Wizara ya Elimu fuatilieni hili Elimu inakufa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wanafunzi wagoma kufanya mtihani

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha iliyo mkoani Pwani wamegoma kwa siku nne kuendelea na mitahani ya ‘Mock’ kwa madai kuwa maswali mengi yaliyoulizwa yamerudiwa kwani yaliwahi kutoka katika mitihani ya mwaka 2008 na 2009.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana wameilalamikia bodi ya utungaji wa mitihani Kanda ya Mashariki na Pwani (EZEB) na kusema badala ya kutunga mitihani mipya wamenakili iliyopita wakati wao wamechanga fedha kuiwezesha bodi hiyo kutunga mitihani ya kuwapima vyema.

Walisema hawawezi kuendelea na mitihani hiyo kwani haiwawezeshi kujiandaa vizuri na mtihani wao wa mwisho badala yake inawadidimiza kitaaluma kwani tayari mitihani hiyo walishaifanyia mazoezi.

Walitolea mfano wa marudio ya maswali katika somo la Civics wakisema kuwa wameulizwa swali la mwenyekiti wa AU ambalo katika majibu yake ya kuchagua hakuna jibu hata moja kwani waliowekwa wote wameshamaliza muda wao kwa sasa.

“Hatuwezi kuendelea kufanya mtihani kwani haitusaidii chochote katika maandalizi ya mtihani wetu wa mwisho, wakitaka watunge tena tufanye tujipime vizuri lakini hiki walichokifanya bodi ya mtihani hakitufurahishi ndio maana tumeamua kugoma kuendelea na mtihani huu,” alisema mmoja wa wanafunzi kwa niaba ya wengine.

Aidha wanafunzi hao walidai kuwa wamekuwa wakichangia sh 12,000 kwa ajili ya mtihani huo jambo ambalo limewashangaza kwa bodi hiyo kurudia mitihani wakati ingeweza kutumia muda kwa ajili ya kutunga maswali tofauti na mitihani iliyopita.

Mkuu wa shule hiyo Sekundi Kayenga alithibitisha kutokea kwa mgomo huo na kukiri kuwa baadhi ya mitihani ukiwemo wa somo la Baiolojia ilinakiliwa kutoka katika mitihani iliyopita.
 
Good steps...hawa ndio vicha vilivyobakia!!sasa mitihani kama hii mtu ukikutana nayo,unapiga div 1 ya ajabu,..siku ya pepa ya mwisho..dah....zero ya ajabu!!
 
elimu inajifia yenyewe kila mtu kawa mchakachuaji!
Good steps...hawa ndio vicha vilivyobakia!!sasa mitihani kama hii mtu ukikutana nayo,unapiga div 1 ya ajabu,..siku ya pepa ya mwisho..dah....zero ya ajabu!!
 
Back
Top Bottom