koo
JF-Expert Member
- Mar 9, 2011
- 258
- 67
Umetokea wizi wa HARD DISK za kompyuta muhimu ndani ya wizara ya nishati na madini katika kile kinachodhaniwa ni kupoteza kumbukumbu muhimu za ushahidi wa ufisadi wa wizara.
Kufuatia hatua hiyo inayo sadikika kufanywa na mtandao wa kijasusi unaomilikiwa na mafisadi serikali imeamua kufunga CCTV cameras katika vyumba vyote 189 vya jengo la wizara na vyooni ili kudhibiti watumishi wanaoiba nyaraka kwa lengo la kuvujisha siri za serikali na msako wa aliye toa barua ya Jairo unaendelea kwa kasi huku watumishi wakifurahia kurejea kwa jairo kwa kile kinachosemekana ni mkombozi.
Chanzo changu kinadai bwana Maswi aliyekua anakaimu ukatibu alipunguza posho za watumishi kwa asilimia 50 jambo lililowaudhi watumishi wengi na urejeshwaji wa Jairo ukapokelewa kama ukombozi wa posho zao zilizo fyekwa
Chanzo nichakuaminika.