Wizi wa gari

Mkuu pole sana.
Inatakiwa na huyo dereva akae ndani ili aisadie polisi.

FIDEL na Mkuu ARway,
Wazo lako Fidel ni zuri ila sipendekezi huyo dereva awekwe ndani kwani uzoefu unaonyesha kuwa kumuweka ndani hakusaidii kupata ufumbuzi ila kuna ziba mlango wa ufumbuzi.Huko ndani atafundishwa njia ya kukwepa.

Bora Araway ajifanye mjinga kidogo, amtumie huyo Dereva akiwa nje , na hata ikiwezekana amuahidi vijisenti fulani,

Mipango mingine ya wizi inapangwa na madereva kwa katamaa ka pesa kidogo tu.

Nashauri tu wakuu.
 
Kama umekamata huyo dereva wako na shanta wake basi gari lako utalipata tu, ni hao tu wala usihangaike

Kweli kabisa, tafuta askari unayemuamini mpe kidogo kitu atawaminya kiasawasawa hadi watasema.....kumbe ufanyaje? wahi kabla gari haijachinjwa
 
Kweli kabisa, tafuta askari unayemuamini mpe kidogo kitu atawaminya kiasawasawa hadi watasema.....kumbe ufanyaje? wahi kabla gari haijachinjwa

mkuu nilitegemea kodi yangu leo ndio ningeona ikifanya kazi kumbe natakiwa nitoe tena kitu kidogo!!?
 
Shida ya wizi wa sikuhizi gari wanaenda kuzichinja ili wauze spea. Kuna haja ya hii biashara ya used spare parts ikawa properly regulated, as of now sijui nani hasa anawaregulate hawa wachuuzi wa used parts. Ndio wanafuga huu wizi.
 
Hebu lichekicheki maeneo ya Kahumba na Chipukizi linaweza kuwa ndio eneo hawa jamaa walienda kuchukua milupo na kulitelekeza. Just figuring out Morogoro during our time dea
 
Shida ya wizi wa sikuhizi gari wanaenda kuzichinja ili wauze spea. Kuna haja ya hii biashara ya used spare parts ikawa properly regulated, as of now sijui nani hasa anawaregulate hawa wachuuzi wa used parts. Ndio wanafuga huu wizi.

kweli mkuu umesema jambo muhimusana. kuna haja ya hii biashara kuchunguzwa na kuwekewa usimamizi flani ambao utazuia haya matukio ya wizi wa magari. naamini wanafanya hivi wakiwa na uhakika wa soko.wakiiba ya wakubwa lazima sheria zitarekebishwa na hii inaenda sambamba na biashara ya vyuma chakavu.
 
Poe ndugu. Hainingii kichwani kuwa derava anapata kilaji ndani ya bar anamwachia d/waka gari na linaondoka kilaini kiasai hicho. Inakuwaje derava au daiwaka anywe pombe na abiria halfu akmbie eti gari imeondoka!!!! Kwanza dereva yoyote yule funguo za gari unahifadhi mahali salama na si mezani tena kwa walevi!!!! Elimu ya usalama wa gari na dereva hawakuipata??? Tatizo madereva wetu wanajifunzia vijiweni na kujipatia leseni za juu kwa juu, tena mkoa wa Morogoro trafic ndiyo unaongoza kwa leseni za vichakani!!! Nakumbuka hata madereva wengi Dar leseni zao wamezipatia Moro hasa class C. Namkumbuka jamaa mmoja wa trafic enzi hizo kazi yake ni leseni za vichakani na ilikuwa ukimpa mtu nauli na posho aende Moro kufuata leseni unaletewa kesho yake!!! Sijui bado yu hai au wapi yule trafic ambaye ndiye aliyetujazia madereva wazwmbe kwa ajali kwani hawana elimu yoyote ya usalama wa abiria na magari wanayoendesha!!??? Tunaelekea wapi?????
 
Rafiki yangu, pole sana.
Mazingira na jinsi gari lilivyoibiwa, akika hutalipata tena na tena.Mara nyingi magari yanayoibwa kutokana na uzembe wa madreva huwa hayapatikani kabisa,hivyo ondoa wazo la kulipata tena,hilo sahahu kabisa.
Kama unataka gari lako lipatikane, basi dreva wako pekee ndo wakukupatia gari lako, full stop.Unajua wewe umeleta mada hapa si kuitaji msaada, inaoneka hata gari hujaibiwa.Watu wanachangia kuwa mbane dreva wako wewe unasema ulimwamini mno,akili huna kabisa,tena wewe mjinga, hulimwani ni mke wako au nani.Sasa kwa taarifa yako dreva ndo ana gari lako, kwaheri.
We MTU ulinitukana sana ujue?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom