Wizi wa NMB

Jaman hebu tuelezane machache kuhusu huduma za hii benk yetu
kwa hapa magu Ukiweka pesa kwenye account isiyo yako ni lazma uambatanishe na shlng 1000/=,
je hii inafanyika hata wilaya zingine au huku MAGU wanaibiwa..!?

hii kitu wanayo NMB toka mwaka jana mkuu wewe ndio unastuka leo pole sana..
 
Naona huo ni utaribu ambao unatumika atleast na benki za Bondeni (RSA). Sijui ni kwa sababu gani, hata mimi first time niliquestion na kuona ni dhuruma. Lakini huo ndiyo utaratibu wenyewe, haiwezekani wakafanya kinyume cha utaratibu ni sheria zao. So get over it, if you do not like it you can go bank your money somewhere else.
 
Tatizo ni kwamba hiyo buku haipo kwenye maandishi yoyote, so hata TRA hawana record kuwa NMB wamekusanya kiasi gani kwa kutoza 1000/= kwa kila mtu anayeweka kwenye account ya mtu mwingine. Kwa mantiki hiyo wanaweza wakatozwa wateja 100 kwa siku jumla ya sh 100,000/= na zote zikachukuliwa na cashier bila ya mtu mwingine kujua
 
Hawa ni wezi kweli, hivi haya mapato 1000/- huwa yanakatwa kodi? Wakati mwingine kwenye zile benki ambazo hazina kamera hawa tellers huwa wanachukua hizo buku buku zetu kwani hakuna monitoring ya kujua kuwa anayeweka ni mwenye akaunti au la, anayejua ni teller tu hivyo hata akila hakuna atakayejua na pia hizo gharama ni za nini maana hakuna tofauti mwenye akaunti anapoweka fedha kwenye akaunti yake na mtu mwingine anapoenda kumwekea. Kama tofauti ipo naombeni mnijulishe
 
NMB ni wapumbavu, yaani hata babu yangu ambaye amezeeka akinituma nikamwekee hela yake lazima wakate buku. kwa hiyo babu yangu itabidi ajikongoje. NMB think about this.
 
Huu mpango wa NMB kukata buku binafsi nimeona sitauweza,
simply nitahamia Equity bank,naona wao wana terms rahisi kidogo
 
Mkuu kote nchini hata ARUSHA hilo tatizo lipo na hasa unapomtumia pesa mtu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.Lakini kwa taasisi za serikali mfano vyuo vya serikali na halmashauri hautozwi hela.
Waziri mkuu (mtoto wa mkulima) alishalitolea kauli hili kuwa wasiwatoze wateja wao buku,lakini wamedharau na kulikaidi agizo lake,sijui ilikuwa siasa!

Mkuu, hilo agizo lilikuwa purely political order....NMB ni commercial entity ambayo lazima itatengeneza njia zake za kuongeza mapato....hiyo, ni njia mojawapo ingawaje haileti sense! Zamani, ilikuwa ni 10,000/= kama mtu unayemwekea ni wa tawi lingine na hiyo ilikuwa ni lazima kv walikuwa wanafanya wire transfer kwahiyo ilikuwa ni lazima wafanye cost sharing! Lakini kwa sasa, hamna suala la wire transfer....kinachifayika is just deposit kwahiyo haina maana yoyote ku-charge....kwa lugha nyingine ni kama una-discourage deposit mobilisation!
 
Hawa ni wezi kweli, hivi haya mapato 1000/- huwa yanakatwa kodi? Wakati mwingine kwenye zile benki ambazo hazina kamera hawa tellers huwa wanachukua hizo buku buku zetu kwani hakuna monitoring ya kujua kuwa anayeweka ni mwenye akaunti au la, anayejua ni teller tu hivyo hata akila hakuna atakayejua na pia hizo gharama ni za nini maana hakuna tofauti mwenye akaunti anapoweka fedha kwenye akaunti yake na mtu mwingine anapoenda kumwekea. Kama tofauti ipo naombeni mnijulishe

Je, hizo buku buku zinaandikiwa CR vourcher?! Kama haziandikiwi, basi zinaliwa na tellers lakini kama zinaandikiwa; no way wanwea kuzitafuna kv mtu anyefanya calling (entries VS Vourchers) lazima atadai hiyo vocha. By the way, kama unatoa 1000/= nawe hupewi Cr vourcher basi unaabiwa kwa kutaka mwenyewe...!
 
Mkuu kote nchini hata ARUSHA hilo tatizo lipo na hasa unapomtumia pesa mtu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.Lakini kwa taasisi za serikali mfano vyuo vya serikali na halmashauri hautozwi hela.
Waziri mkuu (mtoto wa mkulima) alishalitolea kauli hili kuwa wasiwatoze wateja wao buku,lakini wamedharau na kulikaidi agizo lake,sijui ilikuwa siasa!

we unafikiri serikali yako ina say yeyote!! Wenyewe wameuza hisa!
 
Buku buku hizo kwa ajili ya mateller ili wapate japo kikombe cha maziwa chezea vumbi la hela weye!!!!
 
Hii biashara ya buku buku ilishaondolewa toka tarehe 15 Jan 2012 tena walibandika tangazo walipobadilishabaadhi ya rate zao, hao mateller watakuwa wanakupiga mkuu nenda kwenye ubao wa matangazo utaona hilo tangazo.
 
NMB toeni tamko kupitia vyombo vya habari, hii habari ya kuchukua buku buku zetu bila maandishi inakuwaje, kama ipo isemwe na sababu za kuwepo kwake, kama haipo isemwe pia, manake hawa mateller wanaidai utadhani malipo ya choo cha stendi (LIPA KWANZA)
 
Ebwana me nliwaona wezi eti ukiomba bank statement unakatwa buku, mbaya zaidi ni atm card, kama uko mbali na branch ulipofungulia hyo akaunt, kutumia atm card yako ni buku 15.
 
Ebwana me nliwaona wezi eti ukiomba bank statement unakatwa buku, mbaya zaidi ni atm card, kama uko mbali na branch ulipofungulia hyo akaunt, kutumia atm card yako ni buku 15.

Buku 15! Tell me you are joking.
 
Back
Top Bottom