Wizi wa kutisha Benki

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Kwa siku kadhaa sasa, wizi wa kutisha unafanywa na raia wa kigeni katika benki kadhaa nchini, hasa NBC. Akaunti za wateja wengi zimekombwa kabisa fedha, na sasa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wateja. Washiriki wa wizi huu ni raia wa Afrika Magharibi, hasa Nigeria na baadhi ya wazungu kutoka mataifa ya Ulaya. Benki ya NBC imeanza taratibu za kuwarejeshea fedha baadhi wa wateja waliolizwa. Nina ndugu yangu ambaye asubuhi hii kaibiwa Sh milioni 4.65.
 
Wanaibaje? Huyo Ndugu yako mwambie aweke wazi kaibiwaje ili nasi tuchuke tahadhari...
 
Wanaibaje? Huyo Ndugu yako mwambie aweke wazi kaibiwaje ili nasi tuchuke tahadhari...

Wanachofanya hawa matapeli ni kwamba wanachukua fedha kupitia ATM Machine. Si lazima wapate kadi yako. Wanachofanya ni kuingia kwa mbinu wanazojua wao, na mashine zinatema fedha. Utashangaa ATM Card unayo, tena umeitunza vizuri nyumbani, lakini fedha benki zinayeyuka. Aina hii ya wizi imekuwa ya kawaida katika mataifa ya Afrika Magharibi. Nigerians, wanaongoza sana kwenye ushenzi huu. Kwa kifupi ni kwamba wakiingia kwenye akaunti yako, huna mbinu ya kuziokoa fedha zako!
 
hili Tatizo lipo na alitoisha Tanzania Mpaka pale Ubabahishaji wa Police kitengo cha Fraud,utakapoisha.Tutaendelea kulalama wee ila at the end lazima ubabaishaji uishe,
 
Tanzania mpaka uchunguzi uje ufanyike juu ya huu wizi na majibu yakapatikana lazima kwanza zitaundwa tume kama kumi hivi watu wale posho halafu majibu baada ya miaka kama kumi hivi.............
 
Ma benk wako nyuma ya technolojia wezi wako mbele ki tecknolojia ila kuna mabenkinyanayoibia wateja wake kwani kuna wale vijana wa DBM (data base management) wajiriwa wa bank
Hao ndio wezi wa kutupwa wanachokifanya ni kuchukua a/c namba ya mteja na yeye anakuwa na a/c hapo hapo hivyo ukute anakuwa ana numbers za wateja lets say 1000 wa benk zile ambazo zinafanya transaction yeye anakuwa anaziona so utakuta anachukua hata ome amounts, wapo wanao hack ac ya mteja and they are very bright since they walk kinyume nyume katika ku hack huko hawaachi marka (wataalamu wa hacking ) watakuwa wanielewa
So hela hata ikiingia kwenye account yake anaifuta marks alizofuta baadae anaihamisha kwa account ya mtu mwingine rafiki yake ili msiweze kumshtukia halafu anafuta marks na anaitoa kwa rafiki yake kwenda kwa mtu mwingine utakuta ana watu kama 10 kwa mchezo huo halafu wana withdraw kidogo kidogo mpaka wanagawana pesa mazima
Achana na wale mapopo ambao wanaiba kwenye atm wizi wa kizamani huo
 
Ni kweli tatizo kubwa la mabenki yetu yananunua teknolojia ambazo ni mitumba na zilishatumika huko nje kitambo, hivyo jamaa walio mbele ki teknolojia lazima wataendelea sana kupiga kwenye mabenki hapa nchini. Kama sio hivyo basi kuna in side job hasa jamaa ta IT kwenye hayo mabenki.
 
Jamaa angu aliibiwa milioni 2 kwa mtindo huo tena CRDB na alipofuatilia zile kamera hazikuwa zinaonesha picha ang'avu bali mawinguwingu!
 
Kwa siku kadhaa sasa, wizi wa kutisha unafanywa na raia wa kigeni katika benki kadhaa nchini, hasa NBC. Akaunti za wateja wengi zimekombwa kabisa fedha, na sasa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wateja. Washiriki wa wizi huu ni raia wa Afrika Magharibi, hasa Nigeria na baadhi ya wazungu kutoka mataifa ya Ulaya. Benki ya NBC imeanza taratibu za kuwarejeshea fedha baadhi wa wateja waliolizwa. Nina ndugu yangu ambaye asubuhi hii kaibiwa Sh milioni 4.65.

Ndugu zangu wakati nimetoa Tuhuma kama hii hapo jana kuhusu "NBC Benki si Salama" baadhi ya Raia wema walinielewa. Wengine hawakunielewa vizuri. Kwa kifupi ni kwamba, Wizi huu wa Pesa za wateja katika Account zao, unafanywa ndani kwa ndani, tutasingizia utapeli wa Mtandao, pengine ni kweli kwa upande mmoja. Lakini mimi ninayo hakika kuwa kuna genge la wahuni wezi wako ndani kwa ndani wakishirikiana na wale wa nje. Naiomba tena Secret Service Ofisi ya Rais, Kamati za Bunge, Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, Usalama wa Taifa, Polisi Kitengo cha Fraud, Tume/mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (IT) Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na vyombo vyote vya Usalama hata Intelligence ya Jeshi la wananchi kitengo cha Fedha, Uhasibu na IT, wapeleke timu za Upelelezi na Uchunguzi wa Kina katika Benki Hii ya NBC. Kuna mchezo mchafu ndugu zangu. Hapa JF ndiyo mahali pekee salama pa kuanika Uozo.
 
Wanachofanya hawa matapeli ni kwamba wanachukua fedha kupitia ATM Machine. Si lazima wapate kadi yako. Wanachofanya ni kuingia kwa mbinu wanazojua wao, na mashine zinatema fedha. Utashangaa ATM Card unayo, tena umeitunza vizuri nyumbani, lakini fedha benki zinayeyuka. Aina hii ya wizi imekuwa ya kawaida katika mataifa ya Afrika Magharibi. Nigerians, wanaongoza sana kwenye ushenzi huu. Kwa kifupi ni kwamba wakiingia kwenye akaunti yako, huna mbinu ya kuziokoa fedha zako!

Then kunatatizo kubwa kwenye Idara yao ya Kompyuta...either hawana mfumo mzuri wa kompyuta au watumishi wao hawana ujuzi or yote mawili...!!! with all the technology in the market?!
 
Wanachofanya hawa matapeli ni kwamba wanachukua fedha kupitia ATM Machine. Si lazima wapate kadi yako. Wanachofanya ni kuingia kwa mbinu wanazojua wao, na mashine zinatema fedha. Utashangaa ATM Card unayo, tena umeitunza vizuri nyumbani, lakini fedha benki zinayeyuka. Aina hii ya wizi imekuwa ya kawaida katika mataifa ya Afrika Magharibi. Nigerians, wanaongoza sana kwenye ushenzi huu. Kwa kifupi ni kwamba wakiingia kwenye akaunti yako, huna mbinu ya kuziokoa fedha zako!
shida huwa inaanza kama ukifanya online payment au transaction,kwaio kuna website ambazo huwa ni fake wanatengeneza,mfano mzuri dating site,wanakwambia ulipie kwa kutoa details za akaunti yako ya benki then ukirogwa kutoa wao ndo wanazichukua na kuanza kutafta pasword,kadi huwa wanatengeneza fake,kwaio hawa watu ni hatari sana,na huo uharifu hawawezi fanyia kwao kule wamesha wadhibiti wanachokifanya ni kutafuta mahali penye lines of weakness kama hapa Tanzania
 
njia ya kunguza hayo matatizo ni kujiunga na sim banking kama mimi natumia CRDB kwenye akanti yangu pesa yoyote ikitoka inanitumia ujumbe hapo hapo na kinitahadgarisha kama sitambui muamala huo nipige namba flani.
 
Kwa siku kadhaa sasa, wizi wa kutisha unafanywa na raia wa kigeni katika benki kadhaa nchini, hasa NBC. Akaunti za wateja wengi zimekombwa kabisa fedha, na sasa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wateja. Washiriki wa wizi huu ni raia wa Afrika Magharibi, hasa Nigeria na baadhi ya wazungu kutoka mataifa ya Ulaya. Benki ya NBC imeanza taratibu za kuwarejeshea fedha baadhi wa wateja waliolizwa. Nina ndugu yangu ambaye asubuhi hii kaibiwa Sh milioni 4.65.

Mkuu hao wana hack akaunti yako benki na kuhamishia pesa zako zote kwao. Huu mtindo ulikuwa common Nigeria na hata Uganda sasa kama umeingia bongo tuwe makini sana na ATM cards zetu zisiwe visible na hata risiti usiiachea pale kwenye atm bila kuichana ni hatari namba yako tu ya akauti yatosha kufanya mambo.
 
Kifupi ni kuwa wizi huu unahusisha mtandao mrefu kuanzia wafanyakazi wa benki husika hadi hao watekelezaji wa zoezi.
Majukumu yao huwa kama ifuatavyo:

Matapeli - kupata taarifa za mteja ikiwamo jina halisi, card number, A/C Number, na kufanya drawings.
Bank Staff - Kujua kiwango cha fedha kwenye akaunti, Kutengeza ATM Card nk.
 
Ndugu zangu wakati nimetoa Tuhuma kama hii hapo jana kuhusu "NBC Benki si Salama" baadhi ya Raia wema walinielewa. Wengine hawakunielewa vizuri. Kwa kifupi ni kwamba, Wizi huu wa Pesa za wateja katika Account zao, unafanywa ndani kwa ndani, tutasingizia utapeli wa Mtandao, pengine ni kweli kwa upande mmoja. Lakini mimi ninayo hakika kuwa kuna genge la wahuni wezi wako ndani kwa ndani wakishirikiana na wale wa nje. Naiomba tena Secret Service Ofisi ya Rais, Kamati za Bunge, Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, Usalama wa Taifa, Polisi Kitengo cha Fraud, Tume/mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (IT) Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na vyombo vyote vya Usalama hata Intelligence ya Jeshi la wananchi kitengo cha Fedha, Uhasibu na IT, wapeleke timu za Upelelezi na Uchunguzi wa Kina katika Benki Hii ya NBC. Kuna mchezo mchafu ndugu zangu. Hapa JF ndiyo mahali pekee salama pa kuanika Uozo.

NITAKUSAIDIA WEWE NA WENGINE

Mchezo huu hauko katika benki ya NBC pekee bali sasa umeingia katika benk zingine mfano ni NMB na CRDB....
rais wanaofanya mchezo huu ni raia wa bulgaria na wengine wa afrika magaribi......watu hawa huwa ni pair ya watuwawili na mara nyingi ni mwanamke anashirikiana na mwanaume......hawa watu huwa wanalenga matawi hasa yale yanaoyoonekana kuwa na ulinzi hafifu ...namaanisha kwamba kuna baadhi ya ATM mashine ziko sehemu za mbali na zilipo benk n lakipi pia hawa watu wanaweza kuingia hata benk iliyoko mjini yenye ulinzi imara....kinachofanyika ni hiki:

1. wakifika kwenye ATM yoyte ilehawa watu hupachika chip ..chip hizi ni ndogo sana.chip moja hupachikwa kwa juu usawa na pale ilipo sehemu ya kuingizia ATM palipo na na zile button zinazotumika kuingizia namba ya siri.....

2.. mteja akifika na kutoa kadi yake mfuko na kuitumbukiza kwenye ATM....zile namba za kadi huweza kumezwa na chip hiyo na pia anapoingiza namba ya siri pia chip hiyo huweza kuchukua namba hizo za siri...

3.. chip hiyo huweza kuachwa hapo hata kwa siku nzima na baadae wahusika hufika nakuichukua chip hiyo...(wanaingia ndani ya ATM kama wateja wanaochukua pesa) kisha huichukua chip hiyo

4. wakiondoka hapo chip hiyo huweza kuingizwa kwenye laptop na hivyo kuritrieve information zote na wanazitoa na kuzisave kwenye pc...

5. taarifa wanazotoa kwenye chip hiyo ni anmba ya siri ya mteja na namba ya kadi ya ATM...

6. baada ya hapo watu hao huwa wana universal atm card na hivyo huweza kwenda benk yoyote na kutoa pesa hizo kutoka kwenye akunti za wateja wengine.....

7..watu hawa hulenga zaidi benk zenye visa, master card nk...maana ni rahisi kuchukua pesa toka benk yoyote...

.........
juzi kuna tukio la mwenzetu mmoja hapa yeye alikuwa anatoka malawi na alipofika iringa alienda tawi la CRDB pale iringa na kuchukua pesa....kisha akaendelea na safari kwente akauti aliacha mil 16 na ushee..... baada ya siku 5 akaenda tena benk kuchukua pesa (dar) na alpofika akakutta salio ni tsh 8000/= tu..... baada ya kufatilia na kuomba statement akaona pesa zake zimechukuliwa na mtu akiwa maputo msumbiji... katika moja ya benk za huko.... tumefatilia na watu hao tayari wamekamatwa huko na wamekiri walikuwa tanzania mikoa ya iringa na dsm......

vi chip hivyo ni vidogo sana ukifika kwenye atm huwezi kuviona kwa urahisi na pia wegi wakifika kwenye atm hufikana kuingiza kadi moja kwa moja.....

kuweni makini na pia jambo hilo hasa benk ya NBC wamepewa tahadhari maana technology yao ni ya zamani
 
Back
Top Bottom