Wivu!!

Babu heshima kwako
Ulipata divisheni ngapi?

Mhhh CPU,

Nikitaja division itabidi pia niweke na point...DC huwa hapendi kufanya kazi ya comedy...Nadhani inatosha kujua kuwa tulipita vizuri kwenye mitihani na labda ndo maana tunaweza kudonoa hizi key boards!
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Dah, Wivu sio mzuri!!!
Lakini mi nina wivu sijui!!!
Hebu ngoja nijikague aisee!!!

Halafu weee LD, nina kesi na wewe, tena bab kubwa! Ngoja nikatafute judge ila si wale wazee wa Infi....LoL!!!!

Sasa unamwonea wivu nani? Shoga yako anayetesa na Spacio au? Kama ni wivu wa namna hiyo basi kawahi kikombe Loliondo kwa sababu huyo ni pepo!! Ila kama unalinda mali zako au unataka kuvuta mchuma mwakani basi hayo ni maendeleo na Mzee mstaafu DC anakutakia kila la heri,

Mzee DC!
 
hapo nadhan msaada ni kukuzawadia na ww uwe na mtoto mzuri km wa huyo dada.

Kuna mambo mengine siyo ya kuhangaika nayo! Hakuna sababu ya kusumbua kichwa chako kwa vitu ambavyo unajua ni impossible! Ni kujitafutia depression bure. Kwa nini mtu usihangaike kufanya yale ambayo yako kwenye uwezo wako?
 
Mmh Mzee DC kupata mtoto mzuri siyo ndani ya uwezo wetu?
 
Dear Lizzy

kuwa na wivu ni sawa kuna wimbo wa zamani unasema
BILA WIVU ATAJUAJE KWAMBA NAMPENDA lakini wivu unapozidi duu kero
kwa upande wa ndugu/marafiki kuwa na wivu wa maendeleo ni wachache
mara nyingi wanakuwa na wivu wa kwanini
 
Halafu weee LD, nina kesi na wewe, tena bab kubwa! Ngoja nikatafute judge ila si wale wazee wa Infi....LoL!!!!

Sasa unamwonea wivu nani? Shoga yako anayetesa na Spacio au? Kama ni wivu wa namna hiyo basi kawahi kikombe Loliondo kwa sababu huyo ni pepo!! Ila kama unalinda mali zako au unataka kuvuta mchuma mwakani basi hayo ni maendeleo na Mzee mstaafu DC anakutakia kila la heri,

Mzee DC!

Babu ngoja nitoke hapo nje kwanza,
Tumalize hii kesi, ndo mambo mengine yaendelee.
Dah ile namba yako niliificha wapi tena sijui???
Hebu ngoja nikaitafute....
Babu hebu pata kikombe cha chai kwanza hapa.
 
Dear Lizzy

kuwa na wivu ni sawa kuna wimbo wa zamani unasema
BILA WIVU ATAJUAJE KWAMBA NAMPENDA lakini wivu unapozidi duu kero
kwa upande wa ndugu/marafiki kuwa na wivu wa maendeleo ni wachache
mara nyingi wanakuwa na wivu wa kwanini

Sasa huo wa kwanini ndo inabidi tuondakane nao BW!
 
Goodmorning dear!Hehehe...sio mbaya ila tu usije ukafikia kumchukia dada wa watu na katoto kake usije ukakaharibu sura bure. Maana ukizidi unaweza ukaanza kuona kama huyo dada anaringa kwaajili ya uzuri wa mtoto wake hata kama sio kweli...na njia pekee kumkomoa ni kuchakachua uzuri wa mtoto!
badala ya kuniambia nizae kitoto changu unazungushazungusha maneno.
 
Hehehe ningeweza kukwambia hivyo ila kasipokua kacute kama dada wa watu utaongeza wivu then chuki!
natafuta mwanaume handsome wa ukweli.Unajua uongo mbaya handsome atanihakikishia kufyatua katito cute.
 
Hivi hujawahi kusikia wivu mama yako mzazi anaitwa mama fulani yaani jina la dada yako au kaka ukaanza kujisikia mnyonge na kutamani aitwe mama shantel, hamuwezi amini hii ilinitesa sana utotoni hadi kukonda ila sasa hivi nikifikiria huwa nacheka na wala sijawahi kumwambia mama wala ndugu zangu. kwa hiyo wivu ni kwa wote hadi watoto nao wanasikiaga wivu
 
natafuta mwanaume handsome wa ukweli.Unajua uongo mbaya handsome atanihakikishia kufyatua katito cute.

Hahahaha Marytina usishawishike tu kumsaliti morani wetu.Alafu kumbuka na wewe unachangia...mwenzako anaweza asiwe muuza sura sana ila ukapata kacute balaa kama mwenyewe unalipa!
 
mie nina ndugu wa damu kabisa lakini hatuelewani kwa sababu ya huo wivu wa kwanini mwishowe niliamua kujiweka pembeni
kuepusha migogoro ya kifamilia
Ulitumia busara kweli BW...ndugu wa aina hiyo wanaweza kusababisha mtafaruku wa ajabu!
 
Back
Top Bottom