Wizara ya mambo ya ndani na biashara ya dawa za kulevya ukweli uko wapi?

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
Nisaidieni kuziuliza mamlaka husika,miaka mingi sasa imeipita na sijawahi kusikia mamlaka husika zikitaja ni kiasi gani cha dawa za kulevya zimekamatwa hadi kufikia hii leo? Wasiwasi wangu ni huenda hizi dawa zinarudishwa sokoni na wajanja maana bidhaa nyingine zinatangazwa kwenda kuharibiwa lakini sijawahi sikia madawa ya kulevywa .kama wanayatunza yapo kiasi gani?
 
Kuna yule jamaa alikutwa akitengeneza mandrax katika nyumba yake O'bay. Sijasikia tena kesi yake iliishia wapi. Tena kuna vijana wengi
tu wamekamatwa Dar airport wakiingiza madawa hayo, lakini hatujasikia ni nani alifungwa muda gani jela.
 
Alikuwa akiitwa Nurdin Akasha link yake ilikuwa kubwa mpaka Kenya kama sikosei sijui kesi yake iliishia wapi. Pia kuna mtambo wa kutengeneza Noti bandia ulikamatwa O'bey enzi za Mkapa nao kesi yake sijui iliishia wapi?, yaani bongo bwana noma!
 
Back
Top Bottom