Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...

Ingia kwenye skype ( download) kisha jiandikishe. Ukiwa umeshajiandikisha wape member address yako ya skype wakikupata unaweza kuwatumia through skype na hata kuongea bure. Unaweza kutuma kwa skype kama wote mko online file la ukubwa wowote japo inachukua muda. Laini unaweza kuendelea na mambo mengine ikiwa inatuma. Pia nimejaribu kutumi computer ya mpendwa mmoja hapa inayoweza kubadilisha hilo file lako liwe pdf ili lisiweze kubadilishwa. Penye wengi pana mengi. Litume likiwa pdf. Ninakuambatanishia pdf hapa.
Nitakutumia msg ya simu pia.
 
Tumia hii pdf file. Hapa tuko wengi file la kawaida laweza kubadilishwa na yeyote. PIa nimekupa maelekezo ya kujiunga na skyp;e kisha wape watu address yako ukishawaona unaweza kutuma file la ukubwa wowote pamoja na kuongea kwa simu bure. Hata kwa video. Hata hivyo kama inachukua muda kulituma unaweza kuendelea kufanya shughuli zako nyingine ili mradi unayemtumia awe alishakubali.
 
Hata hivyo na mimi mwenyewe nimeamua kutafuta namna ya kuiconvert into VCD ya kama MB 300 hivi. Nikifanikiwa nitakuja tena kwenu kwa maelekezo.

Mungu awabariki sana!!!

Mkuu mchango wako ni mkubwa,, na shughuli iliyobaki hapo ni ndogo tu ni ya kuconvert hiyo vcd to MP4 au FLV then kuiupload kwenye you tube. Kama unaweza kuni-PM ni wapi naweza pata copy ya hiyo vcd kwa hapa dar nitaitafuta then nisaidie kumalizia hapo palipobaki ili elimu hiyo ifike kwa wengi.
 
Nimeisoma na kuikiubali hii thread ya Kamembe, ila mara nyingi wizi mkubwa hufanyika wakati wa kusafirisha masanduku:
Kinachofanyika huwa ni kubadilisha kura ndani ya masanduku na kuyajaza za ccm, halafu fomu alizotaja Kamembe zinabadilishwa. Ni wazi kuwa fomu zilizobadilishwa hazitakuwa na saini za mawakala wengine isipokuwa wa ccm ambaye anahusika moja kwa moja na ubadilishaji huo. Mnapofika kwenye jimbo wakati wa majumisho na kuhakiki, utaona matokeo katika fomu ya wakala wa chama cha upinzani (CHADEMA) ni tofauti na yanayotajwa na msimamizi! Hapo patatokea malalamiko, fomu ya wakala wa ccm itasema sawa na msimamizi alivyosoma, lakini ya CHADEMA tofauti - ubishi huo utapelekea kuhakiki physically kilichomo ndani ya sanduku; hapo ndipo utakuta viroja -kura zimeshabadilishwa ndani ya sanduku, utakuwa huna ujanja tena maana sanduku ndiye msemakweli!
Ndiyo maana mimi nikapendekeza wakala kunukuu namba za karatasi za kupigia kura ili wakati wowote namba hizo hizo ndizo ziwemo ndani ya sanduku- period
Hii itafanya wizi uwe mgumu kwani itabidi wawe na karatasi zenye kufanana namba, na wawe wamepredict vituo watakavyoshindwa.
Pili nikasema wakala aandamane na sanduku lake hadi mwisho wa safari kwa msimamizi wa jimbo na si kwa mtendaji wa kata.
Mkakati narudia tena hapa:(unganisha na elimu nzuri ya Kamembe)
Kwa kuwa kila karatasi ya kupigia kura huwa ina namba, na kwa kuwa kila msimamizi wa kituo hukabidhiwa vitabu hivyo kwa namba; yafuatayo yafanyike

1)Kila chama kipate nakala ya namba za vitabu vya kupigia kura vilivyopelekwa kila kituo
2)Mawakala waelekezwe kunukuu namba za vitabu kwenye kituo kabla upigaji kura haujaanza na msimamizi awadhibitishie kuwa hivyo ndivyo vitabu alivyopokea toka msimamzi wa jimbo
3) Iwe ni lazima kwa kila wakala kusaini fomu ya matokeo kituoni na kama ana malalamiko yoyote yale ajaze kwenye fomu ya malalamiko (unajua mkiachia wa CCM pekee akasaini, hata ikijabadilishwa anatafutwa huyo mmoja anasaini na mchezo unakuwa umeisha)
4) Wakati wa kuhesabu kura, iwe vituoni au wakati wa kuhakiki katika ngazi ya jimbo (ambako huwa ndipo matokeo huwa yameshachakachuliwa), kila sanduku la kura lihesabiwe peke yake na ihakikishwe kuwa namba za karatasi zilizozomo zinaoana na namba alizokuwa amekabidhiwa msimamizi wa kituo na mawakala wawe wametoa taarifa kwa vyama vyao juu ya namba zilizotumika kwenye vituo vyao.
5) Kwa kuwa mawakala ndio wameaminiwa na vyama vyao, wayasindikize masanduku ya kura hadi jimboni pale uhakiki na utangazaji unapofanyikia. Kuyasindikiza hadi kwenye kata na kuishia hapo hutoa mwanya kwa watendaji wa kata kushirikiana na CCM kuyabadili. Sanduku lolote litakalowasilishwa bila mawakala litengwe na lihasabiwe tofauti na kama litakuwa na kura tofauti na fomu za mawakala, likataliwe - Nakumbuka hii ilifanyika Temeke wakati Mrema akigombea. Ni marufuku mawakala kusafiri tofauti na masanduku yao - magari yabebe masanduku kidogo na mawakala.

Mkuu, tunakushukuru kwa mchango mzuri... mimi nashauri MOD Invisible waanzishe GRAPHICS representation ya Tanzania nzima yenye kuonyesha idadi ya kura walizopata wagombea na vyama vyao... hii itazuia uwizi wa kura hususan wakati wa majumuisho kwenye majibo...
 
tunaisubiri hiyo DVD kwani hata maeneo kama tarime na moshi itatusaidia kulinda kura za chama tawala,chama makini,chama cha siasa,si makampuni ya kisiasa!
 
Mimi nilifikiri kuwa kura zinahesabiwa kituoni, hii ya kusafirisha inatokea wapi? Wanajamvi nijuzeni!
 
NImepokea ombi la Jatropha la kuirejesha tena hii post jukwaani.
MOds naomba mtusaidie ikawie kuondolewa ili wengi wapate huu mwongozo wa mafunzo ya MAWAKALA
 
Habari zilizozagaa kwenye tovuti mbalimbali ya kuwa TRA wamekamata shehena ya mfanya biashara maarufu wa kampuni ya AZAM Bw. Said Bakhresa, kuwa lori lake lilisheheni karatasi za wapigakura ya URAISI ambazo tayari zimekwisha kupigwa "NDIYO" kwenye picha ya Raisi anayetarajiwa kubwaga manyanga baada ya uchaguzi huu, Bw. JK zimeleta hisia kali miongoni mwa wapigakura kuwa hakuna namna CCM inaweza kufanya hujuma hii ya kuwadhulumu wapigakura bila ya kuwa imepata mwanya kutoka kwa NEC.

NEC hivi sasa ambayo wajumbe wake wote ni teule ya Jk hakuna mpigakura anayeiamini hata chembe kutokana na maamuzi yafuatayo ambayo imeyafanya:-

1) Kufuta haki ya wapigakura kuwa mita 200 kutoka kwenye vituo vyao vya kupiga kura. Hii inaashiria ya kuwa NEC wapo beneti na CCM katika kuhakikisha ya kuwa kura bandia zinapoingizwa kwenye vituo vya kupiga kura wapigakura hawatakuwepo kuzuia au kukamata ushahidi wa uovu huo.

2) Kuanzisha matumizi ya tekinolojia nyingi na ambazo ni rahisi kurubuniwa na mitambo ambayo si rasmi na hivyo kufanya uwepo uwezekano mkubwa wa kucheza na kuyachakachua matokeo halisi ya uchaguzi huu.

3) NEC kutowapigania wapigakura wa vyuo vikuu wapatao 60, 000 na kuanza kutupiana mpira na serikali ya CCM ikithibitisha zaidi wanajua wanachokifanya hapo. NEC wangeliweza kabisa kuahirisha uchaguzi kwa wiki moja ili wanafunzi hao wapate haki yao ya kupiga kura lakini kamwe NEC haitafnya hivyo kwa sababu lengo ni kupunguza kura za upinzani

4) NEC siyo mgeni katika kucheza rafu. Mwaka 1995, ilichelewesha vifaa vya kupiga kura Mkoa mzima wa Dar-Es-Salaam ili kuilinda CCM iliyokuwa inadondoshwa vibaya hapo. Kama wapo tayari kufanza hivyo siku hizo ni lipi la kuwazuia safari hii kucheza rafu tena za kisomi zaidi?

5) Hadi sasa NEC haijatoa tamko rasmi la kupinga au kukubali kuwa chaguzi hii tayari imeingiwa na dosari ya kura za JK kujaribu kuingizwa kinyemela huko Tunduma na mfanya biashara wa kiarabu Bw. Bakhresa na kampuni yake ya AZAM kuingiza kura haramu hizo. Hili linaongeza mashaka ya kuwa NEC ni sehemu ya mkakati huo ndiyo maana imekaa kimya.

6) NEC ndiyo waliochapisha kura hizo sasa inakuwaje JK na watu wake wajue NEMBO hizo kama siyo NEC hao hao waliovujisha NEMBO hizo? NEC walidai wameikodisha kampuni kutoka UK ili ifanye kazi ya kuchapisha kura kuondoa malalamiko kama yaliyojitokea sasa yawaje Afrika kusini wameweza kuziiba nembo hizo na kuzichapisha. KAMA UFEDHULI HUU NI WA KWELI BASI NEC inabidi iwajibike na kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapigakura na chaguzi ikaahairishwa na tukajipanga upya

7) Kutokana na ukimya wa NEC wa kuvuja kwa NEMBO zake za uchaguzi na wao kukaa kimya wapigakura wana kila sababu ya kuutilia mashaka uchaguzi huu kama utakuwa ni huru na wa haki. NEC walipaswa kutoa tamko kama ni la kukiri basi kutoa tenda nyingine ya kuzuia NEMBO zilizoibiwa kutumika tena katika uchaguzi huu....

8) Tamko la JWTZ la kuwatisha wapigakura kutoleta fujo baada ya matokeo kutangazwa liliashiria ya kuwa CCM yaelewa kuwa wapigakura hawataafiki matokeo yatayotangazwa na NEC kwa sababu watakuwa wameiba kura kimacho macho na kuzima tafurani hiyo ni kulitumia JWTZ na vitisho vyake.

9) Bosi wa NEC kutamka hapa Arusha ya kuwa hata kama mawakala hawatatia sahihi zao bado fomu hizo hazina walakini. Swali la kujiuliza ni kuwa kama mawakala wana madukuduku na jinsi uchaguzi ulivyofanyika ni wapi wataanza kuzionyesha dukuduku hizo. Kauli hii ya NEC imetafsiriwa kuwa ni njama na kebehi za kupuuza malalamiko ya mawakala juu ya wizi wa kura.
 
tUNAAMINI CHADEMA WANAO WATAALAMU KILA IDara tunaomba kitengo cha sheria chini ya gwiji Marando na wengine wafanye faster kukusanya data juu ya tuhuma hii ili ha NEC wajiuzulu mara moja kwa kashfa hii nzito.Mzee makame simuamini kabisa na macho yake ya paka yale.Nashaangaa watanzania atawabebea mbeleko gani??
 
hahaaa sasa huyu Rais si ndo anakubalika vibaya sana ya nini kuiba kura.....mijitu mizima ovyo sana
 
Habari zilizozagaa kwenye tovuti mbalimbali ya kuwa TRA wamekamata shehena ya mfanya biashara maarufu wa kampuni ya AZAM Bw. Said Bakhresa, kuwa lori lake lilisheheni karatasi za wapigakura ya URAISI ambazo tayari zimekwisha kupigwa "NDIYO" kwenye picha ya Raisi anayetarajiwa kubwaga manyanga baada ya uchaguzi huu, Bw. JK zimeleta hisia kali miongoni mwa wapigakura kuwa hakuna namna CCM inaweza kufanya hujuma hii ya kuwadhulumu wapigakura bila ya kuwa imepata mwanya kutoka kwa NEC.

NEC hivi sasa ambayo wajumbe wake wote ni teule ya Jk hakuna mpigakura anayeiamini hata chembe kutokana na maamuzi yafuatayo ambayo imeyafanya:-

1) Kufuta haki ya wapigakura kuwa mita 200 kutoka kwenye vituo vyao vya kupiga kura. Hii inaashiria ya kuwa NEC wapo beneti na CCM katika kuhakikisha ya kuwa kura bandia zinapoingizwa kwenye vituo vya kupiga kura wapigakura hawatakuwepo kuzuia au kukamata ushahidi wa uovu huo.

2) Kuanzisha matumizi ya tekinolojia nyingi na ambazo ni rahisi kurubuniwa na mitambo ambayo si rasmi na hivyo kufanya uwepo uwezekano mkubwa wa kucheza na kuyachakachua matokeo halisi ya uchaguzi huu.

3) NEC kutowapigania wapigakura wa vyuo vikuu wapatao 60, 000 na kuanza kutupiana mpira na serikali ya CCM ikithibitisha zaidi wanajua wanachokifanya hapo. NEC wangeliweza kabisa kuahirisha uchaguzi kwa wiki moja ili wanafunzi hao wapate haki yao ya kupiga kura lakini kamwe NEC haitafnya hivyo kwa sababu lengo ni kupunguza kura za upinzani

4) NEC siyo mgeni katika kucheza rafu. Mwaka 1995, ilichelewesha vifaa vya kupiga kura Mkoa mzima wa Dar-Es-Salaam ili kuilinda CCM iliyokuwa inadondoshwa vibaya hapo. Kama wapo tayari kufanza hivyo siku hizo ni lipi la kuwazuia safari hii kucheza rafu tena za kisomi zaidi?

5) Hadi sasa NEC haijatoa tamko rasmi la kupinga au kukubali kuwa chaguzi hii tayari imeingiwa na dosari ya kura za JK kujaribu kuingizwa kinyemela huko Tunduma na mfanya biashara wa kiarabu Bw. Bakhresa na kampuni yake ya AZAM kuingiza kura haramu hizo. Hili linaongeza mashaka ya kuwa NEC ni sehemu ya mkakati huo ndiyo maana imekaa kimya.

6) NEC ndiyo waliochapisha kura hizo sasa inakuwaje JK na watu wake wajue NEMBO hizo kama siyo NEC hao hao waliovujisha NEMBO hizo? NEC walidai wameikodisha kampuni kutoka UK ili ifanye kazi ya kuchapisha kura kuondoa malalamiko kama yaliyojitokea sasa yawaje Afrika kusini wameweza kuziiba nembo hizo na kuzichapisha. KAMA UFEDHULI HUU NI WA KWELI BASI NEC inabidi iwajibike na kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapigakura na chaguzi ikaahairishwa na tukajipanga upya

7) Kutokana na ukimya wa NEC wa kuvuja kwa NEMBO zake za uchaguzi na wao kukaa kimya wapigakura wana kila sababu ya kuutilia mashaka uchaguzi huu kama utakuwa ni huru na wa haki. NEC walipaswa kutoa tamko kama ni la kukiri basi kutoa tenda nyingine ya kuzuia NEMBO zilizoibiwa kutumika tena katika uchaguzi huu....

8) Tamko la JWTZ la kuwatisha wapigakura kutoleta fujo baada ya matokeo kutangazwa liliashiria ya kuwa CCM yaelewa kuwa wapigakura hawataafiki matokeo yatayotangazwa na NEC kwa sababu watakuwa wameiba kura kimacho macho na kuzima tafurani hiyo ni kulitumia JWTZ na vitisho vyake.

Kijana ni tetesi lakini kuna maswali ya kuuliza

1. Hivi chama gani cha siasa ambacho hakijui/hakikujua kwa NEC ni ya CCM? maana liko wazi kabisa!
2. Je nini matarajio ya vyama hivi baada ya uchaguzi, mathalan akishinda SLAA na NEC ikatangaza mshindi ni JK, what they will do? sheria inasemaje? NEC akisema fulani mshindi is final isnt it?
3 Je ukiingia kwenye ushindani hali ukijua utashindwa tu, kwa sababu ya mambo kama haya ya NEC, dwa yake ni nini?

Athari
1. Kutoamini NEC ni kuendeleza hizi tetesi huoni kunapoteza muda wa campaign, kama vyama vya siasa in the last 5 yrs vingepigania angalau tume ya uchaguzi iwe huru, walifanya hivyo? kwa nini?
2. Hali tete nchini, tetesi hizi zinaweza kuvuruga amani, je inasaidia nini tukipigana nchi hii kisa tetesi

Haya yote washindani(vyama vilitakiwa kujiandaa mapema), bila hivyo vinakuwa subjected kwenye group la blind na wanaosubiri matokeo kwa bahati bahati tu.I am sorry huko kwenye kundi hilohilo. Tulipopiga kelele kuwa vijiandae mapema kwenye mabadiliko ya NEC na katiba wakasema( tena slaa alisema kabisa ni ngumu sana) aliposema hivyo tu ni-ka-conclude hatuna wapinzani nchini,SLAA is not the one, ikiwa mambo ya msingi hayafanywi kwanza basi wote ni walewale,nchi imeuzwa hii kwa uangalifu mkubwa mno.

pole sana hizi tetesi si tetesi, ni hali halisi maana wapinzani watayakubalimatokeo na watamkubatia JK kwa ushindi, tupo, jipe moyo baada ya uchaguzi you will surely confirm my words, HATUNA WAPINZANIA HAWA WOTE NI MAGARASHA TU

Cheers!!!
 
Ama kweli siku za mwizi ni arobaini. Hii inadhihirisha vita dhidi ya ya mafisadi ni vikali. Hivyo, ni lazima tuongeze mbinu za mapambano.
 
Na bado

Mwishowe tutaambiwa Kwenye vituo nya kupigia kura kuna waganga wametumwa na CCM from BWAGAMOYOOOOOOOOOO
 
Na bado

Mwishowe tutaambiwa Kwenye vituo nya kupigia kura kuna waganga wametumwa na CCM from BWAGAMOYOOOOOOOOOO
kwani hujui kuwa ccm wanawaloga watanzania kwa kutumia zawadi wanazowapa kama kanga t.shirts, scarf, kofia. vile vitu vimeshanuiziwa kuwafanya watanzania waendelee kuwa mazuzu. HERI YAO WALE AMBAO HAWATAKUBALI KUPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA CCM MAANA UKOMBOZI WA NCHI HII UTAKUWA MIKONONI MWAO. AMEEEN
 
Kijana ni tetesi lakini kuna maswali ya kuuliza

1. Hivi chama gani cha siasa ambacho hakijui/hakikujua kwa NEC ni ya CCM? maana liko wazi kabisa!
2. Je nini matarajio ya vyama hivi baada ya uchaguzi, mathalan akishinda SLAA na NEC ikatangaza mshindi ni JK, what they will do? sheria inasemaje? NEC akisema fulani mshindi is final isnt it?
3 Je ukiingia kwenye ushindani hali ukijua utashindwa tu, kwa sababu ya mambo kama haya ya NEC, dwa yake ni nini?

Athari
1. Kutoamini NEC ni kuendeleza hizi tetesi huoni kunapoteza muda wa campaign, kama vyama vya siasa in the last 5 yrs vingepigania angalau tume ya uchaguzi iwe huru, walifanya hivyo? kwa nini?
2. Hali tete nchini, tetesi hizi zinaweza kuvuruga amani, je inasaidia nini tukipigana nchi hii kisa tetesi

Haya yote washindani(vyama vilitakiwa kujiandaa mapema), bila hivyo vinakuwa subjected kwenye group la blind na wanaosubiri matokeo kwa bahati bahati tu.I am sorry huko kwenye kundi hilohilo. Tulipopiga kelele kuwa vijiandae mapema kwenye mabadiliko ya NEC na katiba wakasema( tena slaa alisema kabisa ni ngumu sana) aliposema hivyo tu ni-ka-conclude hatuna wapinzani nchini,SLAA is not the one, ikiwa mambo ya msingi hayafanywi kwanza basi wote ni walewale,nchi imeuzwa hii kwa uangalifu mkubwa mno.

pole sana hizi tetesi si tetesi, ni hali halisi maana wapinzani watayakubalimatokeo na watamkubatia JK kwa ushindi, tupo, jipe moyo baada ya uchaguzi you will surely confirm my words, HATUNA WAPINZANIA HAWA WOTE NI MAGARASHA TU

Cheers!!!

Tetesi ni mwanzo wa utafiti, hivyo ni kitu kizuri kabisa kwa maisha ya binadamu. Sasa tetesi hii italeta utafiti na matokeo yake tutayaona kama ni kweli au si kweli!
 
Tanzania ingekuwa ni nchi angalau inayoendelea, Tume ya Uchaguzi ingejiuzuru mara moja na huyo Gabachori aliyetumiwa kuingiza kura feki angekumbatana na nguvu ya umma ambayo ingemfanya ajiue! BUT, Alas! Watz wangapi waliopata taarifa hizi na kuzitafakari na kuelewa kwa kina njama kubwa na mbaya ya KUBAKA demokrasia nchini kwetu? KIKWETE is now placed between the devil and the deep sea! Utashinda lakini huna baraka za Mungu za kutawala!
 
Back
Top Bottom