wivu sina ila roho inauma

VAMPA

Member
Dec 19, 2011
61
4
wana jamvi habari za jioni? nimekuwa na jirani yangu mdada ambaye tumekuwa marafiki sana. ninamheshim mme wake na rafiki zake wengine wa kiume na yy anamfaham mpenzi wangu, lakini roho imeniuma sana aliponiambia kuwa anaanza mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. sijui kwa nini, nisaidieni wana jamvi.
 
Kama umejishtukia maana yake kuna kitu hapo. Au roho imekuuma kuona rafiki yako sio muaminifu?
 
Kama umejishtukia maana yake kuna kitu hapo. Au roho imekuuma kuona rafiki yako sio muaminifu?

mkuu siju kwanini, huyu binti ana mme kama nyumba ndogo na mahawara wengi na wote nawajua na huwa ananiambi wakati anatoka nao, lakini nashangaa kwa huyu mpya mmhhh roho inauma.
 
labda unajua huyo shem mpya jinsi alivyo mbovu,na unamuonea huruma huyo dada kuwa she is making a mistake.....
 
mkuu siju kwanini, huyu binti ana mme kama nyumba ndogo na mahawara wengi na wote nawajua na huwa ananiambi wakati anatoka nao, lakini nashangaa kwa huyu mpya mmhhh roho inauma.
Labda umegundua kua huyu wa sasa hivi anampenda kweli na unaona kama nafasi yako kama rafiki yake mpenzi ipo mashakani...
 
Ushamtamani,acha uzinzi wewe

huenda kabaka unaweza kuwa umenipa jibu kuwa namtamani,ila mkuu huyu binti tunashirikiana kilakitu kasoro tu kila mtu anachumba chake. namchukulia kama dada yangu na nina mpenzi wangu. sijui sasa kwa nini roho iume.
 
ni kweli huyu binti ni mkarim sana ananijali na anawajali sana hata rafiki zangu. nami namjali na ninawajali shemeji zangu wote aliyo nitambulisha. pia huwa napata amani na furaha saana akiwa anafurahi, huwa napenda afurahi muda wote, tunasaidiana kwa mengi, hata akiwa amekosana na bwana ake huwa tunashauriana jinsi ya kusolve tatizo. sikuwa na wivu wowote hapo awali hatakama najua kuwa yuko anafanya mapenzi na mtu yoyote yule, kinacho nishangaza ni huyu mpya du roho inauma utadhani ni mpenzi wangu.
 
mkuu siju kwanini, huyu binti ana mme kama nyumba ndogo na mahawara wengi na wote nawajua na huwa ananiambi wakati anatoka nao, lakini nashangaa kwa huyu mpya mmhhh roho inauma.

sasa nyumba ndogo ni mume?.nawe huyo mpenzi wako mbona unashindwa kumwita mke?, unashusha hadhi ya mume, huyo bibie ni nyumba ndogo, sema anampangaji ambaye wewe unamfahamu, siyo mume. hii post angesoma mpenzi wako ataona humpendi wewe, yaani unashindwa kumwita mpenzi wako mke, ukaenda kukiita kidumu cha mtu mume?
 
ni kweli huyu binti ni mkarim sana ananijali na anawajali sana hata rafiki zangu. nami namjali na ninawajali shemeji zangu wote aliyo nitambulisha. pia huwa napata amani na furaha saana akiwa anafurahi, huwa napenda afurahi muda wote, tunasaidiana kwa mengi, hata akiwa amekosana na bwana ake huwa tunashauriana jinsi ya kusolve tatizo. sikuwa na wivu wowote hapo awali hatakama najua kuwa yuko anafanya mapenzi na mtu yoyote yule, kinacho nishangaza ni huyu mpya du roho inauma utadhani ni mpenzi wangu.
Hapo mwanzo ulimkuta tayari anahusiana na watu fulani, hunge weza kuwachukia maana wewe ndio uliwakuta. ulipo jenga urafiki nae na kua karibu nae ulijikuta unampenda(kimapenzi au kindugu, unajua mwenyewe) na ukaamini kua atawaacha hao wengine wote pole pole hadi arudi kwenye mstari. Sasa amekuonesha mpenzi mpya alie anzana nae baada ya uhusiano wenu, na umegundua kua ukaribu wenu haumziwii kuendelea na biashara yake. Mbaya zaidi umegundua kua yuko karibu sana na huyu wa mwisho. Ndio maana ya roho kukuuma.
 
"Sina wivu lakini roho inaniuma".
"Sina wehu lakini nina wazimu".
Vipengere hivyo vya WIVU na KUUMWA ROHO vikishakua vimelenga Mwanamke toka kwa Mwanaume ama vikitoka kwa Mwanaume kwenda kwa Mwanamke inakua ni WIVU tu! ukikubali usikubali ndiyo hivyo.
 
Duh, dunia ina mambo!
Kila siku nasema ' mbwa akichezea kingozi anachokilalia sana mwishowe hukila'

unataka kula kingozi chako cha kulalia?!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom