Ya Arumeru ni ushidi wa Taifa

nginda

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
744
82
ninaposema Taifa ninamaanisha wananchi wema na wenye mapenzi mema. Ni muda mrefu watanzania tumekuwa kama yatima kutokana na utawala mbovu na wakifisadi kiasi kwamba wengi wamekata tamaa. Bahati mbaya sana wizi umekuwa ukifanywa waziwazi bila woga na hakuna wa kufunga paka kengele. Mungu Asante kwani umesikia kilio cha watanzania.

CCM kwa sasa imekuwa chama cha ukoo. Utasikia, Karume, Mkapa Kikwete, makamba, nauye, Sita, lowasa na sasa walitaka Sumari na ndizo koo zinazoshikilia chama. Sasa watanzania tumeanza lini utawala wa kifalme?

Lakini pia tunahitaji kumshukuru Mungu kwa kuwaamsha watanzania ili kujua haki zao. Najua Arumeru walilishwa sana pilau, kanga, eti ukiweka bendera ya magamba kwenye gari unapewa 10,000/-. Huu ni ujambazi uliozidi wa silaha. Hongereni wana Arumeru kwa kuamua. Ni wakati wa maendeleo na siyo danganya toto ya magamba. lakini siyo tu Arumeru, pia wako wananchi walofanya historia nyingine kwa kuwaondoa madiwani wa magamba na kuweka wa CDM. Hongerenis saana

Ombi langu kwa chadema. mmeanza vizuri. Sasa ujitathmini na mhakikishe kuwa mliyowaahidi wananchi wanayapata. Sina mashaka kuwa maendeleo yanaletwa na wananchi, hivyo kaZI YENU KUBWA NI KUWAUNGANISHA NA SIYO KUSUBIRI KASMA KUTOKA SERIKALI YA MAGAMBA. Uliweza kuwaunganisha wananchi wakatoa fedha kwa ajili ya kampeni za Arumeru, sas tumieni mwanya huohuo kuwaletea maendelea.

Wito kwa wananchi wengine IGENI MFANO.
 
Ni kweli ushindi wa Arumeru Mashariki ni ushindi wa Watanzania wote wenye mapenzi mema, wapenda demokrasia, wapenda maendeleo na wenye hofu ya Mwenyezi Mungu. Asante Mungu wa Bwana Yesu Kristu wa Nazareth kwa kuwabariki watu wako na wao wakaweka hitikadi za vyama nyuma na kutanguliza uzalendo na hofu kwako. Wakati wengine walikuwa na msajili wa vyama, polisi, jeshi, usalama wa taifa, serikali na wastaafu CDM walikuwa na Mungu wa kweli. Wakati wengine walitanguliza matusi na udhalilishaji CDM walitanguliza ukweli na unyenyekevu. Mbegu hii iliyopandwa Arumeru Mashariki tunakuomba Mungu imee na isambae katika kingo zote za Tanzania ili wote wajue na watambue kuwa sadaka ikupendazayo sio ya kuteketezwa bali ni moyo uliovunjika na kupondekapondeka Zab:51
 
Haki ina tabia ya kutafuta muda wake, na kujitokeza hadharani...!
Haizuiwi na nguvu za DOLA wala vipande vya fedha!
 
Haki ina tabia ya kutafuta muda wake, na kujitokeza hadharani...!
Haizuiwi na nguvu za DOLA wala vipande vya fedha!

so PAKA unasema haki ni kama maji....ambayo hutafuta levo yake yenyewe....na kweli maji ni haki ya viumbe vyote kuishi.....
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom