X wake kivingiine!!!

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,503
6,374
Habari wana JF!!

Nilitokea kumfahamu X boy friend wa mke wangu baada ya kupita miaka mitatu ya ndoa yetu kwani alirudi kwake akiwa na nia warudiane but akakuta ameolewa na mimi so ikashindikana kwake!!

Wife yeye akawa hataki hata kumuona au kuwa na mawasiliano naye kutokana na alivyodai kuwa historia mbaya ya mapenzi yao.

Hivi majuzi nimekuta mke wangu kamsevu huyo X wake kwa jina la kike kwenye phone book yake na amekiri kweli kamsevu (X) hivyo, ila ni baada ya mimi kushuku kuwa kuna mawasiliano yasiyo ya kwaida, na kabla ya hapo alijifanya hana mawasiliano naye kabisaaa, kwa namna yoyote ileee!! Isitoshe ni namba ambayo baadae nilianza kuifatilia nikakuta ipo busy sana kwenye simu yake.

Swali lisilo na jibu ni; Kwanini amsave kivingine? Kwanini ajifanye hana mawasiliano naye kabisaaaa kwa namna yoyote ile kumbe wanawasiliana?
 
Ukweli ni kwamba baadhi ya wapenzi wengi wa miaka ya nyuma wana mawasiliano ya karibu sana na hii imesababishwa na urahisi wa mawasiliano katika dunia ya utandawazi kupitia simu za mkononi na internet. Bahati nzuri wewe ulibahatika kumfahamu X Boyfriend wa mkeo lakini wapo wengi hawawajui na hata wakizipekua simu za wake/waume wao na kukuta majina/namba ambayo/ambazo hawayafahamu/hawazifahamu hawatatia shaka yoyote ile.

Hayo maswali mawili anayeweza kuyajibu vizuri ni mkeo.
 
Even though this whole situation seems very suspicios,I think there are two befitting scenarios
1. There maybe something fishy going on.
2. There is absolutely nothing going on. Having dated before, it is possible that they are friends. However, not knowing your reaction to her befriending her ex, akaona kuepuka unneccessary ugomvi its better she keeps their communication a secret
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ex man coming back! na anaseviwa kwa jina la kike! Fanyia kazi hiyo issue mkuu!
 
Pole Mkuu, hapo unaibiwa kwa ULAINI! Ingekuwa hakuna uhusiano, hiyo namba ya simu isingekuwepo au ingeandikwa kwa jina halisi,
 
Umeongea nae ukajua kwanini alikudanganya kwamba hata kuwasiliana nae hataki huku anafanya kinyume cha alichosema??Usirukie kutaka ushauri kabla hujajua tatizo!Inawezekana huyo mwanaume anamsumbua..yani anamtaka kwahiyo amefanya hivyo ili ndoa isiharibike.Au hata anamtukana ila hataki kukuhusisha!Hizi zote ni assumption..nakushauri utafute jinsi ya kumuuliza mkeo taratibu ili akwambie kulikoni.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Umeongea nae ukajua kwanini alikudanganya kwamba hata kuwasiliana nae hataki huku anafanya kinyume cha alichosema??Usirukie kutaka ushauri kabla hujajua tatizo!Inawezekana huyo mwanaume anamsumbua..yani anamtaka kwahiyo amefanya hivyo ili ndoa isiharibike.Au hata anamtukana ila hataki kukuhusisha!Hizi zote ni assumption..nakushauri utafute jinsi ya kumuuliza mkeo taratibu ili akwambie kulikoni.
inaonekana paragrafu ya tatu ya mleta sredi hujaielewa vizuri. hebu isome tena halaf ukuje tena tulisakate hili rumba hehehe
 
duh, kweli ndoa si mchezo!
mi nafikiri ujitahidi uli-solve hili suala mapema kabisa. mkae chini muone njia iliyobora. kama hutaki kumsikia ni vyema ukamuwekea wazi mkeo. Ila kama mnataka awe 'family friend' pia mkubaliane..
make sure mizizi haijajengeka

sijui kwanini watu wako kwenye ndoa bado wana-entertain mawasiliano na ma-ex wao, why did u choose to get married in the first place then??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
hapo kuna kitu kinaendelea.haiingii akilini kama huna interest na mtu,na huyo mtu awe anakutaka,halafu a save no.yake,halafu tena,katika uchunguzi wako,kutwa simu ziwe busy,jee ina maana juu ya kukataliwa wameamua wawe wanaongea weeeeeee,mmmh.muhimu,chunguza taratiiiiiiiiibu,jifanye kama hujali kinachoendelea,mwisho wa yote jibu utalipata tu.maana either maongezi ya kawaida tu hakuna kinachoendelea{ingawa wasiwasi wangu kwa nini aseme hataki hata kumuona ?}kama mtu hutaki kumuona,utakubali uwe unawasiliana nae? au kuna kitu kinaendelea.
 
anaza ndoa viktim. hehehe mkuu mbona hapo ukweli upo wazi labda uamue kuufumbia macho tu.


Inabidi mkuu afanye aumuzi mapema... hili halina mjadala mtu mkweli angekwambia kila kitu, kwani ni wanawake wangapi wako kwenye ndoa na wanat**gozwa, kitendo cha kukana kuwa na mawasiliano na jamaa then unagundua ana mawasiliano... ingekuwa ni mimi sihitaji hata ushauri sababu kesi ishaisha kinachobaki ni uamuzi tu......:smash:
 
Mkuu pole kuna msemo wa kiswahili unaosema kiporo hakiitaji moto mwingi kuliwa, natilia shaka huo uhusiano wa huyo mkeo na X - boyfriend wake maana ni kama mtalaka wake na mtalaka huwa hatongozwi! Pole mkuu kama nimekuudhi lakini huo ndiyo muono wangu.
 
we mwenyewe mbona jibu unalo!!??kama umeamua kuiacha kama ilivyo basi mwambie watumie condom..
 
Wewe pia rudia kiporo chakohiyo ndio staili ya siku hizi mwanangu. Usiumize kichwa mimi ma fiance alimfuta X wake na kuniambia mabaya mengi tu recently nimegundua yumo ndani ya phonebook kwa jina badala ya Bonaventure anaitwa Baina. Nikathink twaisi mh nikampm wa enzi akarespond nikamsevu kama ex love. Hapo tatu tatu. NDIVYO upepo wa mahusiano ulivyo.
 
inaonekana paragrafu ya tatu ya mleta sredi hujaielewa vizuri. hebu isome tena halaf ukuje tena tulisakate hili rumba hehehe

Nimeelewa sana na ndo maana nikasema inawezekana mshkaji anamsumbua hivyo amemsave hivyo kwasababu hataki kumpa mumewe presha!
 
Wewe pia rudia kiporo chakohiyo ndio staili ya siku hizi mwanangu. Usiumize kichwa mimi ma fiance alimfuta X wake na kuniambia mabaya mengi tu recently nimegundua yumo ndani ya phonebook kwa jina badala ya Bonaventure anaitwa Baina. Nikathink twaisi mh nikampm wa enzi akarespond nikamsevu kama ex love. Hapo tatu tatu. NDIVYO upepo wa mahusiano ulivyo.

mmmh,kazi ipo.kama uchumba tu hali hiyo,jee mkiwa katika ndoa itakuwaje?naona tit for tat mapema hivyo,si mnadanganyana wenyewe? samahani lakini
 
Back
Top Bottom