Wizi wa laptop katikati ya jiji

na nyie mmezidi ushamba mnatembea na laptop za nini?fanya kazi ofisini muda ukiisha nenda home acha kitendea kazi ofisini...acha wawapore bana

Katika Computing eras, tupo katika kipindi cha mobile computing. Hivyo kutembelea na laptop ni sawa kabisa. Na ushauri wako ni sawa na kumwambia mtu aache cellular phone nyumbani au ofisini, eti kwa sababu simu za waya zilikuwa za nyumbani na ofisini.
 
Siwezi kuacha Laptop yangu kwani ni ofisi popote na ofisi zingine hazina net ndugu kwa hiyo inabidi ufunge safari ,mimi hutumia backpack ya kawaida sana si rahisi kugundua ndani ya hiyo backpack kuna issue huenda mtu anichomee,pia ndugu zangu lazima uwe na sehemu ingine ya kuhifadhi docs zako badala ya kila kitu kukiweka kwenye laptop ni bora hata uwe unahamisha docs zako kwa kuweka kwenye CD,HD or flash pia kuhifadhi kwenye email ingawa hii ya email si salama sana lakini angalau utakuwa na sehemu ya kukimbilia baada ya wajanja kukukwapua ,oh sasa siendi tena IFM
 
bht

You made my day! Nimecheka kuona mwizi ametumia mbinu na nguvu nyingi na kuishia na videsa!

Hasara zaidi inakuwa kwa mwanafunzi.
 
na nyie mmezidi ushamba mnatembea na laptop za nini?fanya kazi ofisini muda ukiisha nenda home acha kitendea kazi ofisini...acha wawapore bana

Sheikh...fikiri kidogo...Kuna overtime nyingine zinapigiwa nyumbani.Besides kuna watu laptops ndo ofisi zao.
 
na nyie mmezidi ushamba mnatembea na laptop za nini?fanya kazi ofisini muda ukiisha nenda home acha kitendea kazi ofisini...acha wawapore bana

Kaka Laptop sio lazima iwe ya ofisi, yaweza kuwa ya binafsi na pengine ndiyo unayoitumia sehemu zote unazokuwepo hasa kwa wale wanaoingia kwenye mtandao wa internet kwa kutumia wireless connection huna haja ya kuacha Lap top nyumbani au ofisini wakati muda wote unaitumia kwa mawasiliano.

Tuseme tu kwamba kama hali imekuwa mbaya kiasi hicho tuchukue tahadhari, kama hauna usafiri hali ni mbaya zaidi. Yaweza kusaidia kuachana na handbags zenye chatter za computer kama dell,compaq, sonny , toshiba nk. Badaya yake tutumie mikoba isiyo kuwa ya laptop original ikibidi kwa kuwa usalama kwanza weka laptop yako kwenye kikapu, mradi tu kikapu hicho kiwe kinazip na inafunga. Naamini itakuwa ni salama zaidi kuliko ku risk milioni zako, na data kwa pamoja.
 
kubeba laptop sio ushamaba, elewa ile imetebgenezwa kwa ajili ya kufacilitate mobility, pia wengine kazi zetu sio za kukaa kwenye meza tangu asubuhi hadi jioni so we have to move so i wish kama ungejua umechemsha kusema laptop ni ushamba,

kwa ushauri ni vizuri kuwa na back up , mimi nina external drive na huwa ninafanya backup kila mwisho wa mwezi au hata mara 2 kwa mwezi. na na kwa wale wanaoweka laptop siti za nyuma za gari ( sallon cars) nairobi wanajivunjia kioo cha nyuma gari likiwa kwenye jam wanaondoka nayo, bestway weka chini ya seat ( unapoweka miguu) ili isimtamanishe alieko nje

Jaribu kuelewa kilichoandikwa kabla ya kujibu
 
na nyie mmezidi ushamba mnatembea na laptop za nini?fanya kazi ofisini muda ukiisha nenda home acha kitendea kazi ofisini...acha wawapore bana

Mkuu ingekuwa Desktop Computer tusingebeba !! Tunahitaji kuwasiliana na watu na kufanya shughuli zingine za ziada majumbani nyakati za jioni na wk end !! Hahaaaa Mkuu hata kubeba Laptop pia waita ni Ushamba !!!!!
 
Rafiki yangu aliibiwa laptop baada ya walinzi kuvunja kioo cha gari pale karibu na St. Peters. Walinzi wamekamatwa lakini hawajasema laptop ilipo na wako nje kwa dhamana.
 
Back
Top Bottom