X-road (njia panda)

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Jamaa mmoja anaishi mji kasoro bahari[morogoro].Huyu bwana ni driver wa magari ya kusafirisha mafuta ya kampuni moja maarufu hapa nchini.Huyu jamaa anaishi pamoja na mama yake ambaye ni mjane baada ya kufiwa na mumewe.Lakini kuna jambo limezuka,huyu mama ameunda uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa karibu wa mshikaji.Kibaya zaidi,jamaa anadiriki kutangaza kitaa vile anavyomtenda mama wa rafiki yake.Hizi habari zilimfikia jamaa,akaamua kumuuliza bi mkubwa kuhusu hili suala,cha ajabu mama alikuwa mkali.Alimng'akia mshikaji na kumwambia hana jipya la kumfundisha katika maisha haya,yeye ni mtoto na atabaki kuwa mtoto wake,'kama hutaki kunitunza,basi nirudishe kijijini',alisema mama huyo.Kiufupi jamaa kabaki x-road!
 
Sasa huyo kijana anaakili gani mpaka kumuuliza mama yake maswali ya ajabu?!Cha kufanya angempa mkong‘oto huyo rafikiye awe na heshima kidogo basi....
 
si heshima kumuuliza mama jambo kama hilo hata kidogo...kama anaona yamemshinda ahame mtaa au mji.
 
Sasa huyo kijana anaakili gani mpaka kumuuliza mama yake maswali ya ajabu?!Cha kufanya angempa mkong‘oto huyo rafikiye awe na heshima kidogo basi....
dah umenena! Angempa kipondo mwenyewe angeingia mitini bila maza kajua
 
Jamaa mmoja anaishi mji kasoro bahari[morogoro].Huyu bwana ni driver wa magari ya kusafirisha mafuta ya kampuni moja maarufu hapa nchini.Huyu jamaa anaishi pamoja na mama yake ambaye ni mjane baada ya kufiwa na mumewe.Lakini kuna jambo limezuka,huyu mama ameunda uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa karibu wa mshikaji.Kibaya zaidi,jamaa anadiriki kutangaza kitaa vile anavyomtenda mama wa rafiki yake.Hizi habari zilimfikia jamaa,akaamua kumuuliza bi mkubwa kuhusu hili suala,cha ajabu mama alikuwa mkali.Alimng'akia mshikaji na kumwambia hana jipya la kumfundisha katika maisha haya,yeye ni mtoto na atabaki kuwa mtoto wake,'kama hutaki kunitunza,basi nirudishe kijijini',alisema mama huyo.Kiufupi jamaa kabaki x-road!
:- Mpenzi wa mama yako ni baba yako. kwishne.
 
tatizo liko wapi hapo? Mama nae anahitaji mtu...tena ni bora amuache mama afurahie...ila amuonye rafikiye asiwe mgeni wa mapenzi.
 
Huyo jamaa dio kakosa ustarabu mbona wanawake wamejaa tu why kumdhalilisha huyo so called rafiki yake?
 
huu urafiki unatakiwa ufe haraka sana....jamaa alitakiwa kimya kimya amwadabishe mshikaji kwa kutothamini urafiki wao na utovu wa nidhan usioelezeka...yaani wewe ni rafiki yangu bado unadhiriki kumtongoza mama yangu mzazi....hii inaonyesha ni jinsi gani ulivyonidharau mm na mama yangu mzazi....wanaume wengine bana.
 
Duh ndio utandawazi wenyewe huu, wamama wengine ni noma, baasi hana la kufanya, auheshimu tu huo uhusiano ili maisha yaendelee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom