Wito: Tufunge na Kuiombea Nchi Ijumaa Hii

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wapendwa Wana JF, Watanzania na wote wenye Mapenzi mema na Nchi yetu.

Nasukumwa kuwaomba kuwa Ijumaa hii tarehe 17 Oktoba 2008 tujitolee kufunga na kuiombea nchi yetu ya Tanzania.

Wataoweza kufunga kwa kutoonja chochote, watakao kunywa maji tu na kuacha kula, wataoshindwa kufunga; wote kwa umoja naomba tukubaliana kuliombea Taifa letu siku hiyo kama ifuatavyo:

MUDA WA MAOMBI: Saa 7.15 hadi saa 7.45 Mchana

MAHALI: Popote utakapokuwepo, ikifika saa hiyo tuanze kuiombea nchi yetu.

MAMBO YA KUOMBEA:
1. Kumwoba Mungu awape hekima kwa Rais, Bunge, na viongozi wote wa Nchi hii
2. Kumwomba Mungu ampe ujasiri Rais na Viongozi wenzake wenye mapenzi mema ili wapambane bila woga dhidi ya roho za Ufisadi.
3. Kumwomba Mungu atuepushe na vita vya wenyewe kwa wenyewe
4. Kuziharibu roho zote za Ufisadi, hujuma, ubadhirifu na wizi dhidi ya Maliasili za Tanzania na mali zote za Umma.
5. Tuvunje roho zote za kutokutenda haki katika Taifa na kuombea vyombo vya Sheria na Mahakama ili viweze kusimamia haki.

Naamini tukifanya haya, hata milima tunayodhani haihamishiki itatupwa baharini.

Yesu aliwaambia Wanafunzi wake "Namna hii, haiwezekani ila kwa kufunga na kuomba" Matthew 17:14-21

Asanteni.
 
Last edited by a moderator:

Asante kwa Ufunuo Mpendwa, Stay blessed.
 
Hakuna lisilo wezekana kwa Mwenyezi Mungu, nami ninaahidi kufunga. yaliyotokea Tarime ya kupigana mapanga, tuyakemee yasitokee tena hapa nchini kwetu. Iwe ni mwisho.

Pia roho za kifisadi, unyanyasaji, ukandamizaji, nk zitoweke
 
Back
Top Bottom