WORK AT HOME MUM MAKES $10,397/Month Part Time.

Inawezekana ila siyo rahisi kiivyo kwasababu inategemeana mambo mengi, kama kufanya 'good keyword research', kuwa na good copy na kupata na targeted traffic.
 
Mkuu maisha ya sikuhizi mtu unakula kwa jasho lako! kama bwana mungu alivyomwambia Adam na Eva atazaa kwa uchungu. Unaweza kufanya mambo mengi ikiwemo na hiyo unayoiona hapo juu na ukafanikiwa. lakini sidhani kama ni rahisi hivyo siku zote. inawezekana huyo mama kalamba dume this time but kesho inakuaje?? fanya kazi, kaza buti mambo yataenda. tusidanganyike na vishawishi vya kutengeneza pesa kwa njia za mkato kukamilisha ndoto za abunuasi.
 
Jamani hata mimi nina wasi wasi nao maana nami pia wamenitumia email wakanipa hiyo link nijaze form yao kisha eti mara moja nitaanzan kazi nakulipwa
Nina wasi wasi nao semeni wengine
 
mkuu hao jamii ni uzushi mtupu.... tafuta kazi umiza kichwa...
 
Nashauri msijaribu kupoteza muda na hao jamaa, ni matapeli na zaidi wata hack email address zenu. Ni wizi wa zamani hapa USA.
 
Wengi wao ni matapeli. Wataanza vizuri mwisho wa siku wanakuambia tuma kiasi fulani cha fedha ili wa process. Hapo ndio utaliwa
 
Back
Top Bottom