Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,763
- 764
Jana nilikuwa safarini toka Dar kuelekea Mbeya kwa kutumia usafiri wa mojawapo ya basi la kampuni kubwa hapa nchini. Safari yetu ilikuwa nzuri toka Dar asubuhi hadi mida ya mchana saa saba tulishuka Ruaha Mbuyuni eneo la Al Jazeera kununua vyakula pamoja na kuchimba dawa. Abiria wote walishuka ndani ya gari kondakta anadai alibaki garini mlangoni kuangalia usalama wa basi lile. Tuliporejea ndani ya basi abiria wawili walidai kutoziona laptop zao pamoja na simu zao mbili. Taarifa zilifikishwa kwa dereva nae akashauri tuendelee na safari hadi Ilula ambako kuna kituo cha polisi. Tulifika Ilula na ukaguzi kufanyika ndani ya gari na nje kwenye eneo la mizigo. Hadi mwisho wa zoezi hilo hakuna kilichopatikana na kuthibitisha vitu hivyo kuibiwa. Muda uliopotea safarini kutokana na wizi huo ni zaidi ya masaa mawili na kupelekea kufika Mbeya saa 3.30 usiku.
Swali langu ni kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri pamoja na wahudumu + madereva wamejiandaa vipi/wanalichukuliaje tatizo kama hilo?
Pia wasafiri wanajiandaa vipi kukabiliana na matukio kama hayo ikiwa dhamana ya usalama wa mali zao ipo kwa wahudumu na wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri?