Wizara ya maji na idara zake, nini kazi zao?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,971
13,605
Salam Jf! Kwa ukweli mnaweza kunishangaa nitakapokiri hapa kuwa sijui kazi wanazofanya watu/watumishi walioajiriwa na wizara/idara ya maji. Hivi kazi zao nini? Kwa mfano Dsm pale makao makuu wizarani na kwenye vitengo idarani nini shughuli zao ikiwa Dawasco ndo wanashughulika na usambazaji na upatikanaji wa maji kwa wakazi wa jiji? Ikumbukwe dawasco ni kampuni,inayojiendesha kibiasha na inawafanyakazi wake. Ukija mikoani, kama k'jaro, idara ya maji wapo. Hawafanyi chochote,pale kuna kampuni ya JW ndo inayosambaza maji kwa wakazi wa mji wa moshi na vitongoji vyake,nayo kama Dawasco,ni kampuni inayojiendesha kibiashara na inawafanyakazi wake! Hivi hawa watumishi wa idara ya maji kazi zao ni nini? Inakuwaje watu wanapoamua kutumia nguvu na umoja wao kufuata maji toka milimani na kuyaleta kwenye vijiji kwa ajili ya mtumizi, then waje watu wa idara ya maji kuja kudai pesa, (kama bill ya maji) wakati maji yenyewe yalikuwa yanatiririka na kuingia mtoni na kwenda kusikojulikana.? Hivi wizara ya maji inahusika na maji yapi? Mto,bahari,maziwa, au na yaliyo chini ya ardhi? Mbona haya ya chini ya ardhi watu wanajichimbia na kuyatumia bila kuyalipia? Wao idara ya maji kazi yao ni nini? Kwanini wizara ya maji isifutwe tukawa na mikataba kati ya halmashauri/manispaa/ au hata majiji na makampuni kwa ajili ya kusambaza maji kwa wakazi wa maeneo husika? Na wale wavijijini wakapata maji kupitia makampuni yanayochimba visima, na wakalipwa na halmashauri,. kupitia mikataba kati ya baraza la madiwani na makampuni ya uchimbaji visima, pale itakaponekana pana ugumu serekali kuu iombwe iongeze nguvu...kwa mtindo huu wa kuitegemea wizara/idara ya maji hatutafika. Nawasilisha!
 
kazi yao kubwa ni kuandika Bili kila mwezi na kukata maji pindi mteja anaposhindwa kulipa bili.
 
Nimeamini kuwa ufikiri wa mtu aliye ndani ya boksi hutegemeana na ukubwa wa boksi lenyewe! na hili ni tatizo ambalo linatukuta watanzania wengi saaana. Nadhani kwa sasa tuanze kujenga utamaduni wa kufikiri nje ya boksi. Umesema huelewi kazi zinazofanywa na Wizara ya Maji, lakin ndani yake ukaanza kusema kuwa DAWASCO, Idara ya Maji etc. Mimi nadhani kabla ya kuandika hii thread yako ungejipatia ka home work kadogo ka kuijua sector ya maji inavyofanya kazi nchini, then ndo uaanzishe thread yako. Unless labda kama ulitaka kuelezea tatizo la inefficiency katika Wizara ya Maji, ambalo tatizo hilo linaziikumba taasisi nyingi za Serikali ya Kikwete sio Wizara ya Maji pekee.
 
Back
Top Bottom