Wizi mdogo mdogo hatimae mkubwa SWISS PORT-JNIA

Ngonalugali

JF-Expert Member
Jan 12, 2008
659
102
Habari zenu wana JF,

Ni kwamba kuna utaratibu kwenye viwanja vya ndege kuzuia abiria kubeba vichupa vyenye vimiminika zaidi ya ml100. Kwa hiyo inalazimu abiria kulazimisha kupima mzigo hata kama una 6kg ili mradi kusalimisha mafuta na vi-manukato kwa namna moja ama nyingine.

Kitu kilichojitokeza pale ni kwamba kampuni ya kupakia na kupakua mizigo ya Swiss port imeshindwa kudhibiti wafanyakazi wake na hivyo kupoteza hadhi ya kuchukua dhamana ya mizigo ya abiria. Nilichokiona mimi ni kwamba wale jamaa wanaobeba mizigo hufungua zipu na kukagua kilichomo ndani. Wakiona kitu cha thamani wanaweka mifukoni mwao. Na kinachoumiza ni kwamba kama kuna vitu vilikuwa kwenye mifuko midogo ndani ya begi ambavyo labda ulitaka visigusane na vingine basi utavikuta tofauti, maana wanachana vimifuko ili kutafuta wanachokitafuta wao (WIZI MTUPU), ustaarabu hakuna hata kidogo.

Sasa nataka kuuliza kuna usalama gani kama mtuu amepima mzigo ili kufuata sheria za usalama wa usafiri wa anga na hatimae wajinga wachache wapitie vitu vya thamani kwenye mizigo yake?
Na je, hii itatoa picha gani kwa abiria wapendao kutumia viwanja vyetu kusafiri kwa kuchukulia kuwa ni salama kwa kwa mali na mizigo yao?
 
Ndugu yangu una uhakika na POST yako? ninavyojua mimi mizigo kama uliyotaja hapo HAIPIMWI, inapitishwa kwenye screen,kikionekana kiminika chenye ujazo tajwa kulingana na sheria za kimataifa unatakiwa ukiache PALE PALE au ukakicheck in, mimi nautumia sana huo uwanja na sijawahi kuona vitu kama hivyo. besides tuwe na kawaida ya kusoma matangazo yaliyobandikwa bandikwa ni ili kujua kinachoendela, utaratibu huu haujaanza leo.
 
nimeandika kilichotokea. ni kwamba mzigo ukiwa na vimiminika unalazimika kuupitisha chini ili kuepuka usumbufu wa kunyang'anywa unapokwenda kwenye check in ya pili na ya mwisho.

Kilichofanyika ni kwamba jamaa wanafungua zip na kuangalia kama kuna kitu ambacho wanaweza kujichukulia haraka haraka. Niliamua kuwa napitisha begi dogo chini baada ya kunyang'aywa mafuta kwa kuzingatia usalama wa anga.

It is true kwamba Jamaa wa swissport wanafungua vifurushi na mimi ni mwathirika wa kwanza kama haijatokea kwa mwingine maana nimelizwa vitu vyangu ikiwemo simu ambayo sikutaka kuitumia wakati wa safari.
 
Ndugu yangu una uhakika na POST yako? ninavyojua mimi mizigo kama uliyotaja hapo HAIPIMWI, inapitishwa kwenye screen,kikionekana kiminika chenye ujazo tajwa kulingana na sheria za kimataifa unatakiwa ukiache PALE PALE au ukakicheck in, mimi nautumia sana huo uwanja na sijawahi kuona vitu kama hivyo. besides tuwe na kawaida ya kusoma matangazo yaliyobandikwa bandikwa ni ili kujua kinachoendela, utaratibu huu haujaanza leo

MKUU KANDAMBILI LABDA TUSAIDIANE HAPA,NI KWELI HUWA WANAIBA NA WALA SI SIRI
NJOO HAPA UWANJANI UONE MWENYEWE,,VIMIMINIKA VINARUHUSIWA KWA UJAZO MAALAUM SASA UKISHAWEKA WANAOTAKA WAO UNARUHUSIWA KUWEKA KWENYE BEGI LAKO!!!SASA BASI SHUGHULI PEVU INAANZIA PAALE MZIGO UKISHAPIMWA UNAINGIZWA KUELEKEA KWENYE KARANDINGA,,SI LILELE LA MRAMBA ,HILI LA MIZIGO..WAKATI IKIPITWA WANAKUWEPO WENYEWE NA WAKATI MWINGINE WANASHIRIKIANA NA SECURITY WA AIRLINE HUSIKA WAANAOKUWA WAKIANGALIA WAKATI WA CHECK
IN,,WASIVO NA AIBU WALISHAWAHI KUNIIBIA HADI SAMA KI SIKUMOJA NA TOKEA MWANZA KUJA DAR!!1NIKAMWOMBA NDUGUYANGU MMOJA AKANIANGALIZIE KABLA SIJAWASHA MOTO NIKAKUTA WANASHUKA NA MFUKO WASAMAKI!!WALIPOBANWA WAKADAI TUMECHUKUA NDOO NYINGINE!!!!KAZI PALE NI KUBWA MNO MNO,,TUMESHASHAURI KWA BOSS WAO TEMU ANA KAZI KUBWA KUREKEBISHA HII KAMPUNI SI KAMA ABIRIA TUNAJIFUNZA NINI!!!!????

SEHEMU NYINGINE ZA WIZI NA RUSHWA NI PALE KWENYE MIZIGO WAKATI WAKIPIMA!!!!
NILILALAMIKA SIKUNA SAFIRI WALININYANYASA SANA HAO PAKA KUNIAMBIA MZIGO WANGU UMEZIDI KILO KADHAA ,,KUMBE UONGO MAANA ILE MIZANI WANAKUWA WANSOMA WAO,THEN WANAKUTISHA ,,USHAURI WANGU MKIWA MNAPIMA MIZIGO SOMENI WENYEWE KILO MSISIKILIZE WAFANYAKAZI!!WAKO PALE KUCHUMA

IKI
 
Hili jambo naona halikuwagusa sana JF members, lakinii kuna mtu kaitoa huku na kuipeleka kwa MICHUZI naona watu wengi wametoa dukuduku lao.

Sina shaka kuwa jambo hili limewagusa wengi, na nia yangu ilikuwa ni kuamsha watu wengine ambao hawajaumia waangalie sana namna ya kutunza vitu vyao.
Mimi nashangaa sana kwani niliwahi kusafirisha kamera kwa meli kutoka Japan kwa kusudi la kukwepa gharama za ndege na haikusafirishwa kama kamera bali iliwekwa kati kati ya vitu na ikafika bila matatizo.
Mind you, lengo lilikuwa kamera lakinii ililazimu kuweka nguo kadhaa na kufunga ndani ya boksi ambapo ilifika. Hiyo inaonyesha kabisa kuwa wale watu ni waaminifu maana wangepekua kamera isingefika.

Madhani kuna kila haja ya swissport kujirekebisha ili lisijekuwa doa na kuharibu kabisa soko kwa watu ambao wangependa kupitia JNIA.
 
Back
Top Bottom