X wake kivingiine!!!

[QUOTE=Lizzy;1787025]Umeongea nae ukajua kwanini alikudanganya kwamba hata kuwasiliana nae hataki huku anafanya kinyume cha alichosema??Usirukie kutaka ushauri kabla hujajua tatizo!Inawezekana huyo mwanaume anamsumbua..yani anamtaka kwahiyo amefanya hivyo ili ndoa isiharibike.Au hata anamtukana ila hataki kukuhusisha!Hizi zote ni assumption..nakushauri utafute jinsi ya kumuuliza mkeo taratibu ili akwambie kulikoni.[/QUOTE]

Walionana wapi mpaka kukubali kupeana namba na kuificha kwa jinsia nyingine? Amuulize kama it' ok kwake kuendelea kuwasilaiana na X-G wake pia. Asijekuwa yeye ni mkali hataki kusikia mambo ya X-G wa mmewe kumbe yeye anayo namba ya X-B wake. Situation kama hiyo inapunguza trust iliyopo katika ndoa ni kama kuna mambo mengi yasiyo mazuri yanafanyika mwenzi wako hakwambii. Kwa ujumla inaleta mashaka kwenye Mahusiano. Nilishakataa mambo ya X-G kwenye misamiati yangu maana ni baraha tupu. Yanini nimtie presure wife kwa mambo yasiyokuwa na tija kwenye ndoa. Unapungukiwa na nini ukikata mawasiliano na X wako?
 
Mkuu Pole sana, Hapa kuna kitu kinaendelea baina yao, Huenda X anatumika kuziba mapungufu yako na mke wako, Kuna wengine X ANAKUWA MSHAURI MKUU,anapogombana na mume/mke anatafuta Faraja kwa X. Na kama alikuwa na Perception kwamba X anacare sana basi , Hata ushauri kwenye mambo ya nyumbani kwenu hutatoka kwa X. Na kama kwenye mambo ya unyumba hujaweza kuziba nafasi ya X, LAZIMA ATATAFUTWA TU ili aweze kufanya kazi yake sawasawa.
 
Hata kama ni hivyo au la lkn kuna watu wazima wenye heshima zao, msifanye JF ya wahuni ktk maongezi ila jaribuni kutoa ushauri ambao utaleta tija kwa swali alilouliza ndg yetu.
Naungana na Lizzy kuwa ni vema uongee nae kwanza kabla hujachukua uamuzi wa haraka kwa kusikiliza ndg Chwechwe, kuwa mke si mwaminifu.
Km unamashaka nae basi kwanza uwe mume mwema kuliko siku zoteza nyuma, pili, chukua hatua ya kumtoa out mkeo mara kwa mara huku ukimtega, kupitia kwa majamaa au dada zako wenye siri au hata majirani , japo usiwaambie jirani kinachoendelea, ila kuwa nao karibu pia ili km kuna jambo baya utayasikia tu.
najua wazi unampendamkeo kuliko tunavyo wezaa sema cc tuliombali na wewe, mpe muda mkeo mwambie ww c hawala kwangu ila ni mke tunajenga mwaisha c vinginevyo kwahiyo nakupenda nimesamehe yote ila jaribu kuondoa cm namba na pia jaribu kukriate safari za hapa na pale ujuwe nini anakiwazia, kama kipo atamtafuta kisha utajua ''mapenzi ni kikohazi utajua kunamgonjwa wa kifua cha mapenzi kati yenu.
Reargads: wana JF wote.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Habari wana JF!!

Nilitokea kumfahamu X boy friend wa mke wangu baada ya kupita miaka mitatu ya ndoa yetu kwani alirudi kwake akiwa na nia warudiane but akakuta ameolewa na mimi so ikashindikana kwake!!

Wife yeye akawa hataki hata kumuona au kuwa na mawasiliano naye kutokana na alivyodai kuwa historia mbaya ya mapenzi yao.

Hivi majuzi nimekuta mke wangu kamsevu huyo X wake kwa jina la kike kwenye phone book yake na amekiri kweli kamsevu (X) hivyo, ila ni baada ya mimi kushuku kuwa kuna mawasiliano yasiyo ya kwaida, na kabla ya hapo alijifanya hana mawasiliano naye kabisaaa, kwa namna yoyote ileee!! Isitoshe ni namba ambayo baadae nilianza kuifatilia nikakuta ipo busy sana kwenye simu yake.

Swali lisilo na jibu ni; Kwanini amsave kivingine? Kwanini ajifanye hana mawasiliano naye kabisaaaa kwa namna yoyote ile kumbe wanawasiliana?

...kuwa mpole, mpe support mkeo. mfariji na umweke karibu.
Mwelezee madhara ya mawasiliano yake na ex-wake.

...Mwambie ukweli ni jinsi gani imekuuma kiasi ya wewe kufuatilia ukweli,
na hayo uliyoyagundua.

...Mwambie ukweli Umeumia sana, na alivyopunguza uaminifu wake kwako.
Mwambie Ukweli kwa mwenendo huo mnaiweka ndoa yenu mashakani...

...Utaweza kuyatekeleza na kumwambia mkeo haya?
Jaribu leo, jaribu ukiwa tayari. Wengi tulipitia haya,
weye sio wa kwanza.

Kila la heri.
 
duh, kweli ndoa si mchezo!
mi nafikiri ujitahidi uli-solve hili suala mapema kabisa. mkae chini muone njia iliyobora. kama hutaki kumsikia ni vyema ukamuwekea wazi mkeo. Ila kama mnataka awe 'family friend' pia mkubaliane..
make sure mizizi haijajengeka

sijui kwanini watu wako kwenye ndoa bado wana-entertain mawasiliano na ma-ex wao, why did u choose to get married in the first place then??

Hizi entertainment hizi..,zinaniboa mpaka basi...!! kwanini uolewe wakati bado unahisia kwingine..,fasheni eeehh,tunakoelekea huko sio kuzuri hata kidogo..
 
pole sana mkuu nakushauri badilisha namba za mkee kisha fatilia kwa makini

...huo ni wajibu wa mke, kusitisha/kuendeleza mawasiliano. kama mke ameamua usaliti, hata akinyang'anywa simu haitosaidia kutowasiliana.

mjomba! :A S check_03::censored::A S check_03: mkeo kirahisi.

...Lugha haipendezi kabisa kaka. Haipendezi hata kidogo.
Badilika bana.
 
Habari wana JF!!

Nilitokea kumfahamu X boy friend wa mke wangu baada ya kupita miaka mitatu ya ndoa yetu kwani alirudi kwake akiwa na nia warudiane but akakuta ameolewa na mimi so ikashindikana kwake!!

Wife yeye akawa hataki hata kumuona au kuwa na mawasiliano naye kutokana na alivyodai kuwa historia mbaya ya mapenzi yao.

Hivi majuzi nimekuta mke wangu kamsevu huyo X wake kwa jina la kike kwenye phone book yake na amekiri kweli kamsevu (X) hivyo, ila ni baada ya mimi kushuku kuwa kuna mawasiliano yasiyo ya kwaida, na kabla ya hapo alijifanya hana mawasiliano naye kabisaaa, kwa namna yoyote ileee!! Isitoshe ni namba ambayo baadae nilianza kuifatilia nikakuta ipo busy sana kwenye simu yake.

Swali lisilo na jibu ni; Kwanini amsave kivingine? Kwanini ajifanye hana mawasiliano naye kabisaaaa kwa namna yoyote ile kumbe wanawasiliana?

We kilichokufanya ukague simu ya mkeo kitu gani?
 
Back
Top Bottom