Wizi wa gari

araway

JF-Expert Member
Sep 26, 2007
534
144
nikiwa naimani ya kuwa JF ni zaidi ya kijiji na kina mawakala kila kona ya nchi hii naamini pia naweza kupata msaada mkubwa humu wa kimawazo kutokana na tukio la wizi wa gari lilioniksibu.

nimeibiwa gari aina ya NISSAN SUNNY T553 ATW jana usiku mjini morogoro.nimefikisha suala hili police na kupewa rb no(MOR/RB/756/09)WIZI WA GARI TAR 22/07/09.

NIKIAMINI KIJIJI HIKI KIMEJAA WATU KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI NA WAKADA MBALIMBALI NATUMAINI KUPATA MSAADA WA KIMAWAZO NA USHAURI KUTOKAA KWENU!

NI KAGARI KANGU KA KWANZA JAMANI!
 
Ilikuwaje mkuu? ulipark home, bar, au wapi?......mPM Chaku yupo Moro as well anaweza kusaidia...though mwenyewe nipo Moro!

Just eleza vizuri ilikuwaje .....waweza ni PM pia!
 
Ilikuwaje mkuu? ulipark home, bar, au wapi?......mPM Chaku yupo Moro as well anaweza kusaidia...though mwenyewe nipo Moro!

Just eleza vizuri ilikuwaje .....waweza ni PM pia!

maelezo niliyoyapata kutoka kwa dereva wangu ni kwamba alimpa kijana mmoja anayemfahamu funguo amuangalizie wakati yeye kaingia kambarage bar kujisaidia, baada ya hapo yule kijana aliyeachiwa akaondoka na watu wawili ambao kwa madai yake walikuwa washawahi kufanya nao biashara, walimwambia awapeleke mambo club walipofika wakamwambia pale pamepooza watafute bar iliyochangamka, wakaelekea bar moja mitaa ya chamwino inaitwa mriti na hapo wakanywa pombe na jamaa akaacha funguo juu ya meza kuelekea maliwatoni.alivyorudi akakuta meza tupu na jamaa washaondoka na gari. habari ndiyo hiyo mkuu!!

nitashukuru kwa ushauri wako mkuu napatikana 0715026030
 
Araway
Hiyo ni fixi kabisaa, kaa chonjo na huyo dereva wako, yumo kwenye mipango

bwana fathila nashukuru kwa kunialert, najitahidi kutomwamini lakini nashindwa. nilimwamini sana .
 
huo ni mchongo kamata dereva na huyo rafiki yake, kwa nini huyo rakifiki yake aondoke baada ya kupewa funguo
 
huo ni mchongo kamata dereva na huyo rafiki yake, kwa nini huyo rakifiki yake aondoke baada ya kupewa funguo

Yaani kwa maelezo ya jamaa inaonekana wazi kabisa dereva au huyo kijana wake kama si wote kwa pamoja kuna mmoja anashiriki huo wizi.
 
Rafiki yangu, pole sana.
Mazingira na jinsi gari lilivyoibiwa, akika hutalipata tena na tena.Mara nyingi magari yanayoibwa kutokana na uzembe wa madreva huwa hayapatikani kabisa,hivyo ondoa wazo la kulipata tena,hilo sahahu kabisa.
Kama unataka gari lako lipatikane, basi dreva wako pekee ndo wakukupatia gari lako, full stop.Unajua wewe umeleta mada hapa si kuitaji msaada, inaoneka hata gari hujaibiwa.Watu wanachangia kuwa mbane dreva wako wewe unasema ulimwamini mno,akili huna kabisa,tena wewe mjinga, hulimwani ni mke wako au nani.Sasa kwa taarifa yako dreva ndo ana gari lako, kwaheri.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokukumba!kuhusu wizi wa magari siku hizi saloon cars ikiibwa basi jamaa huwa wanalichinja!yanh kutenganisha kila kitu kivyake,Engine inauzwa Kariakoo,gear box morogoro , milango Arusha yanh kulipata ni ngumu sana!kuna jamaa yangu aliibiwa gari yake Corrola moshi hakuipata hadi leo,inasemekana magari madogo yanayoibwa yanapakiwa kwa container usiku na kuchinjwa likifika dar linafika scrap tupu!pole sana ndugu!hope ulikua umewekea comprehensive insurance at least unaweza kuanza kusumbuana nao wanaweza wakakulipa walau kifutia jasho ,kama uliweka thamani halisi ya gar utarudishiwa ila kama ulijipunja manake sis wabongo gar ina thaman ya milion 10 una declare milion 5!likiibwa insurance wana compesate ile milion 5 na si 10 ! pole mkuu!
 
Ebwana pole sana,najua ni jinsi gani imekuuma.
Nami imenitokea hivyo hivyo na chakushangaza tarehe hiyo hiyo ya 22 lakini June!!!!Yaani last month,yangu walichukua RAV 4 kaka,nimehangaika mpaka sasa hakuna dalili ya kuipata.HAWA JAMAA ni wakuchinja kabisa tukiwafahamu.
Pole sana kaka
 
Rafiki yangu, pole sana.
Mazingira na jinsi gari lilivyoibiwa, akika hutalipata tena na tena.Mara nyingi magari yanayoibwa kutokana na uzembe wa madreva huwa hayapatikani kabisa,hivyo ondoa wazo la kulipata tena,hilo sahahu kabisa.
Kama unataka gari lako lipatikane, basi dreva wako pekee ndo wakukupatia gari lako, full stop.Unajua wewe umeleta mada hapa si kuitaji msaada, inaoneka hata gari hujaibiwa.Watu wanachangia kuwa mbane dreva wako wewe unasema ulimwamini mno,akili huna kabisa,tena wewe mjinga, hulimwani ni mke wako au nani.Sasa kwa taarifa yako dreva ndo ana gari lako, kwaheri.

nashukuru mkuu kwa kuniona hivyo! lakini kama kwa muda wa miaka miwili unampa mtu million 10-20 akupelekee bank bila ya escort na anapeleka bila ya tatizo kuna haja ya kutomuamini mtu kama huyo kwa kagari kasiko zidi 10m? imani hujengwa kwa vitu vidogo mkuu.
 
maelezo niliyoyapata kutoka kwa dereva wangu ni kwamba alimpa kijana mmoja anayemfahamu funguo amuangalizie wakati yeye kaingia kambarage bar kujisaidia,
Sina tatizo na yeye kwenda kujisaidia, tatizo langu kwa nini ampe fungua mtu mwingine.....eti kwa kuwa ameingia kujisaidia....how long could kujisaidia would have taken him mpaka akabidhi funguo....huo ni uwongo.....aliingia Kambarage Bara kukata kilaji...akamwachia DEIWAKA....na huo ni mchezo wake wa siku nyingi!

baada ya hapo yule kijana aliyeachiwa akaondoka na watu wawili ambao kwa madai yake walikuwa washawahi kufanya nao biashara,
Rejea maelezo yangu hapo juu, kwa nini huyo kijana achukue jukumu la kuondoka na wateja...kwa kuachiwa tu ufunguo wa gari? mamlaka ya kuondoka na wateja aliyatoa wapi hapa? Na je dereva wako alijuaje ''hao jamaa wawili'' ndio wale waliowahi kufanya nao biashara wakati yeye hakuwahi kuwaona siku ile kudhibitisha kauli ya kijana? Na je angejuaje yule kijana alikuwa anamdanganya au la?

walimwambia awapeleke mambo club walipofika wakamwambia pale pamepooza watafute bar iliyochangamka, wakaelekea bar moja mitaa ya chamwino inaitwa mriti
Well, huyu kijana hii authority ya kuondoka na gari Kambarage aliipata wapi? nani alimwambia apakie abiria....wewe ndivyo mlivyo kubaliana na dereva wako kuwa anaweza na yeye kuajiri mtu mwingine? nani alithibitisha kuwa yule kijana alikuwa qualified driver na kuzunguka na hao wateja sehemu zote hizo hata bila kumsitua dereva wako kinachoendelea ila hata aweze kuwafuata huko waliko?

na hapo wakanywa pombe
Deiwaka anakaa chini kunywa pombe na wateja....bila hata ya kumwambia dereva wake...then na dereva hata baada ya kumaliza kujisaidia alishindwa kumtrace huyo kijana mkuu?
na jamaa akaacha funguo juu ya meza kuelekea maliwatoni.
....Boya, kwa nini aache fungua za gari mezani hapo bar wakati watu aliokaa nao they just wateja?
alivyorudi akakuta meza tupu na jamaa washaondoka na gari
Everyone could expect that mkuu!.....hiyo gari aliwapa hao jamaa!

nitashukuru kwa ushauri wako mkuu napatikana 0715026030
NimekuPM zingatia ushauri huo kama unataka kweli kupata gari lako mkuu!
 
Kama umekamata huyo dereva wako na shanta wake basi gari lako utalipata tu, ni hao tu wala usihangaike
 
pole sana mkuu,ila never mind,hayo ni mambo madogo sana,maadamu uhai wamekuachia!! kaza buti mtu wangu,utalopata jingine
 
Back
Top Bottom