Wizi katika Vituo vya Mafuta!!!

ABEDNEGO

Senior Member
Aug 20, 2009
109
30
Ni saba saba day, nimeenda kwenye vituo tofauti tofauti vya mafuta(Petrol stations) nikitaka diesel kwa ajili ya ka-generator kangu nikijihami na mgao wa umeme,Sasa niliyoyakuta huko ndo yananifanya niwaulize wana-JF wenzangu.Nilikuwa na vidumu viwili vya lita tano tano,Sasa kila kituo nilichoenda naambiwa hawajazi diesel kwenye vidumu(Eti sheria mpya ya EWURA) Sikuamini maneno ya wahudumu kuanzia Mbezi Louis hadi Ubungo Plaza kituo cha Engen(Vituo 9) ndo walikubali kunipa kwa shingo upande!!! Kwa kuwa nilihitaji lita kumi tu dumu la kwanza lilijaa la pili kama lita tatu hivi.Maana yake nilipata lita nane kwa gharama za lita kumi.Hapo nikaelewa maana ya kukataa vidumu vyenye ujazo unaoeleweka.Kwa hali hiyo vituo vya mafuta Jijini Dar vinatuibia sana!!EWURA wanalijua hili au wako zaidi kwenye uchakachuaji tu?
 
Nimejaza ulingano wa lita tano na wala siyo pomoni,Swali langu kweli EWURA wanazuia kujaza diesel kwenye vidumu???
 
tena afadhal umeenda na kidumu cha lita tano, ukienda na cha lita moja ndo hawakupi kabisa kwa kuwa wanajua waz kwamba kitafika robo tatu kwa hiyo utashtukia, Vituo vya Dodoma vingi vina kasumba hiyo labda kile cha Gapco karibu na keep left ya mgahawa wa wimpy ndo ambao si wezi
 
Hawa jamaa wanatuliza sana siku nenda na kidumu wakikomaa waambie wewe niafsa wa EWURA uwasikie mstuko wao watakupoza fasta na Millioni
 
EWURA walikataza vidumu, ila hakutoa ufumbuzi kwa wanaonunua kwa ajili ya jenereta au kukatikiwa mafuta njiani.
 
EWURA walikataza vidumu, ila hakutoa ufumbuzi kwa wanaonunua kwa ajili ya jenereta au kukatikiwa mafuta njiani.
Kama EWURA walizuia wanajua madhara wateja wanayoyapata? Nikizimikiwa gari njiani mafuta yameisha niwaite EWURA kusukuma liende petrol station? Je TANESCO nao niwaombe lori lao lijazwe wakafaulishe kwenye jenerata yangu?Watoe ufumbuzi na siyo kuwajengea mazingira ya kutuibia na kutukomoa.
 
hapo kwenye kuzuia vidumu, ewura walichemka, na kawaida yetu watanzania kukubali makosa ni ngumu sana, wameshasikia mararamiko juu ya agizo lao ila wapo kimya, ilhali wananchi twaendelea teseka.
 
nakujibu kama meneja wa kituo cha mafuta jijin dar es salaam.
sheria ya kuzuia vidumu ilipitishwa na ewura mwaka huu na imejieleza wazi kabisa, haviruhusiwi vidumu vya maji ya uhai na jamii hiyo,sababu surface yake ni ndogo,sio hivi vidumu vingine nyenye surface kubwa,hii ni kwa sababu vidumu nyenye surface ndogo haviwez kukabiliana na density ya petrol vinaweza kupasuka endapo kitapata mtikisiko mkubwa. nazungumzia surface area to volume ratio.
 
Huku Arusha ndiyo usiseme huo uchakachuaji ndiyo imeshika kazi. Kwa mfano kwa wenyeji wa hapa Arusha wanaoielewa ile ki2o kongwe hapa mjini cha Bamparass kilichopo mtaa wa Mianzini ni hatari wanaweza kukuwekea hata hewa. Ila nitajifanya siku moja mi ni afisa wa EWURA halafu ha2taelewana kabisa. Wizi mtupu!
 
kuhusu kuchakachua kwa maeneo ya mjini sio rahisi mkubwa,hao jamaa wa ewura wanakagua karibu kila wiki wanapita kuchek,then kule kwa vendors napo kabla tanker haijatoka inawekewa drops flan hivi,kuna kampun moja ya kisanii inaitwa global fluids international.hizo drops endapo utachanganya mafuta yatabadilika na kuwa creamy colour.
 
then ili kuepukana na hayo ya uchakachuaji,nakushauri uwe na kituo kimoja cha kujaza mafuta ambacho unakiamini,ucjaze mafuta kila kituo kwa usalama wa gari lako,kama inatokea tatizo inakuwa rahisi kujua ni wapi liliposababishwa. ilishatokea jamaa kajaza mafuta kwangu alaf kaenda bigbon napo kajaza katembea kilimita 12 taa ya check engine ikawaja akachukulia poa mda kidogo ikazima,kaikokota mpaka kituon kwangu mafund wakamuangalizia ikawa ameua sensor kakomaa kwamba mafuta yetu ndo yemesababisha.ikwawa balaa anarisiti bili tofaut yangu na ya bigbon so wapi kanyonya mafuta machafu .so hatukumuelewa. ikabidi ile kwake katoa laki tano ya sensor tumbadilishia gari ikawaka.
so tuwe makini kidogo na vituo vyote.
mafuta kupewa kidogo tofauti na lita ulizopewa inategemea na aina ya pump kuna za digital na manual. so kwenye manual kama hazichekiwi kila wiki ni rahisi kutoaa wrong results.
 
Huku Arusha ndiyo usiseme huo uchakachuaji ndiyo imeshika kazi. Kwa mfano kwa wenyeji wa hapa Arusha wanaoielewa ile ki2o kongwe hapa mjini cha Bamparass kilichopo mtaa wa Mianzini ni hatari wanaweza kukuwekea hata hewa. Ila nitajifanya siku moja mi ni afisa wa EWURA halafu ha2taelewana kabisa. Wizi mtupu!

Mkuu kituo ambacho naona hawaibi sana ni Njake pale Mianzini na kama una uwezo nenda BP ingawaje huko kidogo mi simudu.
Ila vidumu hapa Ar hawako strict sana kwani huwa sipati shida nikinunua mafuta ya jenereta
 
Nakumbuka kuna kituo kimoja walikuaga wanaiba mafuta laivu kile pale mwanamboka,kinondoni sijui kama sasa hivi wamejirekebisha ulikua ukienda kuweka mafuta pale kama ni lita kumi utajikuta umewekewa lita 5,nilishawahi kumhoji dada mmoja anayeuza sheli akaniambia wao wanakabiziwa mafuta mfano lita 30,000 kama lita moja ni elfu mbili kwa hiyo wakishauza mafuta yote wanatakiwa wakabizi 30,000*2000 ambayo jumla ni 60,000,000 kwa hiyo ni wao akili kichwani,kuchakachua,kuminya pumpu mwisho wa siku ikipatikana extra wanagawana,na hawa wenye sheli mara ingine wanapataga hasara kubwa manake nasikia dereva wa yale matenka wakati mwingine wanaamuaga kuuza mafuta yote kwenye hayo matenka halafu analipindua tajiri akija anajua lilipopinduka mafuta yakamwajika kumbe dereva kauza mafuta ili asituhumiwe akaamua alipindue
 
Mimi huwa najiuliza kwani haiwezekani ile mipira ya pump za mafuta ikawa myeupe ili nione mafuta yanavyoingia? manake naamini ikiwa myeupe nitaona kama anaminya au la. Hivyo ilivyo myeusi ndo inaweka room ya wizi wa dizaini hiyo... halafu unakuta muuzaji ameshaseti kiasi cha mafuta but bado lazima anaminyaminya lile bomba, kwanini kama sio kubana mafuta? manake mimi naamini akishaseti anatakiwa aweke tu pipe ktk tanki aache ijae yenyewe then ikimaliza ndo atoe sio ashikilie muda wote wakati keshaseti....
 
nakujibu kama meneja wa kituo cha mafuta jijin dar es salaam.
Sheria ya kuzuia vidumu ilipitishwa na ewura mwaka huu na imejieleza wazi kabisa, haviruhusiwi vidumu vya maji ya uhai na jamii hiyo,sababu surface yake ni ndogo,sio hivi vidumu vingine nyenye surface kubwa,hii ni kwa sababu vidumu nyenye surface ndogo haviwez kukabiliana na density ya petrol vinaweza kupasuka endapo kitapata mtikisiko mkubwa. Nazungumzia surface area to volume ratio.

tunashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri sana meneja...but kutokana na hali ilivyo kwamba kuna vituo vinakataa na vingine vinakubali inaelekea bado hawajaelewa vizuri kama kuna madumu fulani yanakubaliwa na mengine yanakataliwa. Nakushauri ulifanyie hilo kazi, ........na kama kuna mtu wa ewura humu, basi ataarifu wahusika ofisini kwao ili wawafahamishe wenye vituo na wananchi wote kwa ujumla kuhusu hili suala...
 
Ulijaza pomoni ndo maana. Inapezekana hujaibiwa.
Nimependa na kufurahia neno hili "pomoni" ni aghalabu kulisikia au kusoma mahala limeandikwa. Hongera Mkuu! Sina hakika kama vijana walowengi wanalitumia.
 
Kumbe ndo maana nanunua mafuta kila siku kwenye kagari kangu na sifiki popote! sasa ntatembea na kidumu. Ila lets be honest..hivi hawa ewura hawa nao vipi mbona bei za mafuta hazijashuka tu mpaka sasa leo tarehe 7?
 
Back
Top Bottom