Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania

" A peacock who sits on his tail is just another turkey"

Tunauwezo wa kugomea ongezeko la bei .Mfano tukiamua kuzima simu zetu zote kwa siku mbili tu wataimba wimbo waupendao. We have nothing to loose.........
Hii imetulia,ila tutawasiliana vipi?
 
" A peacock who sits on his tail is just another turkey"

Tatizo ni sisi wenyewe pia. Tunakubali kila uchafu. Hamna kupinga . Wenzetu wanagomea bei na wanafaulu. Tunauwezo wa kugomea ongezeko la bei .Mfano tukiamua kuzima simu zetu zote kwa siku mbili tu wataimba wimbo waupendao. We have nothing to loose.........


What a brilliant idea !! Sasa next step ndiyo kazi. Hebu tuunguze brain tuone hili wazo linaweza kutekelezwa vipi. Je vyombo vya habari vinaweza kuunga mkono jambo hili maana its impact will be felt all over will need some sacrifice beyond consumers alone.
 
[/size]

What a brilliant idea !! Sasa next step ndiyo kazi. Hebu tuunguze brain tuone hili wazo linaweza kutekelezwa vipi. Je vyombo vya habari vinaweza kuunga mkono jambo hili maana its impact will be felt all over will need some sacrifice beyond consumers alone.

Vyombo vya habari haviwezi kuandika kwasababu hawa watu (VodaCom, Celtel, Tigo etc...) ndio wateja wao wakubwa katika biashara zao.
 
Haya makampuni yana pata faida kubwa sana nchini halafu sijui hizo pesa wanalipa hata kodi ya kutosha. Ni wanyonyaji vibaya sana na kwa vile hakuna regulatory body nchini.

Ukiangaliwa consumers hawajui wanalipa kiasi gani kwa dakika ya mazungumzo....Naamini kama mtu ukijaribu uka time dk unazoongea na malipo yake uatjuwa ni wazi kabisa ni rip off
 
Bei ya kupiga simu duniani inazidi kutelemka. Mwaka 1998 nilikuwa napiga simu Tanzania kutoka Marekani kwa $1.07 kwa dakika, leo hii napiga simu kwa kati ya $0.03 hadi $0.10 kwa dakika. Bei inapungua kila kukicha, ndiyo maana makampuni ya simu yanaongeza huduma nyingine kama GPS, TV, internet na e-mail kwenye huduma zao. Tanzania kulikoni serikali kupandisha huduma hiyo?

Ni kama vile tuko kwenye one way lakini sisi tunalekea upande usioruhusiwa; kwa hiyo tunaelekea ambako wenzentu wanakotoka.
 
By the way. Hivi kwanini meseji nazopata kutoka tanzania zinakuwa alpha-numeric? Kwa wiki moja unusu sasa. Seems very dodgy.
 
Tumekwisha! itabidi tutumie simu za wenzetu ie. celtel Kenya au Safaricom
 
Ukweli ni kwamba uchumi wetu ni mbovu kuliko kabla ya uhuru, mwingereza alianzisha mashamba ya katani, chai, pamba na kahawa na kuliingizia koloni lao mapato makubwa.

Leo tumeanzisha miradi mikubwa ya simu za mkononi, daladala za hiace na pikipiki toka china, tumewakopesha mamalishe mabilioni tele na kukaribisha wawekezaji katika uzalishaji wa soda, bia na maji yachupa.

Tunajivunia kuwatembeza viongozi toka ulaya katika mawodi ya wagonjwa wa ukimwi na kambi za watoto yatima, tunawachangisha fedha za kununulia vyandarua na arv. wakiondoka hawarudi tena, nadhani hujutia safari zao ndo maana hawarudi.

Hivi utajisikiaje ukimtembelea rafiki yako akaanza kukwambia umsaidia pesa ya kitoweo kwani hana uwezo wa kukulisha!
 
Kwa taarifa yenu tu,Bei mpya zilishaanza kutumika bila nyie kuambiwa,utaona jinsi hizi kampuni zinapotoa kiburi..
 
Twafa, nadhani tufikirie la kufanya haraka ili kuhakikisha tunalinda maslahi yetu ambayo viongozi wetu wameshindwa kuyalinda. Hapendekeza, hata kama tukishindwa kuzima simu kama ilivyopendekezwa hapo juu, tunaweza kuamua kususa kutumia baadhi ya mitandao na kustick kwenye mtandao mmoja tu kwa sababu ni lazima tuwasiliane. Wale tutakaowasusia watalazimika ikushusha bei ili kutushawishi twende kwao. Tuwadengulie mpaka watupigie magotina hapo tutakuwa na nafasi ya kuingiza masharti yetu na sisi kama wateja.
 
Ungedhani kwamba kasi ya kupanda kwa bei inapowazidi nguvu wananchi, basi serikali yao ingewapa ahueni kwa kuwapunguzia kodi. Hilo lingewezekana kama serikali ingetoza kodi makampuni yanayokwepa (kwa kubadilisha majina), etc.

Gembe is right: serikali imeshindwa kuyatoza kodi makampuni ya madini, na badala yake inarudi kwa wanyonge wake, yaani wananchi, na bila huruma inawabandika kodi ya kulipizia inflation. Utadhani ni wananchi ndio wamewapa hiyo inflation!

Kibaya zaidi ni kwamba fedha hizo za kodi zitaliwa, karibu zote, na viongozi wa serikali. Baadhi watanunulia magari ya bei mbaya, nyingine ni per diem zao wanapokwenda kufanya kazi zao za kawaida mikoani, na zinazobaki wataziiba directly, kwa kupitia benki kuu na taasisi nyingine walizounda kwa ajili hiyo.

Nyie mlie tu! Si mmewachagua wenyewe!
 
Mimi nimeshapata akili kuhusu hili, pesa za kampeni zitapatikana wapi kama ninyi mumeanza kubana sources zao kama walivyokuwa wanachota pale BOT? Hapa naona wazi kodi nyingi hazitateremshwa wala sehemu mingi za kukusanyia kodi hazitalegezwa maana pesa ya uchaguzi ujao itapatikana kupitia hivi vyanzo vipya. Kulingana na akili yangu mtindi, hizi ni sources mpya za mapato dhalimu ya serikali yetu ya kifedhuli. Tunawakusanyia bila kujua kinachoendelea maana vichwa vinawauma kuhusu wapate wapi pesa za uchaguzi ujao.
 
Kumbe mchawi wa gharama za simu ni serikali. waziri mhusika amekiri Bungeni jana kuwa kiwango kikubwa cha kodi ndicho kinachosababisha gharama za airtime kuwa kubwa nchini. Katika hilo alibainisha kuwa Tanzania ni nchi ya opili duniani kwa kuwa na gharama kubwa za kodi ya simu (at 30 percent). amesema kuwa wlaa haakuna misamaha ya kodi kwa makampuni ya simu
 
Kumbe mchawi wa gharama za simu ni serikali. waziri mhusika amekiri Bungeni jana kuwa kiwango kikubwa cha kodi ndicho kinachosababisha gharama za airtime kuwa kubwa nchini. Katika hilo alibainisha kuwa Tanzania ni nchi ya opili duniani kwa kuwa na gharama kubwa za kodi ya simu (at 30 percent). amesema kuwa wlaa haakuna misamaha ya kodi kwa makampuni ya simu
Tatizo ni watu wa wizara ya Fedha coz wao ndiyo walipendekeza kodi hii.Mbaya zaidi kampuni zinalipa asilimia 7 tu kati ya 30 na zingine 23 zinalipwa na MWananchi...

Walishatuona siye mandondocha.Bei zilishaanza kutumika nadhani toka tarehe moja kutokana na barua ambayo niliiona kwenda kwa kampuni za simu..kwa walio Tz kwa sasa mnaweza kutuambia,ila najua ...
 
Ni kwa mujibu wa Tanzania Daima la leo, pg 3




Viwango vya muda wa maongezi nchini viko juu




na Salehe Mohamed



TANZANIA ni nchi ya pili duniani kwa kutoza viwango vikubwa vya kodi katika muda wa maongezi (air time), katika sekta ya mawasiliano nchini.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alibainisha hayo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi (Chadema ), aliyehoji kuhusiana na misamaha ya kodi.

Msolla alisemaTanzania inatoza kodi kwa asilimia 30 nyuma ya Uturuki inayotoza asilimia 45, hali ambayo ni kikwazo kwa sekta ya mawasiliano.

Alisema viwango vya kodi vinavyotozwa hivi sasa, vilipata baraka ya Bunge lakini vinaweza kupungua pindi mkongo wa taifa wa mawasiliano utakapokamilika.

Aidha, Arfi aliitaka serikali kupunguza kodi ili huduma za gharama za simu ziweze kupungua na kuwanufaisha Watanzania wengi.

Msolla alisema serikali inatoa misamaha kwa kampuni hizo kwa ajili ya vifaa vyao lakini si kuwasamehe kodi kutokana na biashara wanayoifanya.

“Wanachokipata hivi sasa ni msahama wa vifaa wanavyotumia wakati wa ujenzi na si kwenye biashara wanayoifanya,” alisema Msolla.

Kuhusu ubadilishaji wa jina la Kampuni ya simu ya Celtel kuwa Zain, alisema, hatua hiyo haijaathiri mapato ya nchi kutokana na kuwa mfumo wa ubia uliopo na kuongeza kuwa serikali inaendelea kumiliki hisa za asilimia 35, huku Celtel ikimiliki asilimia 65.

Alitanabaisha kuwa hakuna ukweli wowote kuwa ubadilishaji huo unalenga kukwepa kodi za serikali bali ni namna ya kuufanya mtandao huo utumike zaidi, kwani Zain inatumiwa na nchi zisizopungua 22.

“Nasisitiza tena kuwa kubadili jina huko hakuifanyi nchi kukosa mapato bali ni mbinu yao ya kuboresha huduma zao na kuwaunganisha na watu wengine, Watanzania tuondoe hofu,” alisema Msolla.

Katika hatua nyingine, Bunge limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambayo ni sh bilioni 42.8.
 
Wabunge walia ushuru wa simu za mikononi
Cassian Malima, Dodoma
Daily News; Thursday,August 28, 2008 @00:01


Wabunge wameishauri serikali kufuta pendekezo lake la kuongeza ushuru kwenye huduma ya simu za mikononi kutoka asilimia saba sasa hadi asilimia 10. Wakichangia Muswada wa Sheria ya Fedha na Kodi mbalimbali uliowasilishwa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, wabunge walisema ongezeko hilo halistahili kwa sasa kwa sababu simu za mikononi si anasa tena kama ilivyokuwa ikifikiriwa awali.

Aliyeanza kueleza pingamizi lake alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Dk. Abdallah Kigoda ambaye alisema suala hilo linahitaji kuangaliwa kwa makini ili huduma za simu za mikononi zizidi kuenezwa, hasa katika maeneo ya vijijini.

Dk. Kigoda alifuatiwa na Fatma Fereji (Viti Maalumu -CUF), ambaye wakati akitoa maoni kwa niaba ya upande wa upinzani, alisema iwapo ushuru utaongezwa, unaweza kuwa na athari kubwa kwa kusababisha kupungua kwa wateja na kiwango cha kodi ambacho kinalipwa na kampuni za simu kwa serikali.

Katika muswada huo, Waziri Mkulo alitangaza hatua nyingine kadhaa zinazochukuliwa na serikali kuwa ni pamoja na kupandisha ushuru wa vinywaji baridi, bia, mvinyo, vinywaji vikali na sigara.

Serikali pia imependekeza kwenye muswada huo kupunguzwa kwa ushuru wa mafuta mazito ya kuendesha mitambo; kushusha kiwango cha ukubwa wa injini za magari kinachotumika kwa ajili ya utozaji ushuru kutoka cc 2,000 hadi cc 1,500, kupandisha kodi ya usajili wa magari kutoka Sh 90,000 hadi 120,000 na Sh 35,000 kwa pikipiki.

Serikali pia imependekeza kwamba Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF) uanze kushughulikia wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Usalama wa Taifa. Serikali imeahidi kupeleka fedha za usajili na pensheni kwa wastaafu hao kila baada ya mwezi mmoja au mitatu.

Wakati wa kuchangia muswada huo kabla Bunge halijaahirishwa jana mchana, wabunge Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini - CCM) na Job Ndugai (Kongwa - CCM), walieleza wasiwasi kuhusu pendekezo la kumpa madaraka Waziri wa Fedha na Uchumi kuchukua kiasi cha fedha anachoona kinafaa kutoka katika mashirika fulani ya umma na kukiweka kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa wabunge hao, jambo hilo linabidi lifanywe kwa busara na umakini na kuhakikisha kwamba mashirika hayo yanaachiwa fedha za kutosha. Baadhi ya mashirika yanayotajwa kwenye muswada huo ni Mamlaka ya Masoko ya Hisa na Mitaji (CMSA), Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura), Shirika la Michezo ya Bahati Nasibu, Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Mamlaka ya Usalama wa Anga (TAAA), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi
 
Wadau hii imeakeje?
Kila mara kampuni za simu zinapo anzisha promosheni au kubadilisha namna ya kuchaji (Billing plan) wanasema wameanzisha huduma mpya. Mfano hebu angalia hii hapa chini
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain, imezindua huduma mpya ijulikanayo ‘JIRUSHE’ itakayomwezesha mteja kuongea bure siku nzima.

Katika huduma hiyo, mteja atatakiwa kulipia gharama ya shilingi 1,500 hivyo kumwezesha kuingia katika huduma hiyo moja kwa moja kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno JIRUSHE.

Je ni sawa kutumia neno huduma hapa? Mimi ninavyojua hapo hakuna huduma mpya maana huduma ni ile ile ya mawasiliano kwa sauti.

Ninaandika hivi kwa sababu kila mara nikiona kwenye Gazeti sijui kampuni flani yaanzisha huduma mpya, nakimbilia kusoma kujua ni huduma gani mpya tunaletewa nakuta ni billing plan tu. Ni kiswahili kinagomba au ni maneno ya kibiashara tu
 
Heshima Mbele,

Kuna jambo moja ambalo limekuwa likinikera sana hasa pindi napokuwa hapa Nyumbani,kupata Zile SMS ambazo zinakulazimisha wewe kutuma neno flani ali wewe upate huduma Flani.kwa mfano unataka kichekesho,au kupata habari za mpira,kushiriki kitu flani

Kwa kifupi hizi kampuni zimekuwa zikifanya wananchi ni mtaji wao,ukaichilia mbali gharama kubwa wanazowatoza wana wa watanzania masikini ambao wameshindwa kutumia vizuri fursa zao.Kwa taarifa yako tu kila unapopata Message kutoa kwa kampuni hizi basi jua wamekata kiasi flani cha pesa bila wewe kujua.

na siku zote hawako tayari kutoa namba ya kujitoa katika huduma hizo.wanavuna pesa nyingi kila siku toka kwa wananchi.Jenga tabia ya kauangalia salio lako kila upatapo ujumbe utaona wamekata pesa ya SMS.

Hii ni kampeni ili kampuni zitangaze njia ya kujitoa katika huduma hizo.Natoa masaa 48 kama siyo hivyo nitaenda mahakamani kuwashtaki sababu sheria zipo
 
Back
Top Bottom