WOSIA WA MWISHO WA MHANGA WA NSSF Kabla

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
1.Mmetuvunjia makazi yetu kwa kukosa uwajibikaji wenu na kututia hasara na umaskini mkuu

2.Mara mkaanza kuuza mashamba na viwanda vyetu kwa walowezi.

3.Mkaendelea kuiba madini yetu na wanyama na kuwatorosha ulaya .

4.Mkaanza kutuletea vyakula na madawa yasiyo kizi viwango tukanyamaza.

5.Mkaanza kutlipua kwa Mabomu tukawa tunawaangalia tu

6.Mkahakikisha watoto wetu Hawapati elimu bora

7.Mkahakikisha kuwa maji yanakuwa ajenda ya kupata kura hivyo kutuhadaa kwa maji vijiji kumi ili hali fedha mmesha kula mnaishia kutekeleza miradi vijiji 2 au vitatu tu.

8.Mkaanza kutupandishia kodi kwenye ili hali wenye madini wanalipa mrahaba wa asilimia tatu tu

9.Mkatupandishia Kodi mafuta ya taa baada ya kuogopana nyie kwa nyie kushikizana adabu tukawaangalia.

10.Mkaendelea na kuzitumbua kodi zetu kwenye safari za anasa ughaibuni

11.Mkatudanganya kilimo bora nikuweka mbolea tu shambani ili hali hamjui kiasi cha rutuba ya udongo ili muweze kula vizuri ruzuku mlizoiba kwa kutumia migongo ya viwanda vya mbolea.

12.Mkaendelea kuweka 50% katika manunuzi na ujenzi wa mambo mbalimbali kwa ajili ya manufaa yenu tukanyamaza.

13.Mkadiriki kututelekeza wakati madaktari wakiendelea kugoma sisi tukanyamaza na kuendelea kufa ili hali nyie mnatibiwa nnje ya nchi.

14.Mkaleta makampuni yanayoiba fedha kwa kubadili majina ya mahotel kila kuchwao ili hali nikifungua genge mbagala TRA wameshafika.

15. Mkajipa masharti nafuu yakujikopesha nyumba tulizojenga kwa jasho la kodi zetu na babu zetu.


16.maketupiga risasi pale tulipo amua kujishughulisha kujiinua kiuchumi, Mkatutesa na kutupiga pale tulipo wapinga.

17.Mkaendelea kujiongezea maposho na mamishahara makubwa sisi tukanyamaza.

18.Makendelea kutudanganya na kutufariji tuamini hayo ndio maisha tunayotakiwa kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ya Amani.

19.Mkakwapua mabillion hata kudiriki kuyaita vijisenti ili hali wananchi wanakufa kwa kukosa dawa za matumbo.

20.Mkatuhubiria udini na ukabila pale tulipotaka kuwa wamoja kuwapinga

21. Mkatumia mahakama kama chombo cha kulinda udhalimu

22. Makatumia sheria kama mbinu ya kukandamiza

23. mkatumia Bunge kama kichochoro cha madalali/Makuhadi/propaganda

24. Mkatumia vyombo vya usalama kulinda na kubariki uporaji.

25.Leo hii hata kile kidogo cha NSSF tulicho kiwekeza kwa muda mrefu mnatupora jamani imenifaa nini kuishi kama sina uhakika wa maisha baada ya hapa yamenifika shingoni.

Kweli kweli mtatufanya hivi hata lini, hivi kama Amani inashindwa mnafikiri tutakufa wote hakika hamna risasi million 39 hamna na nina imani hamna. Mungu atusamehe kwa yatakayoendelea kutokea sasa.

Kwa yule atakaye salimika na akawe shahidi wa mambo yote. Amani tuliipenda lakini walinzi wa Amani walitusaliti kwa kubaka wake zetu, Kuwanyima chakula wazee na watoto wetu, kuhujumu mali na amana zetu, kutishia na kuharibu utu wetu kwa kisingizio cha Amani. Na sasa tumeamua kudai haki kwa vitendo


Muda wa propaganda umekwisha, kwani maneno matupu................

Action speaks louder than words:
 
Sasa wataleta kodi ya hewa mnayovuta maana ndio pekee ambayo imebaki bila kulipiwa kodi
Maana kila kitu washachukua na hamna hata ardhi tena, wanyamapori sio wenu, mifugo sio yenu na ukitaka mafao yako timiza miaka hamsini na tano na kama hutafiki shauri yako na Mungu wako kwani nani alikuambia ufe mapema
 
Muda wa propaganda umekwisha, kwani maneno matupu................

Action speaks louder than words:
talk the talk but walk the walk mkuu!!

Hawa jamaa wanashangaa ni kwa kiasi gani watz tumelala na wamefanya kila wawezalo ili tuamke lakini wapi, sasa wanakuja na hiyo attempt kuona kama itatuamsha kakini ninavyoijua hii nchi, bado tutaendelea na usingizi tu na wachache wetu huenda tukaishia kwenye key boards!

Ndio maana Madaktari wamejaribu weeeeeeee kutuonyesha njia lakini wapi na wengine wanaona ni bora waende zao nje!

 
Mwanaharakatihuru Umesahau.....wakajipa Bilion 8 kwa mwaka wastaafu watano na wake zao...ilihali Hospitali KUBWA za rufaa zote zikapewa bilioni 6 kwa mwaka.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom