Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,129
- 18,743
Jambo moja linaloniudhi kila siku ni jinsi watanzania tunavyochukuliwa kuwa malofa na mataifa mengine. Habari iliyopo katika magazeti ya Guardian Ltd ni kwamba Qatar walitumia ndege ya kijeshi kuiba wanyama toka Tanzania, ndege iliyotua pale KIA na kuondoka majira ya alfajiri na mapema na wanyama 116.
Hili si jambo ndogo. Ni uhaini wa hali ya juu kwamba ndege ya jeshi la nchi nyingine inaweza kuingia kinyemela nchini na kuondoka. Nani katika jeshi alitoa kibali cha ndege hiyo si tu kuingia anga la Tanzania bali hata kutua, kwa mamlaka ya nani? Ina maana ndege kubwa ya jeshi jingine inaweza kutua nchini bila JK, raisi wa nchi kuwa na taarifa? Na kama raisi alijua aliambiwa inakuja kufanya nini? Na huko Qatar, nani aliruhusu hiyo ndege ya jeshi kuja Tanzania kuchukua wanyama? Nani katika jeshi au serikali za Tanzania na Qatar walijua? Au labda Maige amesema kweli kwamba katolewa kafara?
Inakuwaje nchi inaruhusu hali ambayo inaweza hata kuingiza askari mamluki (mercanaries) kwa kutumia ndege kubwa ya kijeshi na wala lolote lisifanyike? Viongozi wanatenda kulingana na kiapo cha ofisi walichofanya?
Kweli Tanzania tumefikia hatua kama hii ambapo nchi inakuwa kama haina wenye nayo?
Ndege ya kijeshi ya Qatar iliyotumika kuiba wanyama Tanzania pale KIA
Source: IPP Media