Wizara aliyopewa Mwakyembe

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
NAZIR KARAMAGI USO KWA USO NA DR MWAKYEMBE:

RIPOTI YA KIUCHUNGUZI YA KAMATI TEULE YA DR HARRISON GEORGE MWAKYEMBE NDIO ILIYOPELEKEA KUVUNJIKA KWA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUJIUZULU KWA LOWASSA.MIONGONI MWA MAWZIRI WALIOJIUZULU ALIKUWA NAZIR KARAMAGI AMBAYE ANAHUSISHWA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA KUPAKUA MAKONTENA BANDARI YA TICTS.JE,

1.KIKWETE AMESAHAU UGOMVI WA MWAKYEMBE NA KARAMAGI?
2.AU MWAKYEMBE AMEPELEKWA KWA KAZI MAALUM?
3.JE,MADUDU YA TICS YAMEISHA?
4.JE NI MKAKATI MAALUM WA KUFUKUA MADUDU HATA YALE YA ATC YA WAKINA CHENGE AMBAO WOTE NI MAADUI WA KUNDI LA MWAKYEMBE?

UPO WAPI USALAMA WA MWAKYEMBE KWENDA WIZARA AMBAYO INA MADUDU NA ILIWAHI KUKALIWA NA WABAYA WAKE WA KISIASA NA HATA WENGINE KUWA NA HISA KWENYE VITENGO NDANI YA HIYO WIZARA?

au kuna bomu kategewa huko limlipukie?
 
Mtakatifu hiyo ni TICTS, siyo TICS. Tanzania International Container Terminal Services ltd. Nipe ahsante yangu.

Asante ndugu yangu hizi haraka haraka hizi mkuu wangu ngoja nirekebishe, na hizi chemba zao zimekuwa nyingi mkuu wangu kuzijua zote vizuri inakuwa ni issue
 
Funika kombe mwana haramu karamagi apite, by JK...
 
mmmhhh yetu macho but am happy for the guy ameteseka sana kwa kuwekewa sumu bt he never gave up ameendelea kufanya kazi japokua afya yake haikua nzuri na Mzee amem reward kwa kumpa uwaziri sasa asiogope kitu wembe ni ule ule ka kuna madili ya uchafu ya viongozi wengine huko akayesimamishe yote na kuyatupilia mbali...watu kama akina mwakyembe ndio wanaweza kuisaidia ccm 2015
 
IVUGA

Mwakyembe anahitaji usalama gani tena wakati yeye mwenyewe alishasema ule mwili unaharibika kwa sumu aliyopewa??
 
Hiyo nayo ni hoja Mkuu Saint Ivuga!

Nakumbuka hili suala la TICTS, liliishia kwa zengwe tu tukaambiwa lipo kwenye baraza la mawaziri hivyo umma usipige kelele...
Labda JK kasahau? Labda ni kisa cha nani amvishe paka kengere?? Labda JK amemu-underestimate Mwakyembe??

Ila binafsi bandarini sina kwere napo sana, naona kama urekebishaji wake upo dhahiri sana.
Ngoma ngumu ni ATC, TAZARA na TRC....
Hapo ndio masikio yangu nimetega sana!
 
Last edited by a moderator:

jouneGwaluMkuu hawa watu hawaeleweki kabisa,Kama uadui ungekwepo basi wakati ule iliposemekana amewekewa
sumu basi angesema ukweli halisi,kama wakati ule aliogopa we unadhani ataweza kuchimbua madudu hayo?
Ila kwa upande mwingine nimeona kama kambi moja unaongezewa nguvu na lingine linadhoofishwa.
 
Last edited by a moderator:
jouneGwaluMkuu
hawa watu hawaeleweki kabisa,Kama uadui ungekwepo basi wakati ule
iliposemekana amewekewa
sumu basi angesema ukweli halisi,kama wakati ule aliogopa we unadhani
ataweza kuchimbua madudu hayo?
Ila kwa upande mwingine nimeona kama kambi moja unaongezewa nguvu na
lingine linadhoofishwa.

na background yake ya sheria tusitarjie tena mikataba tata bandari, atc, trl, etc!
 
Last edited by a moderator:
Na ule msuguano uliokuwepo kati na Nundu vs Mfutakamba, huku nyuma ya pazia kukielezewa kuwapapo na Rostam Aziz nyuma ya kampuni ya kichina iliyokuwa ikipigiwa bede na Mfutakamba, huku Serukamba akielezwa kutumika na Rostam hatma yake itakuwaje?. Ila Mwakyembe mimi binafsi namkubali ni mbishi asiyependa kuyumishwa hovyo lazima patachimbika kwanza tusuburi picha harisi.
 
But usitegemee jipya sana atakalofanya kwani anaapa kwa anayeyajua madudu yaliyofanyika wakati wake, SIASA ni komedi wacha tuendelee kushangilia SIMBA tu
 
jouneGwaluMkuu hawa watu hawaeleweki kabisa,Kama uadui ungekwepo basi wakati ule iliposemekana amewekewa
sumu basi angesema ukweli halisi,kama wakati ule aliogopa we unadhani ataweza kuchimbua madudu hayo?
Ila kwa upande mwingine nimeona kama kambi moja unaongezewa nguvu na lingine linadhoofishwa.
kweli hapaa no jipya at all.
 
Asante ndugu yangu hizi haraka haraka hizi mkuu wangu ngoja nirekebishe, na hizi chemba zao zimekuwa nyingi mkuu wangu kuzijua zote vizuri inakuwa ni issue

Haraka haraka nani alikua anakukimbiza?au na wewe ni moja wa wale malimbukeni wa hapa jf kujifanya wao ndo wakwanza ku post kitu,mambo hata hayajakamilika mtu ameshapost kitu ukifungua post hakuna kitu
 
Mtakatifu hiyo ni TICTS, siyo TICS. Tanzania International Container Terminal Services ltd. Nipe ahsante yangu.
Unajuwa huyu jamaa tangu aanze kujiita Saint Ivuga na kubadili ile Avatar yake yake ya Simba Sc, naona kama kama hii ID amemkabidhi mtu mwingine, si yule ambaye nilikuwa namjuwa kama Ivuga teja la JF. Ila leo naona amekuja kivingine kama wakati ule.
 
Of all the people namuonea huruma Mgimwa maana kapewa usukani wakati meli ndo inazama.
Mwakyembe nae kapewa mfupa kiaina ili awe busy na migogoro na makarabrasha.
Ila hawa wote wamtangulize mola atawaongoza salama
 
Back
Top Bottom