Wivu!!

Wivu, wivu wivu aaah, Gari nzuri kuliko ya Boss wako, inakuwa ishu....... asante Lizzy.
 
Wivu, wivu wivu aaah, Gari nzuri kuliko ya Boss wako, inakuwa ishu....... asante Lizzy.

Hehehe!Elia sasa bosi akikuonea wivu hapo kuna hatari maana anaweza hata kukufukuza kazi akiweza!Au mwalimu kwa mwanafunzi...ni mwendo wa kufelishana tu kwenye shule zetu hizi!
 
Pole sana. Kuna jamaa tulikuwa naye O-level, yeye alikuwa ni mkali saaana ila alikuwa hataki kutufundisha. Tulimkalia tukamtukana hadi akabadilika. Tulimweleza kuwa yeye akipata A na mimi nikapata F hawezi kufaidi lolote. Ila akitumia nguvu kidogo wakati anafanya mazoezi yake ya kawaida akatusaidia kupata B itakuwa bora kwetu na hatapungukiwa kitu. Huwezi kuamini, timu yetu sote tulifaulu vizuri.

Ila watu wengi huwa tunafikiria kwamba tukiwasaidia wenzetu basi tunapoteza. Ni upuuzi wa hali ya juu. Kama mtu ameumbwa kukupita basi atakupita tu, hata kama hutamsaidia!

Babu heshima kwako
Ulipata divisheni ngapi?
 
Kwenye mapenzi: Wivu kati ya wawili ndani ya mahusiano unaweza kua kirutubisho au chachu ya mapenzi.Ukionyesha kwa kiasi utamfanya mwenzi wako ahisi kwamba unampenda na kumjali...sisemi kwamba ni kitu pekee kinachofanya hivyo bali ni kichocheo kizuri iwapo hakitazidishwa na kusababisha kero.Wivu unapozidi unaonyesha mapungufu yako kanakwamba hujiamini kitu ambacho kinaweza kupelekea mwenzako nae ahisi kwamba HUMUAMINI.

Dear Lizzy, kwa kadiri nilivyoifahamu hii mada, kuna wivu wa aina mbili - wivu mzuri na wivu mbaya. Wivu mzuri ni ule unaokusukuma kufikia hatua aliyofikia mwenzako, mbaya ni ule wa husuda na chuki ambao matokeo yake mwenye wivu huwacha kujiendeleza na kubakia kuumia roho, kupika fitina na kumwaga majungu.

Lakini bado siuelewi huu wivu wa mapenzi/kwa mpenzi wako. Ni nini hasa? Kuuliza uliza "umeenda wapi?", "kwa nini umechelewa kurudi?", ulikuwa unazungumza na nani?", kutaka kujua ameenda wapi na nani", "kupekua mikoba na mifuko ya suruali", "kusoma sms na msgs kwnye simu na internet", "Sitaki uzungumze, uwe na urafiki na fulani" n.k. Ikiwa ni moja, baadhi au yote katika haya hatuoni kuwa ni kero? Ni aina gani ya matendo ya wivu "mzuri" baina ya wapenzi ambayo yatazidisha mapenzi badala ya kuwa kero?
 
MammaMia vyote ulivyotaja hapo ndio kero zenyewe.Mambo yakulindana kama wafungwa sio kabisa.Wivu mzuri ni ule unaokuwezesha kumwambia mwenzako au hata kufikiri tu kwamba siku akikusaliti utaumia na sio kumpekua pekua..wivu unaokufanya ujitahidi kumtendea mema ili asije akawa impressed na mtu mwingine kwa mambo ambayo unapenda atake/afurahie kutoka kwako tu..wivu unaokufanya utamani kua bora kuliko wote kwake.Wivu mzuri ni ule unaokusukuma kufanya mambo yatakayo mfanya asitake kukuacha!
 
Mi mbona nishamuova teki zamaaaaani.
Imagine hata akisalimiana na mama ake kwa kukumbatiana namfokea
Hehehehe...hubby anataka mikono ya wifey imhusu yeye tu na kifua chake kimguse yeye tu.Ndo maana na kupenda..na wivu wako unaniongezea raha!
 
Dah, Wivu sio mzuri!!!
Lakini mi nina wivu sijui!!!
Hebu ngoja nijikague aisee!!!
 
Back
Top Bottom