Wizara ya fedha kutangaza nafasi 200 za kazi

Gerald David

Member
Nov 2, 2010
10
0
Naibu waziri fedha ameliambia bunge asubuhi ya leo kuwa wizara ya fedha imetenga kiasi cha Tsh. bilioni moja kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi wapya 200 katika mwaka huu wa fedha, aidha waziri amesisitiza uharaka wa kutangaza ajira hizo ili ziweze kusaidia upungufu wa wafanyakazi katika wizara hiyo.
haya wajomba mwezi wa saba wizara ya fedha wanatemesha mzigo kaeni mkao wa kula.
 
Tunashukuru jamani kwa habari njema hizi kwa vijana wetu ambao kweli wamekata tamaa ya maisha maana wengine wamemaliza Ealimu ya juu llakini hawapati ajira. Tunawaombea Wizara ya Fedha waajiri nafasi hizo kwa haki , na Mungu atabariki management yote kwa UAMINIFU wao katika kujaza hizo nafasi. Wenye sifa na watakaofanya interview na kufanya vizuri ndio wapewe.......
 
Tunasubiri tuone. Tukijumlisha na zile za National audit 100, tunapata nafas300. Afadhali japo haijakidhi matakwa kwa kuwa mliman bcom tu wale wa mwaka jana wanazidi nafasi izo,na IFM mwaka jana wamehitimu 400 kwa kozi ya Uhasibu tu. Hapa sijagusia Mucobs,tia,iaa,saut,tumaini,nk. Ok si wote watapata nafasi za serikali ila wajitahidi kuajiri zaidi ili wale wazee waweze kwenda kupumzika. Thanks 4ujumbe.
 
Nina uhakika kati ya watu 200 sitokosa..CV nimeshaiandaa ni kuituma tu!..btw, NAO wametangaza shortlist?
 
Nina uhakika kati ya watu 200 sitokosa..CV nimeshaiandaa ni kuituma tu!..btw, NAO wametangaza shortlist?

nimetoka kwenye paper la INTERNATIONAL TRADE FINANCE Sasa hivi................. hapa CV nmeshka mkononi, sikosi hapo.......kwishney!!!!!
 
Naibu waziri fedha ameliambia bunge asubuhi ya leo kuwa wizara ya fedha imetenga kiasi cha Tsh. bilioni moja kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi wapya 200 katika mwaka huu wa fedha, aidha waziri amesisitiza uharaka wa kutangaza ajira hizo ili ziweze kusaidia upungufu wa wafanyakazi katika wizara hiyo.
haya wajomba mwezi wa saba wizara ya fedha wanatemesha mzigo kaeni mkao wa kula.
POLITIKE......Billioni moja kwa watu 200 ni sawa na basic ya Ths 416,666.67 per month kwa average ya mwaka maana budget ya mwaka...hapo mbwembwe tupu!!!!.mtakuwa mmenisoma

1000,000,000/= divide by 200 = 5,000,000/= hiyo figure inamaanisha freshers watakuwa wachache kwa maana hiyo bilioni moja iliyotengwa ni kwa ajili ya new promotions labda na ma xpertriate, nawakilisha
 
nafasi 200 hazitoshi kabisa, ukizingatia idadi ya wanaomaliza vyuo ni wengi sana kuliko soko la ajila, imefikia wakati watanzania tufikilie ajira
binafsi, ni bora kulima kijijini kuliko kukaa mijini na kujiingiza katika mambo yasiyofaha .
 
wengne mkimaliza shule rudini vijijini mkalime na kuvua samaki kwa utaalamu mlioupata knye vyuo!, mtaajiriwa wangapi nafasi 400 kwa mwaka mnaomaliza mpo 40,000 wap na wap!
 
1000,000,000/= divide by 200 = 5,000,000/= hiyo figure inamaanisha freshers watakuwa wachache kwa maana hiyo bilioni moja iliyotengwa ni kwa ajili ya new promotions labda na ma xpertriate, nawakilisha
Divide by 12 maana ni budget ya mwaka mzima
 
Nipeni email ya mkulu wa kaya, ni-apply kwake moja kwa moja manake haiwezekani kila niki-apply utumishi wa umma sipo hata kwenye short list!
 
kaka hata mimi kila nikituma kitu hakijipi mambo magumu kweli sijui hizi NAO kama watanikumbuka mungu saidia
tusaidiane waungwana
nawasilisha
 
Join Date : 2nd November 2010
Posts : 6
Thanks0Thanked 4,294,967,295 Times in 4,294,967,295 Posts

Rep Power : 0

Naona JF sasa inapoteza image iliyojijengea kwa muda murefu!Huu ni upuuzi na sijui ina maana gani,inachefua sana na kuondoa kabisa maana ya thanks!!
 
Back
Top Bottom