Mil. 3 kuja kuchunguza kumbe alikuwa anamuendesha Katibu mkuu, Wanunue double cabin hilux 2.8 wakiuza kwa mil 2 sio mbaya.
 
Suala hilo ni zito na hakuna wa kumbana Kandoro. Nasema hivyo kwa sababu serikali yote ya CCM imeoza kuanzia juu kabisa. Nani angeweza kufanya hivyo leo akaendelea kuwa madarakani iwapo serikali yetu ingekuwa makini?
Hatuna serikali makini na utashangaa wale wanaoibua hoja kama hizo kama wako kwenye system ya Kandoro au serikali wakachukuliwa hatua kali na ikiwezekana kufukuzwa kazi.
Hii ni dalili ya wazi ya ufisadi nchini na Mungu atuhurumie.
Watanzania jinsi tunavyozidi kujadili bila kuchukua hatua ndivyo mambo yanavyozidi kuharibika.
Kwa nini tusiamue kuwang'oa hawa watawala wezi?
 
Kuna siku tutatandikana viboko humu mitaani humu, we ngoja tu. Yametokea Cairo na Tripoli. Gari ina miaka mitano unasema ime depreciate kutoka milioni mia mpaka milioni mbili? Yana mwisho, walahi.
 
kuna siku watakuja kulipa ipo siku tuu,wasidhani ccm itakaa madarakani milele
lini kama siyo sasa kwa sababu we will die anyway kama si kwa maboom kama gongolamboto basi kwa treni, na kama si hivyo kwa meli hawa watu bora kupambana nao sasa kwa mapanga tuu! Utaona mnaniita mchochezi eeeti!
 
Mali ya umma tafsiri yake kwa Mwana-CCM yeyote wa tangu jana, leo na kwa yeyote yule atakayezaliwa kwa jina hilo; ni mali ya bwerere bila mwenyewe.

Kuna siku watakuja kulipa ipo siku tuu,wasidhani CCM itakaa madarakani milele
 
15 Vehicles Found. Change your search options...
<Prev 12Next>
2009 Toyota Land Cruiser PRADO
$88,995.00
12,758 kms
White
Automatic

View vehicle #449301
2006 Toyota Land Cruiser PRADO
$52,000.00
90,024 kms
Grey
3000cc
Automatic
View vehicle #408828
2007 Toyota Land Cruiser
$50,000.00
87,043 kms
Grey
4500cc
Manual
View vehicle #468607
2007 Toyota Land Cruiser PRADO
$49,995.00
68,723 kms
Blue
Automatic

View vehicle #471166
2007 Toyota Land Cruiser PRADO VX
$48,990.00
73,768 kms
Silver
3956cc
Automatic
View vehicle #497662
2004 Toyota Land Cruiser PRADO VX
$36,995.00
86,000 kms
Black
4000cc
Automatic
View vehicle #499033
2001 Toyota Land Cruiser
$28,000.00
103,050 kms
Green
3000cc
Automatic
View vehicle #229770
2002 Toyota Land Cruiser
$23,000.00
183,427 kms
Blue
3000cc
Automatic
View vehicle #403419
1995 Toyota Land Cruiser
$20,995.00
288,000 kms
Green
4200cc
Automatic
View vehicle #498763
1999 Toyota Land Cruiser PRADO
$20,990.00
White
3000cc
Automatic

View vehicle #497683
<Prev 12Next>
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom