Wote wangu sasa niende wapi .............

DOGOSA

Member
May 22, 2012
8
1
Kuna bi mdashi mmoja kitaa cha jirani alitoa kali ya mwak, lakini yote ilikuwa katika kudhihirisha upendo wake kwa ndugu jamaa na marafiki zake.

One day alipokea taarifa ya msiba kutoka kwa swaiba wake ambaye alifiwa na mwanaye na wakati huohuo kuna jirani yake alikuwa anamwozeza bintiye. Hawa watu wawili wenye matukio tofauti nyumba zao zilikuwa zimetenganishwa na fence ta maua na kwa bahati mbaya kulikuwa na tundu katika hiyo fence ambalo lilikuwa kubwa kiasi.

Ili kuwaridhisha wote na kuwaonyesha ukaribu wake kwaoilikuwa ni kupitisha kichwa katika lile tundu la fence, kilichotokea unajua ninini? Kile kichwa kilikuwa kimetokeza upande wenye msiba hivyo alikuwa akilia na kutiririsha machozi ya haja pamoja na waombolezaji wengine. Wakati huohuo kiuno kilikuwa upande wenye harusi na alikuwa akizungusha nyonga si mchezo siunajua tena mambo ya twaarab na mduara.

Kwa kufanya hivyo alihisi amewaridhisha wote wawili ila kama alikuwa sahihi ama la jibu litategemea na msimamo wa kila mtu anavyohisi!!!!!!!!!!!
 
Mambo ma2 hayaend kwa wkt m1.atacheza kikwel.lkn kulia atalia machozi ya mamba!
 
Back
Top Bottom