Wz'bar wasifu umoja na mshikamano ktk Serekali ya SUK kuwa imara kwa kuwaunganyisha tena.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130



Written by Mrfroasty (Ufundi) // 29/03/2011 // Kitaifa // 2 Comments

11-564x272.jpg
Na Salma Said,
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amewataka wajumbe wa baraza hilo kuunga mkono juhudi ya asasi za kiraia katika kupigania haki na maendeleo ya wananchi.
Alisema asasi hizo zinatoa mchango mkubwa unaosaidia kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuwapa wananchi uwezo wa kutatu matatizo ya maendeleo katika maeneo yao .
Kificho alikuwa anafungua mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Asasi za Kiraia Zanzibar (ANGOZA) jana na kuwashirikisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika ukumbi wa baraza hilo huko Mbweni nje kidogo kutoka mjini hapa.
Alisema utendaji wa asasi za kiraia ukiungwa mkono na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na jamii kwa jumla utasaidia kuharakisha unaqweza kuharakisha upatikani wa maendeleo ya wananchi.
Wakati wa mdahalo huo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wadau wa asasi mbali mbali zinazoshirikishwa na ANGOZA walijadili “umuhimu wa wa ushiriki wa wananchi na asasi za kiraia katika usimamizi wa utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya serikali za mitaa, Zanzibar.
Mpango huo wa miaka mitano una lengo la kutoa elimu juu ya ushiriki wao katika kubuni mipango ya maendeleo inayotekelezwa na serikali za mitaa na kusimamiwa na mabaraza ya madiwani.
“Wananchi wengi hawajui sheria na sera zilizounda serikali za mitaa. Vile vile hawajui mchakato wa utekelezaji wa mchakato wa utekelezaji wa mpango wa kuleta mageuzi katika serikali za mitaa, Zanzibar ,” alisema Katibu wa ANGOZA, Asha Aboud wakati wa mdahalo huo.
Sambamba na mdahalo huo, ANGOZA pia imeandaa maonyesho ya siku mbili juu ya kazi mbali mbali zinazofanywa na asasi za kiraia Zanzibar .
Maonyesha hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Mbweni na kuwashirikisha wajumbe wa baraza hilo na wadau wengine za kiraia.
Taasisi za kiraia 57, zinashiriki katika maonyesho hayo na 52 zinatoka Zanzibar na tano zinatoka Tanzania bara. Nia ya maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa mpango wa mageuzi ya serikali za mitaa Zanzibar ambao unafadhiliwa na taasisi ya Sweden iitwayo The Foundation for Civil Society.
 
Back
Top Bottom