Wizara ya afya bado wiki mbili

MITOCHONDRIA

Senior Member
Feb 21, 2013
147
34
ZIKIWA ZIMESALIA WIKI MMBILI KUFIKA TAREHE 25 JUNE, IKIWA NI TAREHE ILIYOWEKWA NA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KATIKA TANGAZO LAKE LA KAZI KWA WATUMISHI WA KADA ZA AFYA, BADO MAJINA HAYO HAYAJATOLEWA, KWA MTAZAMO WANGU NILITEGEMEA MAJINA NA SEHEMU WALIZOPANGIWA YANGETOKA MWANZONI MWA MWEZI JUNE, ILI KUTOA NAFASI KWA WATU KUJIANDAA.LAKINI MPAKA LEO TAREHE 04 JUNE BADO. JE MUDA HUO UMEONGEZWA? AU WATU WATASHITUKIZWA TU.



REJEA TANGAZO LENYEWE HAPA CHINI.

KWA HESHIMA NA TAAZIMA NAOMBA KUWAKILISHA.

SENT BY MITOCHONDRIA










JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TANGAZO LA KAZI
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa wote wenye taaluma za Kada za Afya ambao wako tayari kufanya kazi katika Utumishi wa Umma.
Vigezo na Masharti:
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Watumishi wa Kada za Afya waliojiendeleza wakiwa kazini wasitume maombi bali waombe kwa waajiri wao kubadilishwa vyeo kulingana na sifa walizopata.
4. Watumishi ambao walikwishapangiwa vituo vya kazi miaka ya nyuma na hawakuripoti au kuacha kazi hawatapangiwa vituo vya kazi, kwa sababu hawataweza kuingia kwenye ‘Payroll’ ya Serikali.
5. Maombi yote yaambatanishwe na:- Nakala ya Cheti cha Taaluma, Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita, Maelezo binafsi (CV), Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni, Nakala ya cheti cha usajili.
6. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au Wakili anayetambuliwa na Serikali.
7. Waombaji wanatakiwa kuchagua/kupendekeza maeneo matatu (Mikoa na Halmashauri) ambayo wangependa kupangiwa kazi kwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa kwenye Kibali (Tazama Tovuti ya Wizara).
2
Waajiri wote wanatakiwa kuharakisha zoezi la kuwaajiri na kuwaingiza kwenye ‘Payroll’ ya Serikali wataalam wote watakaopangiwa vituo vya kazi kwenye mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kujikimu kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima watumishi husika.
Aidha, Waajiri wanakumbushwa kukagua na kuthibitisha uhalali wa vyeti vya kidato cha Nne na Sita vya wataalam hao kabla ya kuwaajiri.
Kwa utaratibu wa mwaka huu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hatatoa barua za kupangiwa Vituo vya kazi. Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Ministry of Health and Social Welfare). Ukiona jina lako kwenye Tovuti au Gazeti nenda karipoti kwenye kituo ulichopangiwa kabla ya tarehe 25 Juni, 2013 ambako taratibu za ajira yako zitakamilishwa.
Maombi yote yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Mei, 2013.
Tangazo hili pamoja na mchanganuo wa nafasi za kazi vinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Ministry of Health and Social Welfare)
 
Back
Top Bottom