Wizi wa mabegi/mikoba na simu kwa kutumia magari, pikipiki,na kwa miguu washamiri Dar

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
WIZI WA MABEGI/HANDBAG NA SIMU KWA KUTUMIA MAGARI, PIKIPIKI NA KWA MIGUU WAKITHIRI DAR

Hivi karibuni kumekuwa na kuthiri kwa wizi wa aina ya uporaji wa magi na pochi pamoja na simu kwa kutumia magari, pikipiki na kwa miguu. Ni muhimu sana kwa jamii kuwa makini na kufuata ushauri huu hapa chini

  1. wakuwa waangalifu na mazingira unayopita
  2. beba begi lako au handbag kama ni muhimu au toa vitu vya thamani kama ni lazima upite maeneo hatarishi
  3. Usitumie simu unapotemmbea maeneo hatarishi au usioyajua
  4. Kama umemeba mkoba wako basi ushikilie na kumbatia kwa makini sana
  5. Tembelea upande umbao utayaona magari yanapokuja
  6. sehemu hatarishi hakikisha unatembea na mtu mwingine
  1. Kama bahati mbaya ndio umebiwa mkoba wako basi usiung'ang'anie, achia mkanda wake kwani waweza kuburuzwa na kusababisha majeraha makubwa zaidi
  2. chukua namba za gari na ripoti polisi mara moja
CHUKUA TAHADHARI!
----------------------------------------------------------------------
BAG/CELLPHONE SNATCH

As usual TI RESPONSE TEAM continues to issue alerts after learning about incidents/crime.

BACKGROUND
Recently, the bag and mobile phone snatching has increased by gang of thieves on motorbike and vehicle in Dar es Salaam region. Example at Upanga area, Mikocheni and Recently near DTV round about.

WHO ARE THE TARGETS?
Those walking on the streets carrying handbags, laptop bags & talking on the cellphone.

It is important to take necessary precautions while walking; Few tips are as stated hereunder :-

1. Beware of the surroundings that you are walking.

2. Carry the handbags, Laptop bags only when it is necessary.

3. Avoid talking on the cell phone while walking on the streets.

4. If carrying your handbag or laptop bag is necessary; hold it firmly across your shoulder and not hanging ( shorter belt)

5. Use pedestrian walkway paths (Avoid walking on the streets, while holding the bags or talking on the cell phone).

6. Incase you are carrying a bag or talking on the cellphone; Ensure its on opposite direction to the moving vehicle or motorbike.

7. Walk on opposite direction.

INCASE YOU ARE A VICTIM ALREADY:-

Use the following tips

1. Don't panic

2. Ensure that the belt of the bag that you are carrying has been removed or else you will be dragged for a longer distance and suffer major injuries.

3. Take note of the registration number of the vehicle.

4. After the incident runaway to the side aways; to minimize the chances of being run over by another vehicle.

5. Report to police.

TI Response Team
 
Ungetaja maeneo kabisa tujue moja BTW hawa watu wanajulikana nina imani hiyo wapo humu humu kwenye bar zetu tunazokunywa na wanatembea na akina dada hawa hawa tunaogegedana nao ila nashangaa sijui kwanini hawakamatwi...
 
Huu mchezo uko kila mahali hapa dsm, sana sana sehemu za starehe, na alfajiri nina matukio ma 4 ya watu tofauti
1. Aunty yangu Jumapil alikuwa pale cape town fish market, mida ya saa tano akiwa anatoka jamaa wakampitia na gari wakampora pochi ina dola 900, credit cards, us green card, work ID's, na ndio alikuwa amefika kwa kukaa wiki 1

2. Shemeji yangu alikuwa anatoka nyumbani saa 12 maeneo ya sala sala, jamaa wa boda boda wakampitia alivyong'ang'ania pochi wakamtolea sime ya kimasai ikabid aachie tuu

3. Nilishuhudia kwa macho yangu pale coco beach kwenye mihogo jamaa ya boda boda wamemkanyaga mdada wanampora pochi

3. Leo asubuh karibu na ofisin kuna dada kaporwa pochi jamaa wakiwa na sime ya kimasai

Hali inatisha ni ngumu kupambana na hawa watu hasa mida ya alfjir watu wakiwa wanaenda kupanda dala dala
 
Maeneo ya oyster bay na masaki wadada wanaporwa sana mipochi yao
 
Hii inatokana na hali ngumu ya maisha. Sasa hivi waalifu hawajali na hawaogopi kabisa kuiba hadharan. Nchi kamwe haiwez kuendelea kama hamna usalama wa raia.
 
Maeneo ya MLALAKUWA wanaiba vifaa vya magari hasa kwenye baa hasa Calabash, Brajec etc.
 
Ungetaja maeneo kabisa tujue moja BTW hawa watu wanajulikana nina imani hiyo wapo humu humu kwenye bar zetu tunazokunywa na wanatembea na akina dada hawa hawa tunaogegedana nao ila nashangaa sijui kwanini hawakamatwi...
Masaki along haile selassie road,chole road,toure drive, oysterbay area....huku kuko kimya sana kwahio wezi wanapapenda sana!
 
Kama magari yapita upande wako wa kulia we basi beba pochi yako upande wa kushoto
 
Back
Top Bottom