World Economic Forum yaja - wadaresalama mtapita wapi?

6am-9am and 3pm-7pm Ali Hassan Mwinyi Road will be closed, Ohio closed off/on ,Nyerere road closed off/on.
· Mwenge area near mlimani city,Buguruni ,Uhuru and the city centre will be impassable during certain hours.
 
Naona tuwaunge mkono TUCTA - Tuanze mgomo mapema kesho, wewe fikiria barabara zipo 3 tu, sasa ufunge moja ubaki na 2 hiyo foleni sijui itakuwaje?
 
Jamani mimi namsifu Lukuvi unajua nini? angekuwa mtu mwingine wala asingetangaza mngekupandana na mikono ya trafic. Lakini !! Lukuvi vipi bana nakujua wewe ni mtumiaji wa forum kaka badilisha schedule tusipunguze uzalishaji wa nchi yetu. Tena nilikusifu mkuu wakati wa hotuba yako ya Mei Mosi maana uliwaponda wale waliojitenga na TUCTA hawakuelewa tu kaka. maana mambo ya TUCTA yakitengemaa kaka na wewe unafaidika.
 
wanaomlaumu Rukuvi,sidhani kama ana makosa. yeye ni mtekelezaji tu. wanaofanya maamuzi kama hayo ndo wawe responsible.
but all in all this is not fair kabisa.
this is our country not otherwise.
 
wageni gani hao mpaka tufungiwe barabara??

Festi ledi, hawa wageni wetu wanakuja kujadili mambo ya uchumi wa bara la africa - kawaidia huwa mgeni njoo mwenyeji apone lakini naona kwa sasa itakuwa tofauti - tutaumia sana na mifoleni ya jijini.
 
muda ndo huo hapo 12-3 asubuhi, na jioni saa 9-1 usiku kuazia tarehe 4-7 May 2010
mbona mtakoma uko dar?poleni sana maana muda wenyewe ulowekwa ni muda wa kwenda makazini/biashara na muda wa kurudi home sasa sijui siku iyo watu waende makazini kuazia saa 4 asubuhi na kutoka iwe saa 7-8??,,,,
sijui wamefikilia nini kuufanya huu mkutano Dar???na limvua linyeshe adi washangae fulu dayz

fulu wehuz
 
Naona tuwaunge mkono TUCTA - Tuanze mgomo mapema kesho, wewe fikiria barabara zipo 3 tu, sasa ufunge moja ubaki na 2 hiyo foleni sijui itakuwaje?

uwoga ndugu,uwoga ndo unaotuponza!!yaani hii kitu ingefaa kama thailand vile hakuna kazi hadi kieleweke
 
Ni miongoni mwa maamuzi ya kipuuzi kabisa yaliyowahi kufanywa na hawa majambazi wa CCM. Huo muda walioutaja ni wa foleni kubwa sana barabarani, sijui kama wamefikiria madhara yake iwapo hizo barabara zitafungwa wakati huo!
 
Si wangepeleka Arusha Mungu wangu? yaani nashindwa kuelewa kutakuwaje!
 
Dar zaidi uijuavyo!

Na hapo ikinyesha kama last week tumekwisha!
 
Hawa viongozi wetu hawataki kukuna vichwa vyao, kabla ya mkutano huu si wangechonga barabara za pembezoni ili zitumike na wananchi? kwani huo mkutano wao ndiyo utawafanya watu wasiende kazini? Mfano kwa wale wanaotumia nyerere road kwanini wasingechonga barabara za pembezoni mwa reli ambapo kuna nafasi kubwa tu na ingesaidia kupunguza msongamano usiokuwa wa lazima kwa wananchi. Jamani viongozi wetu amkeni wakati unawapita sasa!!
 
Hivi hakuna njia nyingine mbadala huko Tanzania mpaka kufunga barabara na kuzuia wazawa wasifaidi matunda ya uhuru wao?
 
Sijui kwa nini watu tunaogopa kufa wakati hapa TZ kuna shida hivi. Mfano mimi nakaa BUNJU A nitafika Kariakoo kweli ofisini mwangu?
 
Tatizo sio la mkutano kufanyikia Dar,bali tatizo ni venue ya mkutano huo yaani Mlimani City... Na wageni woote wanafikia City centre.... Yakh!!!
 
Nimeisikia hii habari katika radio leo asubuhi kuwa barabara ya Nyerere na Ali Hassani Mwinyi zitafungwa ili kuwapisha wageni wanaokuja kwenye mkutano wa maedeleo Africa.

Je,hii imekaaje waungwana?


Yale yale ya SUILVANIIIIIIII, hakuna lolote hapo, usumbufu A faida F.
 
Jana baada ya kuangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku nikamwona Mh LUKUVI akitangaza utaratibu wa barabara zitavyokuwa zikitumika kuanzia tar 4-7 May.

Mimi nimejiuliza maswali mengi sana, bila kufunga barabara mji huu umejaa Traffic Jam sasa zitakapofungwa saa 1-4 asbh na saa 9-1 jioni hali itakuwaje?

Na hawa walioamua kuuweka hapa DSM kwa nini wasiupeleke huko Arusha kulikofanyika SULIVAN ambako Trafic Jam sio kubwa?

Jamani hata hili limewashinda kuliona TUNAENDA WAPI!!!
 
6am-9am and 3pm-7pm Ali Hassan Mwinyi Road will be closed, Ohio closed off/on ,Nyerere road closed off/on.
· Mwenge area near mlimani city,Buguruni ,Uhuru and the city centre will be impassable during certain hours.

muda ndo huo hapo 12-3 asubuhi, na jioni saa 9-1 usiku kuazia tarehe 4-7 May 2010 mbona mtakoma uko dar?

Hii imekaa wazi kabisa. Mbona mnashindwa kuiona?

Watu sasa hivi Dar wataanza kuongelea Ugeni na foleni za Dar na si MGOMO. Media zote zitajadili ugeni huo na kuacha kuongelea Mgomo. Naungana na wengine wanaoombea Mvua ya gharika inyeshe ili hao WAGENI wasiotutakia mema Tanzania (nina uhakika wanafahamu kwa nini wanakuja/mgomo) basi wakione cha moto. Na ikinyesha basi watu tapisheni vyoo vyenu kwa nguvu hasa Nyerere Road.

Hii hufanywa na nchi nyingi sana. Wakati wa Yeltsin huko Russia, baada ya kugundua maasi yanaweza kufanyika, basi Yeltsin aliona dawa ni kuwa karibu na jeshi. Hilo bunge acha wajitenge (duma). Baada ya Yeltsin kutumia mabavu kuvunja bunge bila kufuata katiba, bunge liliamua kumuondoa yeye na kumuweka makamu wa Rais (mwaka 1993) na matokeo yake Jeshi liliingilia kati.
Kuhusu maasi kutokea, yeltsin alifahamu mapema na akawa hana jinsi ya kujisogeza karibu na wanajeshi. Akasuka mipango yake (nafikiri alishirikiana na USA) na wakaona dawa ni kumpeleka Marehemu Michael Jackson. President Yeltsin kwa kutumia kisingizio cha kuandaa UGENI WA MICHAEL JACKSON, akawa kajisogeza karibu sana na wanajeshi. Wale wabunge na jamaa waliovamia White house na kujifungia, vilitumwa vifaru na vikarusha risasi chache na jengo likawaka moto kidogo tu. Ugomvi ukaisha na mtu aliyesaidia kuzimisha akawa Michael Jackson. Sijui hata alifahamu kuwa alitumika au laa ingawa MJ mara nyingi sana walimtumia. Kila nchi iliyokuwa na uhusiano mbaya na USA, alitumwa huko MJ na wale waliokuwa wakichoma bendera ya USA jana, basi kesho yake walikuwa wanaonekana wakifurahia concert na kubeba bendera ya USA.

Picha ya kwanza: Vifaru vinashoot Russian White house.
Tanks_before_Russian_White_house.jpg


Jengo lilivyokuwa baada ya vifaru kuondoka.
Whitehouse.burnt.93oc.jpg


Michael akiwa kazini kumsafishia njia (hapa kashasafisha tayari, Mageneral wote wako kwa Yeltsin) President Yeltsin.
michael-marches-with-the-russian-defence-ministry-orchestra(95)-m-6.jpg


Huu ugeni unaokuja kesho na kesho kutwa unaanza mgomo, hauna tofauti sana na bwana hapo juu mwenye miwani na Rungu la dola.
 
Back
Top Bottom