Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010

Wakati mwingine jukwaa hili linakuwa kama klabu cha pombe! analysis zingine zinazotolewa hapa ni tepe tepe sana,kwa mfano si lazima iwe ccm au chama kingine chochote rais ajaye lazima akubalike zanzibar! vigezo vya hivi haviwezi kutupa rais bora! anayechaguliwa na rais wa jamhuri ya tanzania!

Pengine kubwa la kutizama na linalotuunganisha watanzania wote ni kama candidate anaiweza kazi! kwa maana ya uzoefu,uaminifu,hekima,ujuzi,uthabiti nk, bahati mbaya sana watanzania wengi wanaochangia hapajf wanaiona kazi hii kama rahisi tu!!! ndio maana wanasikika wengine wakisema aje kijana next time!

Lakini ukweli kabisa kwa sasa hakuna kijana iwe kwa wale walio ktk uongozi sasa au walio nje anaweza kuwa rais mzr wa tz! pengine wengi wanavutwa kwa kutaka kuiga tu, kutaka nchi zingine zenye marais vijana.kwa tz ni vigumu!kwa sababu structuire ya malezi katika familia zetu ni mbovu kabisa siku hizi!!! hazimjengi mtoto au kijana kuwa kiongozi mzuri!! zinamjenga kuwa mbinafsi,mpenda anasa,mchoyo,mbaguzi,mnafiki nk. kwa maana hiyo bado tunahitaji sana kuwa na vongozi wa umri kama wa salim,shein,mwandosya,sitta, nk kwenye nafasi ya urais na makamu ili kutunza tunu za taifa letu,AMANI,UTULIVU,KUHESHIMIANA,UPENDO nk.

Mifano ipo mingi lakin ni vzr tunapojadili watz wanaoweza kufanya hii kazi tuongozwe na sifa ya UWEZO na siyo kutanguliza uwepo wa mizengwe au cjui mtandao hiyo ni fanatism tu haina nguvu sasa hivi,lkn mwisho kabisa yupo mwenyezi Mungu nayye ana hesabu zake! our choise is not ABSOLUTE!! it can be changed!!

Mkuu umechemsha ukweli ni huo uloelezwa na haupingiki makundi yapo, CCM Znz wanampiga vita SAS nk, sasa wewe unaleta picha ya nchi ilo na raia wanaijua demokrasia na ambayo haiendeshwi kwa mizengwe.
 
nasikia yale yaliyosemwa yalikuwa kweli,kama tz tayari tumeuza loliondo kwa waarabu sasa si tutaanza kuuza mko wa arusha kwa falme za kiarabu? Halafu yatafuata yale ya oic na kadhi yaani inji haitatawalika......aachane na mambo haya apumzike kwani heshima aliyojipatia inamtosha........self actualization
 
Loliondo na falme za kiarabu vinahusiana vipi na SAS?
 
..siyo lazima agombee kupitia CCM.

..kwa vitimbi alivyofanyiwa na wanaccm wenzake namshauri ajiunge na chama cha upinzani na agombee Uraisi kupitia chama hicho.
 
SAS anafaa sana. Pamoja na kusema siasa yeye basi kitendo chake cha kukaa kimya wakati nchi inaenda mrama mimi kinanisikitisha sana.

Kwanini mtu mwenye hadhi kubwa kama SAS katika jumuiya ya Kimataifa anakaa kimyaaa huku nchi ikendelea kwenda mrama!? Huu ni uzalendo kweli!? Unaiona nchi yako inasambaratika na wewe kutotia neno kuhusu hali mbaya ndani ya nchi yako kwa maoni yangu sijambo jema kwa kweli. Kuna haja ya SAS kuanza kuongea sasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa 2010 hata kama hayuko tayari kugombea tena.
 
Kama ungekuwa unaelewa Tatizo hasa lipo wapi au lilitokea wapi basi ushauri wako naimani ungeutowa tafauti na hivi ulivyouleta.4your information mmoja kati wa maduwi ya viongozi waliomkalia kwa ubaya na chuki anajityarisha kuwania Urais wa Zanzibar (Huhitajii operation ya Ubongo Kumjuwa mtu huyo )funika kombe mwanaharamu apite.
 
Bhaghosha,

SAS me namwaminia na anapendwa watanzania wengi sana tena kwa 95%, ingawa kila binadamu anamapungufu yake ila huyu bwana kwa uwajibikaji yuko makini, Jambo moja tu ningewauliza na muweke adharani kama angelikuwa Rais je Baraza lake la mawaziri lingekuwaje From Prime Minister etc
 
SAS anafaa sana. Pamoja na kusema siasa yeye basi kitendo chake cha kukaa kimya wakati nchi inaenda mrama mimi kinanisikitisha sana.

Kwanini mtu mwenye hadhi kubwa kama SAS katika jumuiya ya Kimataifa anakaa kimyaaa huku nchi ikendelea kwenda mrama!? Huu ni uzalendo kweli!? Unaiona nchi yako inasambaratika na wewe kutotia neno kuhusu hali mbaya ndani ya nchi yako kwa maoni yangu sijambo jema kwa kweli. Kuna haja ya SAS kuanza kuongea sasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa 2010 hata kama hayuko tayari kugombea tena.
Barua ya wazi kwa Dr.Salim -
Mhe. Salim - Wahenga walisema sadaka inaanza nyumbani, ndugu yetu SAS ukiwa unajua nchi yetu iko katika hali mbaya sana kiuongozi na ikiwa una uzoefu na sifa za kuliokoa taifa lako, kwa nini unalisaliti na kukaa kimya?
Ikiwa jumuiya za kimataifa zilikutegemea na kukuamini katika kusuluhisha migogoro mbalimbali ikiwemo Darfur iweje unakaa kimya kuhusu mustakbali wa Tanzania? nchi yako? Mpasuko wa kisiasa Zanzibar? Uongozi ndani ya chama chako unalegalega? Kwa nini hatukusikii katika issues kama hizi? Tunakuhitaji na tunahitaji kuona mwanasiasa kama wewe uwe mstari wa mbele na sio kukaa kimya! usiwe na tabia ya "mambo ya Ngoswe tumuachie Ngoswe" huku nchi inateketea, kwa sababu mtoto wa Ngoswe anacheza na kukua na mwanao,na pindi akiharibikiwa mtoto wa Ngoswe inamaanisha na mwanao ataharibikiwa vilevile, juu ya kuwa kaishi na kusoma Ughaibuni lakini endapo hirimu yake (young generation) hapa nyumbani itaharibikiwa ina maana ni maharibiko kwake yeye vilevile. na juhudi zako kumjenga katika misingi na kumpatia elimu haitoleta maana katika jamii atakayoishi.
Huu ni wakati ambao tunazihitaji sauti, busara na mchango wenu katika kupigania maisha bora kwa kila Mtanzania, Please, please sikiliza vilio vyetu, tunaamini mchango wako na moyo ulio thabiti unahitajika sana katika kipindi hiki kuliko wakati wowote ule,kumbuka wewe ni baadhi ya watu wachache wanaoweza kubadilisha sura ya CCM na nchi kwa ujumla, nasema pigana na uwe mstari wa mbele kwa ajili ya jamii ya watanzania na kile unachoamini na historia kamwe haitokusahau kama inavyomkumbuka Nyerere. Kumbuka kuwa wewe ni mmoja katika vijana aliowandaa Baba wa taifa kuliokoa taifa hili pale akiondoka.
Kumbuka wewe, The late Sokoine, Kikwete, Maalim Seif na Mkapa ndio vijana muliolikuwa tegemeo la Nyerere kuliokowa taifa hili, Kama ilivyo katika familia, Baba huweka matumaini kwa wanawe wote lakini kuna mipango ya Mungu, ingawa Nyerere alikuwa na matumaini kwa wanawe wote hawa, ukiachia Sokoine na wewe wengine wote walimuangusha Mzee wao na kwa vile Sokoine alikufa wewe pekee ndie unaweza kuendeleza ndoto za mwalimu na kuliokoa taifa hili, na ni imani ya wengi unaweza.
Tafadhali Timiza wajibu wako.
Ahsante.
 
Salim is a dejected man.He was literally brushed aside because of his ancestry! And.....in Tanzania where racialism was condemned and so much money was put to destroy APARTHEID!
How sad..I suport he should come and take over leadership.
 
Ndugu zangu, dont even waste your time to think that a clean man can ever get access into CCM leadership. Kuwa kiongozi ndani ya chama hiki lazima uwe mafya, mnywa damu za wanyonge yaani "vampire". Hiki ni chama kwa wachache wasiojua, lakini kwa wenyewe hili ni genge hatari sana ambalo moja malengo yake yasiyoaandikwa ni pamoja na kungamiza watanzania na yeyote atakaye watetea.

Unajua habari ya roli lililo taka kumuua Mwakyembe hadi leo halijulikana wala hakuna aliyehangika kulitafuta? Unajuakuwa trafiki walimwambia dereva "Huyu kesha kufa, wewe twende tu ukatibiwe Iringa". Unajua kuwa makamanda wa polisi wakubwa kabisa na tena wasomi wazuri waliharakisha taarifa inayofanana na ramli ya mganga wa kienyeji na kumwambia Mwakyembe "you have no right to speak about the accident that befell you"?

Connect hayo yote na kauli za kina Makamba, Kingunge, Chiligati, NEC na wenzao kuwa wapinga ufisadi wanakidhalilisha chama hivyo wanastahili kufukuzwa ndani ya chama. Utajua akina nani walitaka kumfukuza Mwakyembe duniani.

Mwalimu Wa Zamu
 
..siyo lazima agombee kupitia CCM.

..kwa vitimbi alivyofanyiwa na wanaccm wenzake namshauri ajiunge na chama cha upinzani na agombee Uraisi kupitia chama hicho.

Jokakuu,

Uwezekano wa SAS kwenda upinzani ni mdogo sana. Kama waliweza kumfanyia haya akiwa ccm, si watamkolimba kabisa akienda upinzani!

Yeye apigane kabisa kurudisha heshima yake iliyochafuliwa na Kikwete na wanamtandao wake at the same time akiindolea nchi uongozi mbovu wa Kikwete na wanamtandao wenzake.
 
Sijasoma post zote kwa hiyo nikirudia point naomba mniwie radhi, hapa naona CCM ime recall Kikwete kwa kuchagua mtu mwingine iwe Salim Ahmed Salim au Sita etc
 
Ndugu zangu, dont even waste your time to think that a clean man can ever get access into CCM leadership. Kuwa kiongozi ndani ya chama hiki lazima uwe mafya, mnywa damu za wanyonge yaani "vampire". Hiki ni chama kwa wachache wasiojua, lakini kwa wenyewe hili ni genge hatari sana ambalo moja malengo yake yasiyoaandikwa ni pamoja na kungamiza watanzania na yeyote atakaye watetea.

Unajua habari ya roli lililo taka kumuua Mwakyembe hadi leo halijulikana wala hakuna aliyehangika kulitafuta? Unajuakuwa trafiki walimwambia dereva "Huyu kesha kufa, wewe twende tu ukatibiwe Iringa". Unajua kuwa makamanda wa polisi wakubwa kabisa na tena wasomi wazuri waliharakisha taarifa inayofanana na ramli ya mganga wa kienyeji na kumwambia Mwakyembe "you have no right to speak about the accident that befell you"?

Connect hayo yote na kauli za kina Makamba, Kingunge, Chiligati, NEC na wenzao kuwa wapinga ufisadi wanakidhalilisha chama hivyo wanastahili kufukuzwa ndani ya chama. Utajua akina nani walitaka kumfukuza Mwakyembe duniani.

Mwalimu Wa Zamu

...na si ndio hii serikali ya CCM ilimwua yule mzee wa usalama Kombe kwa kutumia polisi wake na kumsingizia mzee wa watu jambazi na alikuwa hana silaha yeyote,nasikia wali mshoot akiwa anaongea nao na kuwaambia yeye ni Kombe..lakini dawa ya serikali inayo uwa au kuwafanyia umafia wenzao nao ni kuwafanyia same thing ndio kutakuwa kuna kuheshimiana!
 
...taja sifa au dalili za aliechoka na kukosa uwezo kuliongoza taifa.

Mambo mengine ni intuitive tu ndugu yangu.Naomba nikuulize swali umeshaona mababu wangapi kati ya 100 unaowajuwa ,walio zidi miaka 70 kuwa wakali kwa wajuguu wake kwa kuwachapa bakora na adha za namna hiyo.?
Na u conside mababu wale tu waliokuwa wakorofi wakati wa ujana wao. Na ukimaliza uje na majibu kwanini saizi hao mababu wako hivyo tofauti na ujanani mwao.?Ukileta majibu hapo nipo tutajadiri vizuri.
 
...na si ndio hii serikali ya CCM ilimwua yule mzee wa usalama Kombe kwa kutumia polisi wake na kumsingizia mzee wa watu jambazi na alikuwa hana silaha yeyote,nasikia wali mshoot akiwa anaongea nao na kuwaambia yeye ni Kombe..lakini dawa ya serikali inayo uwa au kuwafanyia umafia wenzao nao ni kuwafanyia same thing ndio kutakuwa kuna kuheshimiana!

Mkuu wangu mengine ni historia yani hadithi hadithi --- hadithi njoo na utamu kolea.

Watu wengine wanasinginzia tu mara wamekoribwa mara wame wachifupa lakini wengine wana UKIMWI ,wamebadirisha damu mara kadhaa wakiwekwa kati kwa kuhojiwa na kupewa kapresha kidogo ,haooooooo wamekwisha .

Hakuna anayeua mwingine mpaka pale ushahidi unapokuwepo wa wazi zingine nafikiri ni kuzidanganya nyakati.
 
Back
Top Bottom