Wizi mpya simu za mikononi waingia kwa sms

maju

Senior Member
Oct 20, 2011
118
28
Watanzania wenzangu kuna wizi mpya unaotumiwa na kampuni inayotoa huduma kushirikiana na makampuni yetu ya simu za mnkononi inayojitangaza kupitia radio ya clouds FM, kwamba wanauza magari, viwanja , kupangisha nyumba na kutafutia watu kazi.Utafiti uliofanyika umeonesha dhairi hii kampuni ni ya kitapeli na haina uwezo huo technically.

Hawa wahuni wanachofanya ni kumiliki namba ya SHORT CODE mfano; 155xx ect, ambayo hutolewa ana TCRA kisha kuisajili kwenye makampuni ya simu ili wagawane mapato kwa kila sms zipitiazo kwenye SHORT CODE hiyo (kila sms Tshs. 500). Kisha huitangaza kwa nguvu zote kwenye Radio station husika.

Mtanzania anayetuma sms huliwa pesa zake wakati hawa jamaa hawana hata database ya huduma husika, hata ofisi zao hawana hata miundombinu zaidi ya komputa ya muhudumu wa ofisi. Mwisho wa siku hawa jamaa hupitia kwenye makampuni ya simu kufuatilia sms zilizoingia ili wapate mgawo wao.

Nawasihi watanzania tuwe makini na hizi promosheni za wizi zinazopitia short code zitolewazo na tcra kwenye simu za mkononi. Na TCRA wawe makini na watu wanaowapatia hizi short code kwani watanzania wanazidi kuibiwa na hawa matapeli.
 
Hivi TZ itakuwa kichwa mwendawazimu mpaka lini?HIVI YULE MCHUMIA TUMBO WA BUMBULI ANAHABARI HII,maana hv sasa kapewa unaibu wawizara inayohusika na mawasiliano.
 
kaaaaazi kweli kweli tutaliwa mpaka lini wabongo jamani!!!!!!!!!!!!!!! hopefully huyo mchumia tumbo wa bumbuli kwa vile huwa anapita anga hizi anaweza kuipata hii taarifa
 
Hapa ninavyoona tusiwalaumu Clouds fm kwani wao kazi yao ni kufanya biashara ya matangazo tuu.
Wa kulaumiwa ni TCRA tuu.
 
Jamani ninyi nanyiiiiii heeeeeee
Mwl Nyerere alipata kusmema hivi, "mtu mwenye akili akikwambia jambo la kipuuzi kabisa, akiwa anaamini kuwa ni la kipuuzi, na anjua kuwa unaakili, lakini ukalikubali! atakudharau sana"
sasa wewe unajua kabisa kuwa hakuna kazi inayopatikana katika sms, wala hakuna kiwanja ndani ya sms, na wewe ukatumia ubongo wako na ukatuma huo ujumbe unategemea nini hapo!???
 
Watanzania wenzangu kuna wizi mpya unaotumiwa na kampuni inayotoa huduma kushirikiana na makampuni yetu ya simu za mnkononi inayojitangaza kupitia radio ya clouds FM, kwamba wanauza magari, viwanja , kupangisha nyumba na kutafutia watu kazi.Utafiti uliofanyika umeonesha dhairi hii kampuni ni ya kitapeli na haina uwezo huo technically.

Hawa wahuni wanachofanya ni kumiliki namba ya SHORT CODE mfano; 155xx ect, ambayo hutolewa ana TCRA kisha kuisajili kwenye makampuni ya simu ili wagawane mapato kwa kila sms zipitiazo kwenye SHORT CODE hiyo (kila sms Tshs. 500). Kisha huitangaza kwa nguvu zote kwenye Radio station husika.

Mtanzania anayetuma sms huliwa pesa zake wakati hawa jamaa hawana hata database ya huduma husika, hata ofisi zao hawana hata miundombinu zaidi ya komputa ya muhudumu wa ofisi. Mwisho wa siku hawa jamaa hupitia kwenye makampuni ya simu kufuatilia sms zilizoingia ili wapate mgawo wao.

Nawasihi watanzania tuwe makini na hizi promosheni za wizi zinazopitia short code zitolewazo na tcra kwenye simu za mkononi. Na TCRA wawe makini na watu wanaowapatia hizi short code kwani watanzania wanazidi kuibiwa na hawa matapeli.

Ni kweli na hii naona Clouds wanashirikiana nao kwani wameipigia debe sana kampuni hiyo, mie nilisikiliza kwa makini sana na nikajaribu kama mtangazaji wa Clouds alivyoelezea baada ya kutuma SMS yangu nilishangaa kuona kuwa hakuna kitu nilichoulizia na badala yake nikaambiwa kuwa hivi sasa wana huduma ya mashamba na nyumba tu, then nikajaribu kuulizia huduma ya hayo mashamba napo nikajibiwa kuwa huduma hiyo hawana ila wana huduma ya magari tu,

TUWE MAKINI SANA NA MATANGAZO YA CLOUDS, NAKUMBUKA CLOUDS WALIWAHI KUTANGAZA SANA AGENT WA KAMPUNI YA KUUZA MAGARI YA SBT DAR ES SALAAM, NA NILIPOWAULIZIA WAHUSIKA KULE JAPAN WAKANITAHADHARISHA KUWA MAKINI NA MTU HUYO AMBAYE KAMPUNI YAO HAIMTAMBUI, MKIMSIKILIZA KIBONDE MTAJIKUTA BONDENI JANGWANI
 
kila kukicha mbinu mpya za wizi na utapeli hubuniwa,kutibu hili tatizo ni kuwa vyombo vya dola vinatakiwa kwenda na wakati kwa kuwatibulia hawa matapeli njama zao kwa kuzianika hadharani na kuwakamata wahusika,wana jf mupo juu karibuni itabidi tuwakabidhi magwanda!
jaribu kufanya hesabu ndogo tu
500 kwa sms 1 mara watumaji 40000/= kwa siku=20000000/= ni milioni ishirini na watumaji huwa ni zaidi ya idadi hiyo mara dufu kwa maana hiyo hawa jamaa wamejipanga na kama ni mtu wa kawaida tu ukiwaandama wanakuuwa bila kusita ili mpango wao uendelee.
 
January inabidi alifanyie kazi hili sio kuuza sura tu kwenye makampuni hayo ya simu
 
aisee...hata mimi nilijaribu na sikupata response.imagine watu laki moja wakituma sms......500x100,000=50,000,000/=Cash
 
Watanzania wenzangu kuna wizi mpya unaotumiwa na kampuni inayotoa huduma kushirikiana na makampuni yetu ya simu za mnkononi inayojitangaza kupitia radio ya clouds FM, kwamba wanauza magari, viwanja , kupangisha nyumba na kutafutia watu kazi.Utafiti uliofanyika umeonesha dhairi hii kampuni ni ya kitapeli na haina uwezo huo technically.

Hawa wahuni wanachofanya ni kumiliki namba ya SHORT CODE mfano; 155xx ect, ambayo hutolewa ana TCRA kisha kuisajili kwenye makampuni ya simu ili wagawane mapato kwa kila sms zipitiazo kwenye SHORT CODE hiyo (kila sms Tshs. 500). Kisha huitangaza kwa nguvu zote kwenye Radio station husika.

Mtanzania anayetuma sms huliwa pesa zake wakati hawa jamaa hawana hata database ya huduma husika, hata ofisi zao hawana hata miundombinu zaidi ya komputa ya muhudumu wa ofisi. Mwisho wa siku hawa jamaa hupitia kwenye makampuni ya simu kufuatilia sms zilizoingia ili wapate mgawo wao.

Nawasihi watanzania tuwe makini na hizi promosheni za wizi zinazopitia short code zitolewazo na tcra kwenye simu za mkononi. Na TCRA wawe makini na watu wanaowapatia hizi short code kwani watanzania wanazidi kuibiwa na hawa matapeli.

Mkuu umenena kweli. Mie nilituma kudadisi kazi fulani wakanilletea web address ya Zoomtanzania - na kweli kule siku hiyo kulikuwa na nafasi hiyo. Lakini hiy web inatembelewa sana. Lakini je ambao hawana accessibility ya internet je. hata hivyo wao walitakiwa watoe digested information ili mtu awasiliane na watoa kazi moja kwa moja sio kuishia kukata 300/=.
Clouds wanawapromote hawa ma TP ni juu yao kuwa question baada ya kupata malalamiko haya - sio kuchukua kila hela hata ile yenye taint ya damu.
kuna mchango wa mwanahabari mmoja - clouds wakatangazqa na kusambaza namaba ya simu ya kutuma hela MPESA zikawa zinaingia kwa one ELIZABETH. baada ya kudadisi mbona hela inaiingia kwa huyu badala ya jina la Mwanahabari aliepata ajali miaka iliyopita hakuna jibu lililopatikana.

Ulaya wananunua hizi short codes kuweka miguno - si ajabu na kwetu ikaja hiyo kama TCRA hawataamka usingizini
 
Jamani nimeamini wizi upo kwenye hii mitandao hata tiGo wanadai piga *148*01# utapata internet kwa 450/ data siku au 700/ standard au Vodacom 250/ nimenunua zote hamna kitu hela inaliwa
Kuja wauliza mm natumia BlackBerry wakaniambia hao B/Berry wanatumia mitandao yao hawahusiki na Internet na hela wameipokea hairudishwi
Ushahidi ni facebook ukiwabana huko wanakiri hawahusiki
Nimewaambia kwa nini wanatangaza uongo? Afadhali watumiaji watahadharishwe
 
Tatizo hawa jamaa BR Solution Waliiba hiyo idea kwa mtaalam moja ila wakashindwa kui implement ni vilaza watupu. sasa wameishia kuwaibia watanzania. system yao iko empty haina database yoyote ya huduma wanazotoa. sasa wanadirect watu kazi website ya zoomtanzania.com. kwani kuna gharama gani kufungua website ya zootanzania.com. ni wezi ambao hawajajipanga.
 
Hiyo kitu ni uwizi, jana nilituma sms 15450 kufanya testing ya system yao.
Warudisha message eti samahani hawana huduma hiyo kwa sasa jaribu huduma nyingi.
 
kaaaaazi kweli kweli tutaliwa mpaka lini wabongo jamani!!!!!!!!!!!!!!! hopefully huyo mchumia tumbo wa bumbuli kwa vile huwa anapita anga hizi anaweza kuipata hii taarifa

Mpaka siku tutakayoamka na kuamua kuitumia kura yetu kwa pamoja kuipinga hii serikali legelege isiyokuwa na msimamo wa maendeleo bali wa wizi tu!
 
Back
Top Bottom