Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania

Special Request for Mwankijiji and you all and now you will know who own all of these Companies

ABOUT TIGO
MIC Tanzania Limited (tiGO) was found on November 30, 1993. This incorporation was a joint venture between Millicom International Cellular based in Luxembourg, Ultimate Communications Limited of Tanzania and Tanzania Posts and Telecommunications Corporation. In this venture 27.7% of the issued share capital were alloted to the Ultimate Communications Limited and Tanzania Posts and Telecommunications Corporation[4].

In 1993, there was liberalization of telecommunication sector in the country which result into dissolution of Tanzania Posts and Telecommunications Corporation (TPTC) in early 1994. Its shares ware then transferred to Tanzania Telecommunications Company Limited. Further steps towards full liberalization of the market causes the privatization of TTCL in February 23, 2001 and its shares were transferred to the Tanzanian Government

About Vodacom
Vodacom Tanzania was licensed in Tanzania with its local partners Planetel Communications holding 36 % and Caspian Construction holding 16%. Later Planetel decreased its stake to 16%, while Caspian’s increased to 19%[7].

A representative of Caspian on the Vodacom Tanzania board is businessman-politician Rostam Aziz, a close supporter of President Jakaya Kikwete. At the time Vodacom was licensed in Tanzania, neither man was quite as powerful as now.Kikwete was Foreign Minister and Aziz had yet to occupy any formal position in Tanzanian politics.

While spreading its political bets, the CCM's and the former Speaker of Parliament Pius Msekwa was granted Vodacom Tanzania’s non-executive chair between 2003 and 2005. When Vodacom Tanzania hosted a “VIP gala night” to bid farewell to outgoing president Mkapa in December 2005, Msekwa attended, presumably in both capacities.

About Celtel
Yenyewe ilianzia pale TTCL

conecting to the dot....
 
Project ya Cable ya TZ labda itapunguza bei. Huku USA $50 unapata dakika 500 au 600, usiku kuanzia saa tatu free,week-end free, na kama unapiga kwa mtu wa kampuni moja free. Tanzania mnaliwa ndugu zangu
 
Kazi ipo.......haki ya nani vile wakati ulimwenguni kwingine amwasiliano yanakwenda chini hawa wanapandisha......tutaweka simu chini tutainua.....juu.....
 
Uuuwi!!!!!!!!!!!!! Tanzania tunarudi hapa
fire_mkr.jpg

na hapa

CaveMan.jpg

BTW: Nimeshindwa ku-embedd Youtube viedo hapa; je kuna anayejua namna ya kufanya hivyo?
 
Uko tuendako kila kitu kina lengo la kumnyonya mtanzania wa kawaida,comparatively speaking sisi tuko juu kwa gharama za simu bado wanaendelea kutuumiza.
Ivi uyu mtanzania atatetewa na nani kama vyote ivi vyafanyika ingali wawakilishi wetu wanaangalia jamani.
Ifike wakati nasi tuwe twagoma tuu,mwisho wa siku watatia akili
 
Hilo darasa hapo juu ni MUHIMU SANA!

Someni..Chukueni time mtafakari kwani ndani yake kuna namna pia ya kupambana na hali hiyo ambayo hata sisi tunayo kwani ndio hayo hayo ya wabunge kuwa wanahisa wa makampuni nk.

Na hivyo kusimamia maslahi ya makampuni badala a wananchi.

Na kwahiyo ni lazima tubadili utaratibu ili malobyst wawe ni wa wananchi.

Kama ilivyoainishwa na quote hiyo hapo chini...Basi tunaomba hayo maswala yazingatiwe ili tupate lobbysts wa wananchi kama ilivyo ainishwa hapo chini....

To be clear, not all lobbyists represent big business, not all of them are Abramoff-style operator and not all of them toe the line between legality and criminal corruption. In fact, most lobbyists are respectable folks legitimately conveying the interests of organized groups to those whose actions and votes have an effect on the way we live in America. They may represent churches, universities, charities, senior citizens groups or environmental concerns, or they may represent Enron or the Northern Mariana Islands. Basically, a lobbyist's job is to persuade lawmakers to view an issue in their clients' interest and will urge them to vote in a way that benefits their clients, whether that means more federal research contracts for a college in a congressman's district, more affordable drug prescriptions for the elderly or bigger tax loopholes for corporations.

Masalahi ya wananchi yaweza kuwakilishwa kama ideas kwa namna nyingi...Si lazima tuwe na mfumo kabisa wa aina hiyo lakini ni muhimu tuwe na mwelekeo huo ili kuwaondolea mbali kina RA na kina Siclair ambao wameshawanunuwa wabunge wengi tu na viongozi wetu wakuu wa serikali.

Na yote hayo yatawezekana kama wabunge wakitowa ripoti za maslahi yao kwenye makampuni hayo ili tujuwe kama ni manufaa ya wananchi kwa kivipi!
Na kwahiyo basi..Sisi wananchi tunataka kujuwa ni lobyst gani aliyeileta hio mada ya ongezeko la kodi hiyo!
Na pia kama ana maslahi na kampuni hiyo then kuna conflict of interests na hivyo ni wazi kuna UFISADI HAPO!
 
Maisha Bora yanakuja na Bei za Mabasi nazo kwenda juu..do wwe accept this?
 
Nawasihi tuangalie pia madhara yanayosababishwa na simu hizi hasa za mikononi ikiwemo maambukizi ya nguvu na ya haraka ya UKIMWI kutokana na mawasiliano kuwa rahisi; watoto wetu wameharibika mno kutokana na mawasiliano haya; watu hawanunui machungwa badala yake wanaweka "dola" kwenye simu; matumizi mengi ya simu hizi kwa Mtanzania wa kawaida hayana tija bali kumfukarisha zaidi. Kwa kweli matumizi ya simu za mkononi umegeuka kuwa ULEVI fulani hivi au KAMARI ambayo inaishia kuwatajirisha wachache. Teknolojia hii imetuvamia na imetutesa kwelikweli.
 
Maisha Bora yanakuja na Bei za Mabasi nazo kwenda juu..do wwe accept this?

Sio mabasi tu everything is up from 1st July, Nyama buchani ni 3800 mpaka 4200 kwa kilo, bei ya mafuta petrol ni 1810 mpaka 1850 kwa lita Diesel 2000 mpaka 2015 kwa lita, then tunaongelea maisha bora kwa kila mtanzania, hivi hii 100,000 waliyompa mfanyakazi wa serikali inatosha nini, maana bei ya maharage ni sawa na nyama sasa.

Dagaa usiseme kilo sh. 12000 kwa dagaa la kigoma na la mwanza sh.4000 sasa watu wa kipato cha chini wanaishi maisha ya aina gani kama sio mwaisha bora kwa wateule wakati watu wa kawaida wanakufa na njaa.
 
duh..itabidi nimuongozee maama watoto bajeti yake..sikujua kama imefikia huko katika chakula.

huko Uingereza watu wameanza kuandamana..hapa kwetu je?Hivi ni kweli siye ni matajiri kiasi hiki?Kama Serikali inaweza kulipa pesa 152million kwa ajili ya Umeme wa dharula,Je kwetu inakuwaje katika hili?
 
Sio mabasi tu everything is up from 1st July, Nyama buchani ni 3800 mpaka 4200 kwa kilo, bei ya mafuta petrol ni 1810 mpaka 1850 kwa lita Diesel 2000 mpaka 2015 kwa lita, then tunaongelea maisha bora kwa kila mtanzania, hivi hii 100,000 waliyompa mfanyakazi wa serikali inatosha nini, maana bei ya maharage ni sawa na nyama sasa.

Dagaa usiseme kilo sh. 12000 kwa dagaa la kigoma na la mwanza sh.4000 sasa watu wa kipato cha chini wanaishi maisha ya aina gani kama sio mwaisha bora kwa wateule wakati watu wa kawaida wanakufa na njaa.

Huu mfumo wa serikali wa kodi ni wa kutupiwa macho.
Kama kweli wana nia nzuri...Then ni kwanini Diesel ni ghali kuliko petrol?
Ama kwasababu wanajuwa kuwa inatumika kwenye mashangingi yao pamoja na vyombo vya usfiri kwa ujumla?
Kwa uelewa wangu...Petrol ni lazima iwe ghali kuliko diesel kwani diesel ni level ya chini.
Hapo kuna utata unless kama kuna mtu ana maelezo ili tuelimishane kwenye hili.
 
Na Jabir Idrissa
Gazeti la Mwanahalisi

UONGOZI wa kampuni ya Celtel International jijini Dar es Salaam, umeshindwa kujibu tuhuma zinazoukabili kuhusu kutumia mali za TTCL kujiimarisha.

Wiki iliyopita gazeti hili lilinukuu baadhi ya vyanzo vilivyosema Celtel International inatumia mitambo ya TTCL iliyotapakaa nchini kuimarisha biashara yake ambayo haina mafao kwa TTCL.

Celtel International iliundwa kutokana na Celtel Tanzania ambayo nayo ilitokana na mtaji uliopatikana kwenye biashara ya makampuni ya MSI/Detecon yaliyokuwa na ubia na TTCL.

MSI/Detecon ambao walipaswa kuimarisha TTCL kwa kulipa dola 120 milioni kama malipo ya hisa 35 katika kampuni hiyo, wanadaiwa kulipa nusu ya malipo hayo hadi walipoondoka nchini mwaka 2005.

Ni MSI/Detecon waliounda Celtel Tanzania na baadaye Celtel International ambayo imekuwa ikitumia mitambo na mali nyingine za TTCL kwa kujiimarisha hadi kuwa katika nchi za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Maghgaribi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Uhusiano wa Celtel International kwa mwandishi wa gazeti hili inaeleza matukio ya mwaka 2005 ambayo hayana uhusiano na hali halisi ya sasa inayolalamikiwa.

Katika mawasiliano yake Alhamisi, 10 Julai 2008, kwa njia ya baruapepe, ofisa huyo Georgia Mutagahywa amewasilisha andishi “ TTCL and Celtel Separated” (Makampuni yatenganishwa) ambalo halisemi lolote juu ya hali ya sasa.

Hata hivyo, taarifa ya Mutagahywa imethibitisha kuwa Celtel International inatokana na Celtel Tanzania ambayo ilikuwa kampuni tanzu ya TTCL.

Aidha, imefahamika kuwa hata Celtel International imeishanunuliwa na kampuni ya MTC ya nchini Kuwait inayoendesha makampuni matano makubwa ya simu za mkononi eneo la Mashariki ya Kati.

“Unaona sasa, mitambo ya TTCL ambayo ilianza kutumiwa na MSI/Detecon na kuzaa Celtel, ndiyo imezaa Celtel International na sasa in aendelea kuhimili mtandao mkubwa hadi nchi za Arabuni,” amelalamika mmoja wa wafanyakazi wa TTCL ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.

Waraka wa Mutagahywa haujibu hoja Celtel kuwa kampuni tanzu; kutumika kwa fedha za TTCL kuanzisha Celtel; matumizi ya mitambo ya TTCL kusambaza mtandao na kudhoofisha na hata kuua miradi ya TTCL iliyokuwa muhimu kwa nchi zote za Kusini mwa Afrika.

Aidha, imefahamika kuwa maofisa waandamizi nchini walioshiriki kubinafsisha TTCL kwa mwekezaji mgeni, ndio wanaounda Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia menejimenti ya kampuni hiyo kwa sasa.

Imefahamika pia kuwa maofisa waliofanikisha utaratibu wa kuiingiza TTCL katika menejimenti ya wabia wa kigeni baada ya MSI/Detecon, ndio sasa sehemu ya menejimenti ya TTCL.

Mmoja wa maofisa hao ni George Mbowe, mfanyabiashara wa siku nyingi nchini ambaye sasa ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL.

Wakati mchakato wa kubinafsisha TTCL unaanza na ulipokamilika, Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kurekebisha na Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC).

Awali Mbowe alikuwa mjumbe wa Bodi ya lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania (TP&TC) ambalo baada ya kugawanywa, ndipo ilizaliwa TTCL na Shirika la Posta (TPC).

Wajumbe wengine wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL kama walinzi wa hisa 65 za serikali, inayoongozwa na Profesa Mathew Luhanga, ni Agnes Bukuku na Iddi Suwedi.

Upande wa Celtel International, mkurugenzi wao katika bodi hiyo, ni Jaji Joseph Warioba wakati Gilder Kibola ni Katibu wa Kampuni ya TTCL.

Profesa Luhanga ambaye aliwahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2006, kwa muda mrefu sasa amekuwa Afrika Kusini.

Kulingana na taarifa ya menejimenti ya TTCL ya mwaka 2006 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Celtel International inatambulishwa kama mbia wa TTCL.

Vyanzo vya habari vimesema kwamba Celtel ilianzishwa katika mazingira tata kwa kuwa wakati MSI/Detecon wanaingia TTCL, kulishasajiliwa kampuni ya Celnet iliyokusudiwa kutoa huduma ya simu za mkononi.

Mpaka sasa haijulikani mradi huo pamoja na mingine kadhaa iliyokuwa ndani ya mipango ya maendeleo ya TTCL, ilivyofutwa.

Uendeshaji TTCL ulioacha maswali mengi, ulisukuma baadhi ya wataalamu wa kampuni hiyo waliosomeshwa na TTCL hadi kufikia shahada ya falsafa (PhD) kuacha kazi kwa kukerwa na mazingira mabaya ya uendeshaji kampuni.

Matatizo yalioko TTCL hadi sasa yalisababisha chama cha wafanyakazi wa mawasiliano (TEWUTA) Mkoa wa Dar es Salaam kupeleka malalamiko kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006.

Moja ya mapendekezo ya msingi waliyotoa ni kuondolewa kwa uongozi wote uliopo TTCL ili kampuni irudi kwenye mstari.
 
Umaskini wetu unasababishwa zaidi na ujinga wetu sisi wenyewe. Wakati tunapata uhuru wetu mwaka 1961 kiwango chetu cha maendeleo kilikuwa sawa na nchi za Singapore, Malaysia na zaidi ya Vietnam ambayo baadaye iliunguzwa na mabomu ya Marekani kwa karibu miaka kumi, lakini leo hii nchi hizo ziko mbele yetu kwa mbali sana pamoja na kuwa hazina raslimali kama tulizo nazo sisi; sababu? Ujinga wetu.

Ingawa tuna ujinga wa aina nyingi, kinachotuanguasha sisi ni ujinga huu wa kutokuwa na sera nzuri za kuhamasisha maendeleo yetu. Katika dunia ya leo hii ya information, tunatakiwa tuimarishe sana njia za mawasiliano na habari, na vile vile tuzifanye ziwe rahisi sana kufikiwa na raia wetu. Vitu kama barabara kuu na ndogo, njia za reli, internet access, wireless communication (cellphone), matangazo ya television na radio, pamoja na magazeti ni vitu vinavyotakiwa viwe accessible kirahisi kwa raia wetu ili wawe connected na hivyo wasiachwe nyuma katika dunia hii inayokimbia haraka sana. Serikali yetu kwa upande wake imeshindwa kuimarisha njia hizi kwa mfano barabara na reli, ila sekta binafsi imejitahidi sana kutimiza wajibu wake kwa kuimarisha television, radio, magazeti, cellphone na kwa kiasi fulani internet. Serikali ilitakiwa iwe na sera zinazotoa incentive zaidi ili huduma hizi ziendelee kuboreka zaidi.

Nchi nyingi nilizowahi kuishi hapa duniani hutoza kodi kubwa kwa zile bidhaa na huduma zionekanazo kuwa siyo za muhimu, na hutoza kodi ndogo sana kwa bidhaa na huduma ambazo ni za muhimu sana kwa survival ya raia wake; ndiyo maana chakula, na madawa hayalipiwi kodi kabisa wakati sigara zinatozwa kodi kubwa sana. Serikali yetu inapoamua kupandisha kodi ya simu za mkono, ina maana wameona kuwa huduma hiyo ya simu siyo ya muhimu kwa raia wetu; Mungu wangu. je huu siyo ujinga jamani?

Leo nilikuwa naangalia bei ya dhahabu ni $970.70 kwa aunzi ( gramu 28), ina maana kuwa $34,240 kwa kilo moja ya dhahabu, au TShs 39,000,000 kwa kilo. Je ni dhahabu kilo ngapi zinaondoka nchini kila siku? kwa nini serikali isijipatie mapato yake kutokana na dhahabu hizo? Kwani lengo la kuwaleta hawa wawekezaji lilikuwa nini?

Hapo ndipo unapoona ujinga wetu; hata serikali yetu pia ina sera za kijinga kama kawa.
 
...believe me,kama bei itaongezeka 240Tshs kwa kila 1000Tshs utakayotumia,matumizi ya simu yatashuka kwa kiasi kikubwa sana na wengine wataacha kabisa,nimeona americans wakijidai mafuta hayawezi kubadilisha tabia zao za kuendesha magari lakini sasa mabasi vituoni ukichelewa hata nafasi hupati na hybrid cars kupata sasa hivi unasubiri line zaidi ya miezi sita,subiri uone hiyo tax itakavyofanya then tuje tuongee hapa baada ya miezi sita!

Matumizi ya simu yanaweza kushuka kwa wasio na uwezo lakini si kwa mafisadi serikalini na kwenye mashirika ambako hayo matumizi pengine yanalipiwa na serikali/shirika. Viongozi wetu hawana uchungu wowote na sisi walalahoi.
 
Unafikiri ni kwanini Viongozi wetu hawan uchungu wowote wa maisha tunayoishi?

Je bila sisi wanaweza endela kuwapo hapo walipo,na kama ndiyo ni sisi kwanini tusiwatoe kwa njia rahisi
 
Leo nilikuwa naangalia bei ya dhahabu ni $970.70 kwa aunzi ( gramu 28), ina maana kuwa $34,240 kwa kilo moja ya dhahabu, au TShs 39,000,000 kwa kilo. Je ni dhahabu kilo ngapi zinaondoka nchini kila siku? kwa nini serikali isijipatie mapato yake kutokana na dhahabu hizo? Kwani lengo la kuwaleta hawa wawekezaji lilikuwa nini?

Hapo ndipo unapoona ujinga wetu; hata serikali yetu pia ina sera za kijinga kama kawa.
Mkuu kichuguu,

Kwani walioanza kuchimba Dhahabu ni kampuni gani>?TANGOLD ambao walikuwa wakimiliki Mgodi wa Geita Gold Minning..Je unamfahamu mwenye Share katika Kampuni hiyo..ambaye anapenda sana kumwalika Mkuu wetu kila akikutana naye
 
Mkuu Gembe,

Inamaana mzee "Kichaka" ana share zake TANGOLD?! Basi tumekwisha! Nasikia ana share hata kwenye makampuni ya mafuta duniani. Tz.Coltex na Chivurone ni moja ya hizo kampuni. Usije ukashangaa ukisikia kwamba anampango wa kuchimba mafuta tz.
 
Kichaka wenyewe hawezi kumiliki bila ya watu nyuma yake,Familia ya kichaka ndiyo ina hisa
 
Sio mabasi tu everything is up from 1st July, Nyama buchani ni 3800 mpaka 4200 kwa kilo, bei ya mafuta petrol ni 1810 mpaka 1850 kwa lita Diesel 2000 mpaka 2015 kwa lita, then tunaongelea maisha bora kwa kila mtanzania, hivi hii 100,000 waliyompa mfanyakazi wa serikali inatosha nini, maana bei ya maharage ni sawa na nyama sasa.

Dagaa usiseme kilo sh. 12000 kwa dagaa la kigoma na la mwanza sh.4000 sasa watu wa kipato cha chini wanaishi maisha ya aina gani kama sio mwaisha bora kwa wateule wakati watu wa kawaida wanakufa na njaa.

" A peacock who sits on his tail is just another turkey"

Tatizo ni sisi wenyewe pia. Tunakubali kila uchafu. Hamna kupinga . Wenzetu wanagomea bei na wanafaulu. Tunauwezo wa kugomea ongezeko la bei .Mfano tukiamua kuzima simu zetu zote kwa siku mbili tu wataimba wimbo waupendao. We have nothing to loose.........
 
Back
Top Bottom