U a wrong Lizzy. Jamaa yuko Kitaa na anafanya biashara ya Hardware mitaa ya Kariakoo. Hajawahi hata kukamatwa kwa kosa hilo. Kitu pekee ninachokijua aliubeba mzigo wa matibabu ya mkewe hadi mwisho. Kuanzia Malago Hospitali Kuu ya Uganda hadi Kwa T.B. Joshua gharama zote hizo pamoja na zile za Blood Detoxification (280,000 Kwa wiki) jamaa alizibeba yeye. Hapo katikati alizaa mtoto na mwanamke mwingine!!
Mikono ya sheria haikuwahi kumfikia!!
mwanzoni alidhani atapona haraka na kurudia maisha yake ya zamani. Lakini baada ya juhudi zote za kumtibia wakiwa wanaishi Bukoba kushindikana na kupelekwa Uganda kwa matibabu. Hatimaye naona akakubali "kumsamehe" mumewe na kukubali kuishi kama alivyo. Shida ilikuja pale ilipogundulika kwamba damu yake imechafuliwa sana na madawa.Basi pengine mke wake hakuona haja ya kumshtaki au walikubaliana anyamaze apate msaada.
Ni kisa cha kweli kabisa kilichomtokea mtu ninayemfahamu kwa miaka mingi sana. Msiba uko Kijitonyama nyumbani kwake. Nimetumia neno "dada" kwa sababu nilimheshimu hivyo siku zote na yeye alinichukulia hivyo hivyo kuwa ni kaka yake. Ameacha watoto wawili wa kiume mmoja yuko Chuo Kikuu na mwingine anatarajia kusomea Comm. Dev pale kijitonyama.
Hakuna alichofanywa kwani wanandugu waliona kwamba jamaa "kajutia" alichokifanya!! Flora ndiye alionyesha moyo wa kishujaa kabisa kwani pamoja na kuwa na hali dhaifu kwa miaka yote alikuwa anajitahidi kusimamia maisha yake na ya familia yake!Huyo mumewe alichukuliwa hatua gani?