Wizi wa kura

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,081
5,061
Tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi na ushiriki wa vyama hivi katika chaguzi pamekuwa na malalamiko mengi kuhusu wizi wa kura.
Ninanzisha uzi nikiamini kuwa vidonda vya uchaguzi vimekauka na nafsi zimetulia hivyo michango itakuwa mizuri bila ushabiki mkubwa.
Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa na ushindani mkubwa na tuhuma za wizi wa kura zimesikika sana ila mpaka leo sijaona ushahidi ukiwekwa mezani.
Naomba wale wote waoamini ya kuwa kura ziliibiwa watusaidie kueleza kuwa ziliibiwa vipi na kwa jinsi gani ushahidi ulipotezwa.
Karibuni waungwana.
 
Mkuu sina ushahidi kwa sababu kazi yangu sio kufanya upelelezi. Nikuulize tu swali moja, kwa mujibu wa mwenyekiti wa NEC, walijiandikisha watu wangapi kupiga kura? Na baada ya uhakiki wa daftari la kupiga kura unakumbuka walisema kuna wapiga kura halali wangapi? Umewahi kufuatilia takwimu za matokeo ya uchaguzi kuona kura zilizopigwa, zilizoharibika na halali kama zinashabihiana na takwimu za awali za NEC? Kama matokeo yote kuanzia rais hadi udiwani yalikua yanabadikwa vituoni kulikua na haja ya kuzuia watu kujumlisha matokeo ya vituo vyote? Unawezaje kusema kura ziko sawa wakati kuna maelezo yanayotofautiana kuhusu idadi ya waliojiandikisha kupiga kura?

Wengine wataendelea....
 
Mwanzo mzuri.Nashukuru.Ngoja tuwasubiri wadau.
 
Tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi na ushiriki wa vyama hivi katika chaguzi pamekuwa na malalamiko mengi kuhusu wizi wa kura.
Ninanzisha uzi nikiamini kuwa vidonda vya uchaguzi vimekauka na nafsi zimetulia hivyo michango itakuwa mizuri bila ushabiki mkubwa.
Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa na ushindani mkubwa na tuhuma za wizi wa kura zimesikika sana ila mpaka leo sijaona ushahidi ukiwekwa mezani.
Naomba wale wote waoamini ya kuwa kura ziliibiwa watusaidie kueleza kuwa ziliibiwa vipi na kwa jinsi gani ushahidi ulipotezwa.
Karibuni waungwana.
MIGNON hakuna kura iliyoibiwa. Sababu za chama kilichokufa na nyeupe wao kusema kura ziliibiwa ni:
  1. Kuwapa matumaini hewa wanachama wao
  2. Kwa kusema tulishinda ila basi tumeibiwa
  3. Ili kujenga chuki kati ya aliyeshinda (Dkt Magufuli) na wale wote (wachache wa upinzani) waliowapigia upinzani
  4. Pia ili kuhakikisha wanakuwa na uungwaji mkono na kundi lile lile ktk uchaguzi unaofuata
  5. Kuonesha kuwa wamedhulumiwa ili kupata huruma ya kuchangiwa hela za kujikimu wapinzani
 
Nashukuru pia ila naomba umsome aliyetangulia na tuangalie kama kweli ukweli katika aliyosema.
 
Chaguzi zet bado sana, udanganyifu kibao,inabidi kukomaa kama jiwe, watu wanakusanya matokeo yao kadri wanavyoyapata wanakamatwa na kunyan'ganywa vifaa.Hivi tabu ilikuwa nini kama matokeo waliyokuwa wakikusanya hayakuwa halali si yangelinganishwa tu kule yalikotoa, ya tume na ya wao walionyan'ganywa vifaa walogopa nini? kwa mtindo huo walichofanya kwa nini watu wasihofu kuwa kulikuwa na wizi wa kura
 
Back
Top Bottom