Wizara ya Afya na ARV Feki Nayo ni Siasa Chafu?

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
335
Ndugu zangu nadhani wote tumesikia sakata la kusambazwa kwa dawa feki za ARV na inasemekana kiwango kikubwa cha dawa hizo feki zimesambazwa na zinatumika. Kwa kuwa dawa hizi kwa kiwango kikubwa hutolewa bure na serikali katika hospitali nyingi za serikali nini malengo ya wahusika? Je Tanzania Food and Drug Authority ilikuwa wapi wakati kiwango hiki kikubwa hivi cha dawa feki zinazosadikiwa kutoka India zinaingia nchini, Je Wizara inataarifa ni kwa kiasi gani Watanzania wameathirika kwa matumizi ya dawa hizi feki na wako iko tayari kutoa taarifa ya wahusika wote.

Ni hatua gani zilizochukuliwa hadi sasa kwa wahusika? dawa ziliingizwa kwenye mfumo mwezi Mei, 2012 hadi sasa zinaaza kutolewa kwenye mfumo ni miezi minne baadaye, ni hasara kiasi gani serikali imepata kutokana na ujangiri huu kwa maana ya fedha zilizoibiwa kwa dawa hizi feki?

Kwa hili sidhani kama serikali hasa Wizara ya Afya, TFDA na vyomba vya usalama kama wanataka kutuambia kuna uchunguzi unfanyika maana katika hali ya kawaida hakuna kitu cha kuchunguza hapo zaidi ya kuwa tia hatiani wahusika wote.

Aidha, sitashangaa kusikia Wizara inaibuka na kusema taarifa hizo siyo sahihi kama ilivyozoeleka kwa kuwa kwao hilo Tanzania kwa kuwa wako kimaslahi na siasa zaidi kuliko madhara yanayompata maskini mwananchi wa kawaida ambaye hivi sasa hana uhakika na afya yake baada ya kulishwa sumu kwa dawa feki ambazo pia serikali haitakuwa tayari kuyaeleza madhara yake wazi ili kil mtu afahamu.

Zinduka mwananchi na ujuwe kudai haki yako bila kujali itikadi, dini, rangi au kabila, hili ni janga la kitaifa siyo chama au kikundi cha watu.Leo ni dawa kesho ni mchele, keshokutwa unga, dagaa, bia, maji n.k

Monday, 24 September 2012 20:11

aids-arvs-vidonge.jpg
ATAKA IJIHOJI IJE NA MAJIBU, AELEZA ATHARI ZAKE, NAIBU WAZIRI ATAKA IPEWE MUDA ZAIDI KUCHUNGUZA TATIZO
Elias Msuya
WAKATI utata ukiendelea kugubika usambazwaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), daktari katika Kitengo cha Ukimwi, Dar es Salaam ameitaka Serikali kujichunguza yenyewe, kwa kuwa dawa hizo hazisambazwi na watu binafsi.

Daktari huyo, Charles Lyimo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dawa katika Kitengo cha Ukimwi Hospitali ya Amana, alisema jana kuwa hakuna sababu ya kutafuta mchawi kwenye tatizo hilo; Serikali inahusika.

"Siyo rahisi kujua kwamba hii ni dawa halisi au bandia, lakini tuna uhakika na dawa tunazotumia kwa sababu zinaagizwa na Serikali peke yake. Hakuna mtu binafsi aliyepewa tenda (zabuni) ya kuziagiza," alisema Dk Lyimo.
Dk Lyimo alisema awali, dawa hizo zilikuwa zikiagizwa kutoka Marekani, lakini baadaye utaratibu huo ukabadilishwa na zikaanza kuagizwa kutoka India.

"…(Serikali) inapeleka oda kiwandani na ndiyo inayozigawa dawa hizo na kuzisambaza kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Lakini pia dawa hizi zinatengenezwa Arusha kwenye kiwanda kilichopewa kibali na Serikali," alisema Lyimo na kuongeza:

"Kama kuna dawa bandia, basi Serikali ijihoji. Kwanza mimi ninaposikia habari hizo huwa nacheka tu kwa sababu tangu sakata hili limeanza, wizara inajigongagonga tu… hawatuhusishi wala kutuuliza… na sisi tunaendelea tu kugawa dawa…"

Alipotakiwa kueleza tofauti iliyopo kati ya ARV zinazotengenezwa India na zile za Tanzania, Dk Lyimo alisema: "Ni sawa na dawa za kutuliza maumivu za Panadol na Asprin. Kuna wagonjwa wenye vidonda vya tumbo hawawezi kutumia Asprin, hawa wanatumia Panadol. Vivyo hivyo kwenye Ukimwi kuna wagonjwa ambao wanapata madhara wanapotumia dawa za India. Hawa sasa tunawapa dawa za Tanzania."

Dk Lyimo alisema mgonjwa anabadilishiwa ARV kulingana na jinsi zinavyompenda au kumdhuru na ikifikia hapo, mgonjwa huyo anahitaji uangalizi wa karibu wa daktari.

"Kuna dawa zinazonyonya damu, nyingine zinakula nyama na nyingine zinaleta maruweruwe na njozi mbaya. Kwa hiyo tukiona athari hizo tunambadilishia mgonjwa dawa hizo," alisema Dk Lyimo.
Akizungumzia madai hayo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alikiri kuwa ni Serikali pekee inayoagiza dawa hizo kwa ajili ya wananchi wake na akataka jamii ifahamu pia kuwa ni Serikali hiyohiyo iliyogundua tatizo hilo na kuanza kulifanyia kazi.

"Ni kweli Serikali pekee ndiyo inayoagiza dawa na Serikali hiyohiyo ndiyo iliyounda TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa), ambayo kwa kazi nzuri imefanikiwa kugundua kuwapo kwa dawa bandia. Kwa hiyo tuwape muda wa uchunguzi," alisema.

Hata hivyo, hakusema itaichukua TFDA muda gani kumaliza kazi hiyo akisema: "Hii ni kazi ya kitaalamu na inayohusisha mambo mengi. Siyo kwamba muda haujulikani, ripoti hiyo bado iko kwenye uchunguzi na uchunguzi unachukua muda mrefu… Tuwape muda wataalamu."

Hata hivyo, mmiliki wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPIL) kinachotengeneza dawa hizo, Zarina Madabida alikaririwa na gazeti hili jana akisema kuwa ndicho kilichogundua kuwapo kwa dawa hizo na kutoa taarifa kwa TFDA kikiomba iingilie kati ili kuondoa dawa hizo bandia kwenye mzunguko.

Athari za ARV bandia
Kuhusu athari za dawa bandia, Dk Lyimo alisema mgonjwa anayezitumia hana tofauti na mtu anayekula unga ambao kimsingi hauwezi kutibu maradhi.

"Dawa bandia siyo lazima iwe na madhara kwa mgonjwa. Cha msingi hapo ni kwamba mgonjwa anayetumia ARV bandia anakuwa tu hajatumia dawa kwa muda unaotakiwa," alisema na kuongeza:

"Mtu anaweza kutumia tu unga kutengeneza vidonge kisha akaweka nembo kwenye makopo na kuziuza kama ARV, hii ni kuwalaghai wagonjwa."

"Mtu asipotumia dawa, kama CD4 zake zilikuwa zimeongezeka hadi kufikia 500, hushuka tena na wale wadudu hupata nguvu ya kushambulia vile virutubisho vya seli. Kwanza wadudu wale huwa wajanja zaidi na wanaweza kujibadilisha kama kinyonga. Hivyo mgonjwa hurudiwa na magonjwa nyemelezi… ni hatari mno."

Dk Lyimo alisema kwa wastani hupokea kati ya wagonjwa 250 hadi 300 kwa siku hospitalini hapo na wote huja kuchukua dawa ili kuendelea na dozi zao. Alisema kutokana na usugu wa wadudu hao na tabia yao ya kubadilika badilika, dawa hizo ziko katika mchanganyiko wa makundi matatu yanayotosha kupambana nao.

"Kwa kawaida mwanadamu akiwa mzima ana CD4 1,500. Lakini akiathiriwa na Ukimwi zinapungua kwa sababu wale wadudu wanapoingia hushambulia virutubisho (membrane) na seli za kinga ndani ya damu.

"Hujipenyeza kwenye seli hizo na kujibadilisha na kufanana na seli hizo na huko ndiko wanakozaliana. Mtu anapotumia ARV, huvilewesha virusi na kuvifanya vishindwe kuzaliana, hivyo hula na vikishiba vinalala tu, lakini havifi," alisema.

Alisema kutokana na gharama kubwa ya dawa hizo, wagonjwa hushauriwa kutumia ARV wakiwa na CD4 350, hata hivyo, wapo wanaoshindwa kuvumilia hasa kutokana na kuandamwa na magonjwa nyemelezi hata wanapokuwa na CD4 600.
 
Kama serikali yenyewe ni feki na inaendesha nchi kwa sera feki kwanini ARVs zisiingizwe. Utakuta nyuma ya ujambazi huu kuna wakubwa wapenda pesa ambao wamegeuza nchi shamba la bibi.Fake ARVs hazina tofauti na bangi na unga unaowaingizia noble thieves wetu,
 
Tuwe makini kujifunza nano anafanya nini. Tfda haisimamii usambazaji, dawa zimesambazwa through msd... Hilo no bomu na kuna watu wa ccm wamo...
 
Tanzania haina hata kiwanda kimoja wala wasomi wa kutengeneza dawa za ARV wametambuaje kwamba hizo dawa ni feki? What I know is that tbs and the mkemia mkuu are not conversant with the ingredients of ARV. Au kwa kuwa zimetokea India na sio US. Tangu lini mtoto wa standard II aka-moderate mtihani wa form VI?
 
again, sidhani kama uko sahihi

tuna kiwanda kinatengeneza ARVs (suala la GMP compliance au hapana, hilo siwezi ku-comment)
wanaokagua na kuthibitisha ubora wa dawa ni TFDA (internally au kwa kushirikiana na quality control labs nyingine nje ya nchi)
tumeaminishwa hizi ni dawa feki (counterfeit), nijuavyo mimi si rahisi a counterfeit product kuingia kwenye public system if the manufactuer is the host country, most of counterfeits are "imported" and for a local product to filter into the national supply chain, it requires public procurement principles to be followed

hapo vidole vinaenda procurement, MSD, TFDA na local manufacturer
 
Kwa hali hii ya kuruhusu na kuachia dawa bandia ziingie nchini na kusababisha vifo na maafa kwa wananchi hawa mawaziri na kundi lake lazima wawajibishwe. Tukumbuke ni hivi karibuni ziliingizwa dawa za malaria fake na dawa nyingine nyingi. Rushwa uvivu na kutokupenda maisha ya wengine vinatuuwa sasa. Wito lazima wawajibike.

Daktari: Serikali inahusika ARV bandia Send to a friend
Monday, 24 September 2012 20:11

aids-arvs-vidonge.jpg
ATAKA IJIHOJI IJE NA MAJIBU, AELEZA ATHARI ZAKE, NAIBU WAZIRI ATAKA IPEWE MUDA ZAIDI KUCHUNGUZA TATIZO
Elias Msuya
WAKATI utata ukiendelea kugubika usambazwaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), daktari katika Kitengo cha Ukimwi, Dar es Salaam ameitaka Serikali kujichunguza yenyewe, kwa kuwa dawa hizo hazisambazwi na watu binafsi.

Daktari huyo, Charles Lyimo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dawa katika Kitengo cha Ukimwi Hospitali ya Amana, alisema jana kuwa hakuna sababu ya kutafuta mchawi kwenye tatizo hilo; Serikali inahusika.

“Siyo rahisi kujua kwamba hii ni dawa halisi au bandia, lakini tuna uhakika na dawa tunazotumia kwa sababu zinaagizwa na Serikali peke yake. Hakuna mtu binafsi aliyepewa tenda (zabuni) ya kuziagiza,” alisema Dk Lyimo.
Dk Lyimo alisema awali, dawa hizo zilikuwa zikiagizwa kutoka Marekani, lakini baadaye utaratibu huo ukabadilishwa na zikaanza kuagizwa kutoka India.

“…(Serikali) inapeleka oda kiwandani na ndiyo inayozigawa dawa hizo na kuzisambaza kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Lakini pia dawa hizi zinatengenezwa Arusha kwenye kiwanda kilichopewa kibali na Serikali,” alisema Lyimo na kuongeza:

“Kama kuna dawa bandia, basi Serikali ijihoji. Kwanza mimi ninaposikia habari hizo huwa nacheka tu kwa sababu tangu sakata hili limeanza, wizara inajigongagonga tu… hawatuhusishi wala kutuuliza… na sisi tunaendelea tu kugawa dawa…”

Alipotakiwa kueleza tofauti iliyopo kati ya ARV zinazotengenezwa India na zile za Tanzania, Dk Lyimo alisema: “Ni sawa na dawa za kutuliza maumivu za Panadol na Asprin. Kuna wagonjwa wenye vidonda vya tumbo hawawezi kutumia Asprin, hawa wanatumia Panadol. Vivyo hivyo kwenye Ukimwi kuna wagonjwa ambao wanapata madhara wanapotumia dawa za India. Hawa sasa tunawapa dawa za Tanzania.”

Dk Lyimo alisema mgonjwa anabadilishiwa ARV kulingana na jinsi zinavyompenda au kumdhuru na ikifikia hapo, mgonjwa huyo anahitaji uangalizi wa karibu wa daktari.

“Kuna dawa zinazonyonya damu, nyingine zinakula nyama na nyingine zinaleta maruweruwe na njozi mbaya. Kwa hiyo tukiona athari hizo tunambadilishia mgonjwa dawa hizo,” alisema Dk Lyimo.
Akizungumzia madai hayo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alikiri kuwa ni Serikali pekee inayoagiza dawa hizo kwa ajili ya wananchi wake na akataka jamii ifahamu pia kuwa ni Serikali hiyohiyo iliyogundua tatizo hilo na kuanza kulifanyia kazi.

“Ni kweli Serikali pekee ndiyo inayoagiza dawa na Serikali hiyohiyo ndiyo iliyounda TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa), ambayo kwa kazi nzuri imefanikiwa kugundua kuwapo kwa dawa bandia. Kwa hiyo tuwape muda wa uchunguzi,” alisema.

Hata hivyo, hakusema itaichukua TFDA muda gani kumaliza kazi hiyo akisema: “Hii ni kazi ya kitaalamu na inayohusisha mambo mengi. Siyo kwamba muda haujulikani, ripoti hiyo bado iko kwenye uchunguzi na uchunguzi unachukua muda mrefu… Tuwape muda wataalamu.”

Hata hivyo, mmiliki wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPIL) kinachotengeneza dawa hizo, Zarina Madabida alikaririwa na gazeti hili jana akisema kuwa ndicho kilichogundua kuwapo kwa dawa hizo na kutoa taarifa kwa TFDA kikiomba iingilie kati ili kuondoa dawa hizo bandia kwenye mzunguko.

Athari za ARV bandia
Kuhusu athari za dawa bandia, Dk Lyimo alisema mgonjwa anayezitumia hana tofauti na mtu anayekula unga ambao kimsingi hauwezi kutibu maradhi.

“Dawa bandia siyo lazima iwe na madhara kwa mgonjwa. Cha msingi hapo ni kwamba mgonjwa anayetumia ARV bandia anakuwa tu hajatumia dawa kwa muda unaotakiwa,” alisema na kuongeza:

“Mtu anaweza kutumia tu unga kutengeneza vidonge kisha akaweka nembo kwenye makopo na kuziuza kama ARV, hii ni kuwalaghai wagonjwa.”

“Mtu asipotumia dawa, kama CD4 zake zilikuwa zimeongezeka hadi kufikia 500, hushuka tena na wale wadudu hupata nguvu ya kushambulia vile virutubisho vya seli. Kwanza wadudu wale huwa wajanja zaidi na wanaweza kujibadilisha kama kinyonga. Hivyo mgonjwa hurudiwa na magonjwa nyemelezi… ni hatari mno.”

Dk Lyimo alisema kwa wastani hupokea kati ya wagonjwa 250 hadi 300 kwa siku hospitalini hapo na wote huja kuchukua dawa ili kuendelea na dozi zao. Alisema kutokana na usugu wa wadudu hao na tabia yao ya kubadilika badilika, dawa hizo ziko katika mchanganyiko wa makundi matatu yanayotosha kupambana nao.

“Kwa kawaida mwanadamu akiwa mzima ana CD4 1,500. Lakini akiathiriwa na Ukimwi zinapungua kwa sababu wale wadudu wanapoingia hushambulia virutubisho (membrane) na seli za kinga ndani ya damu.

“Hujipenyeza kwenye seli hizo na kujibadilisha na kufanana na seli hizo na huko ndiko wanakozaliana. Mtu anapotumia ARV, huvilewesha virusi na kuvifanya vishindwe kuzaliana, hivyo hula na vikishiba vinalala tu, lakini havifi,” alisema.

Alisema kutokana na gharama kubwa ya dawa hizo, wagonjwa hushauriwa kutumia ARV wakiwa na CD4 350, hata hivyo, wapo wanaoshindwa kuvumilia hasa kutokana na kuandamwa na magonjwa nyemelezi hata wanapokuwa na CD4 600.
 
Wapi kwa kujiuzuru!?? Tanzania ya leo!? so far to resign is unTanzanian!
 
Tuwe makini kujifunza nano anafanya nini. Tfda haisimamii usambazaji, dawa zimesambazwa through msd... Hilo no bomu na kuna watu wa ccm wamo...

Ni vyema ukafuatilia suala hili vizuri, medical store department yes, lakini kabla dawa hazijaingizwa ndani ya nchi ni lazima TFDA waidhinishe ubora wa dawa au chakula kwa maisha ya binadamu. Suala la usambazaji ni lingine kwa kuwa tayari zipo ndani ya nchi. Hata kama zimezalishwa ndani ya nchi bado TFDA bado wanarole ya ku-play usiwatete hapa. Narudia hapa hakana upelelezi unaohitajika zaidi ya watu kuwajibika kwa kuwa kila kitu kiko wazi hizi dawa hazikushuka kutoka juu bali zilipokelewa kutoka taasisi moja kwenda nyingine kwa utaratibu maalum na unaoeleweka.
 
Kama serikali yenyewe ni feki na inaendesha nchi kwa sera feki kwanini ARVs zisiingizwe. Utakuta nyuma ya ujambazi huu kuna wakubwa wapenda pesa ambao wamegeuza nchi shamba la bibi.Fake ARVs hazina tofauti na bangi na unga unaowaingizia noble thieves wetu,
we are not serious kam nchi.
tungelikuwa angalau mpaka sasa mtu mmoja (aliyekamatwa nazo) angelikuwa anashikiliwa na vyomba vya dola.
...lakini kama suala la mwandishi wa habari Mwangosi lililokuwa wazi na ushahidi hadi wa video na sauti upo linaundiwa tume na kamati, unadhani kuna mwenye ubavu miongoni mwao kupeleleza au kufuatilia suala kama hili!?

Ni vyema ukafuatilia suala hili vizuri, medical store department yes, lakini kabla dawa hazijaingizwa ndani ya nchi ni lazima TFDA waidhinishe ubora wa dawa au chakula kwa maisha ya binadamu. Suala la usambazaji ni lingine kwa kuwa tayari zipo ndani ya nchi. Hata kama zimezalishwa ndani ya nchi bado TFDA bado wanarole ya ku-play usiwatete hapa. Narudia hapa hakana upelelezi unaohitajika zaidi ya watu kuwajibika kwa kuwa kila kitu kiko wazi hizi dawa hazikushuka kutoka juu bali zilipokelewa kutoka taasisi moja kwenda nyingine kwa utaratibu maalum na unaoeleweka.

Kweli unategemea kuna atakaye wajibika hapa? Tusubiri tuone!
 
we are not serious kam nchi.
tungelikuwa angalau mpaka sasa mtu mmoja (aliyekamatwa nazo) angelikuwa anashikiliwa na vyomba vya dola.
...lakini kama suala la mwandishi wa habari Mwangosi lililokuwa wazi na ushahidi hadi wa video na sauti upo linaundiwa tume na kamati, unadhani kuna mwenye ubavu miongoni mwao kupeleleza au kufuatilia suala kama hili!?

Watanzania tuna shida ! Sijui lini tutafika .
 
Nakumbuka nilileta thread hapa inayohusu matumizi ya ARV na madhara yake nikaonekana mkatili lakini leo ukweli umejulikana. Kuna siri kubwa imejificha nyuma ya ARV na matokeo yake watu watakuja kujua wakati imeshakuwa too late
 
Zinatengenezwa na moja ya viwanda vya::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
 
Mkuu huo msamiati wa kujiuzulu hapa kwetu aupo.......:yo:hapa ni mwendo wa kufunika kombe tu
 
Tuwe makini kujifunza nano anafanya nini. Tfda haisimamii usambazaji, dawa zimesambazwa through msd... Hilo no bomu na kuna watu wa ccm wamo...

lakini MSD hawezi kupima na kujua ufake wao si wanasambaza.
Kwani hawa TFDA wanajukumu gani kama sio kuhakikisha hatutumii vyakura au madawa fake?
 
Back
Top Bottom