Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010

We want a new blood and revolutionary ideas. Yes, Salim is a leader of his time. We want people who can focus and think of Tanzania 100 years to come and not only their office tenure...
\
Nanu & Geoff,
I support you. Tunataka damu mpya. Salim is too old now. Pia atatuletea matatizo huko ZNZ. Hafai kabisa. Kama Watanzania watashindwa kumchagua mtu atakaeiweza kazi, basi ninaamua nchi kuipa jeshi kuliko kuja kumpa mtu kama mkwere huyu wa sasa!
 
kwa mtizamo na mawazo yako unadhani ni nani anafaa kuwa rais ...siasa za bongo kweli utata
 
Sahau kitu kama hicho mkuu maana huyu jamaa alipata zahama kubwa sana kipindi chote cha mwaka 2005, Siasa za Tanzania ni za hatari sana

Ndio Salim alipata zahama kubwa sana 2005 na kuna sababu zake.

Tukumbuke huko nyuma Salum alituhumiwa na SMZ kushiriki mauaji ya Mzee Karume. Wakati akiwa mwakilishi UN alitakiwa aende Zanzibar kwa mahojiano na vyombo vya usalama Mwalimu Nyerere akamkingia kifua hasa Kutokana na yaliyowatokea wakina Mzee Hanga huko nyuma. Mwalimu alitaka vyombo vya usalama vya Zanzibar vifanye mahojiano na Salum hapa DAR na SMZ ikakataa. Tangu hapo katika macho ya SMZ ndugu Salim Ahmed Salim hajawahi kujisafisha kuhusu mauaji ya Mzee karume pamoja na kwamba SMZ ilikubali "yaishe". This is Salum's greatest political weakness.

Ndio maana 1985 baada ya Mzee Rashi Kawawa kukataa kumrithi Nyerere kwa sababu za kiafya pamoja na Nyerere kumtaka Salim aingie Ikulu wajumbe wa Kamati Kuu toka Zanzibar wakiongozwa na Marehemu Natepe
waliweka pingamizi kubwa sana. Pingamizi hili ndilo lililomuweka Mzee Mwinyi kwenye Urais 1985.

Ya 2005 wote tunayajua. pamoja na nguvu ya mtandao kumchafua Salum hilo halikuwa sababu muhimu sana. Sababu kubwa ni kwamba Salim hana support ya CCM kutoka Zanzibar. In other words he has no real consituency. Inasemekana kwamba karibu kura zote alizopata Salum kwenye mchakato wa Urais kwenye Halmashauri ya CCM zilitoka bara. Hata tukirudi nyuma kidogo wakati Makamu wa Rais Dr. Omar alipofariki ghafla wengi tulitegema Rais Mkapa amteue Dr. Salim (alisharudi toka OAU) kuwa makamu wake, lakini wapi? Kama angekuwa Mwalimu Nyerere angefanya lakini Mkapa hakuwa na ubavu huo.

Katika siasa za Tanzania na hasa Zanzibar, CCM kumteua Dr. Salim kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM ni kama ndoto za Alinacha! Na baada ya 2005 Salim analijua hilo.
 
Hivi Halmashauri Kuu ndo inamchagua Rais??
waliopewa pesa za kifisadi kumkaanga Spika??
Du! tutegemee Rais bora kutoka CCM! Ni ndoto!

Hivi Kamati Kuu wajumbe wake si ndo RA, Chenge, Mahanga, Makamba??
Au naota! Sipati jibu nani awe Rais.
 
Ni kweli kuwa jamaa anafaa, lakini kwa Tanzania Hawezi hasa ukianzia na ile mizengwe ya 2005, halafu CCM yenyewe hainamwelekeo wa kimaendeleo ya nchi ila mtu mmoja hasa vigogo. Ila kubwa kwa yote jamani ni UELWA WA WATANZANIA WENGI NI MDOGO. wanaopiga kura wanaamini ccm ndo amani, Hivyo uelewa ungekuwa mkubwa angeenda upinzani na afanye mambo
 
Hayo makombora ya 2005 ndiyo inabidi ayasahau...............

Hayo Makombora nina imani kabisa hata wale waliyoyaamini wakati ule sasa wameshagundua kwamba ulikuwa uzushi na uongo mtupu. Sidhani kama watarudia uzushi ule na this time anaweza kupeta
 
Wee bwana wee acha kumtakia mzee wa watu matatizo! hivi tu umesema hivyo watakua wamesha anza kumchunguza kama ni yeye kakutuma
 
Nasema hata ashuke Yesu au nabii yeyote yule mkubwa aliyepata kutokea duniani ili aiongoze my beloved country TANZANIA kupitia CCM, hataweza kufanya lolote la maana.
 
Yes!! Salim as a person is good...but tatizo si kuwa na mtu mzuri pekee...tatizo ni CCM. CCM as a system ndo inakwamisha maendeleo ya nchi hii. Hata mtu akiwa mzuri vipi.. it will take him years to reform this system. Ndani ya system hili nidhamu imepotea kabisa. Ingekuwa enzi zile Mwalimu bado ana nguvu ya kukemea... SAS angefaa kutusogeza japo for the next 10 years.
 
\
Nanu & Geoff,
I support you. Tunataka damu mpya. Salim is too old now. Pia atatuletea matatizo huko ZNZ. Hafai kabisa. Kama Watanzania watashindwa kumchagua mtu atakaeiweza kazi, basi ninaamua nchi kuipa jeshi kuliko kuja kumpa mtu kama mkwere huyu wa sasa!
Huyu Rais wetu ni mwanajeshi au tumesahau hilo? Once a soldier, you will always be a soldier. Tusije kuleta balaa bure maana what we need is leaders na sio kubahatisha bahatisha tu ili mambo yaende
 
huyu SALIM,akiwa hana shule alipewa ubalozi na KARUME,sasa uhusiano na karume mpaka kuumpa kijana mdogo kazi kubwa ambayo ilimsumbua sana kuitekeleza(this is in his own words)inaleta utata sana-could someone enlighten us on this
 
....tofautisheni askari au maafisa wapiganaji au wapiganishaji na maafisa au maaskari wahamasishaji ...jk ni mfano wa general sahef[wa iraq ya sadam].....yaani hawa kazi yao ni uhamasishaji la longo..wengi walichagua siasa..ie ...capt.john komba,marehemu nnauye.,jk,mkuchika ,jaka,etc...kitengo chao kilikuwa na bendi pia mwenge jazz,les mwenge na JWTZ taarab...bosi wao alikuwa MAJ gen.abdalah natepe.....akisaidiwa na nnauye.....tunawaita askari makamisaa wa chama!!![the so used to be called TPDF POLITICAL WING]
 
huyu SALIM,akiwa hana shule alipewa ubalozi na KARUME,sasa uhusiano na karume mpaka kuumpa kijana mdogo kazi kubwa ambayo ilimsumbua sana kuitekeleza(this is in his own words)inaleta utata sana-could someone enlighten us on this

salim hakupewa cheo na karume kwa kuwa alipendwa..bali ulikuwa mkakati wa karume kuwaondoa vijana wote waliokuwa HIZBU ....kwenda ubalozini au bara ...hapa alimuomba nyerere awachukue salim,babu et al.na siku za karibuni kina maua daftari...alikuwa akiwaona tishio kwa utawala wake...na hata kusingiziwa mauwaji ....ilitokana na hisia kuliko ukweli halisi.....

Tabia ya karume na waliomfuata ...kuwakimbiza kijanja vijana wa kipemba kwa kuwapeleka masomoni nje ndio imewafanya wapemba wengi wawe wasomi na kubakia nje...kwani wakishasoma walijikuta hawawezi kupata kazi za kuwafaa nyumbani.....au mazingira ambayo makusudi yalibakishwa duni ...hayakuwavutia kurudi!!!
 
Ndio Salim alipata zahama kubwa sana 2005 na kuna sababu zake.

Tukumbuke huko nyuma Salum alituhumiwa na SMZ kushiriki mauaji ya Mzee Karume. Wakati akiwa mwakilishi UN alitakiwa aende Zanzibar kwa mahojiano na vyombo vya usalama Mwalimu Nyerere akamkingia kifua hasa Kutokana na yaliyowatokea wakina Mzee Hanga huko nyuma. Mwalimu alitaka vyombo vya usalama vya Zanzibar vifanye mahojiano na Salum hapa DAR na SMZ ikakataa. Tangu hapo katika macho ya SMZ ndugu Salim Ahmed Salim hajawahi kujisafisha kuhusu mauaji ya Mzee karume pamoja na kwamba SMZ ilikubali "yaishe". This is Salum's greatest political weakness.

Ndio maana 1985 baada ya Mzee Rashi Kawawa kukataa kumrithi Nyerere kwa sababu za kiafya pamoja na Nyerere kumtaka Salim aingie Ikulu wajumbe wa Kamati Kuu toka Zanzibar wakiongozwa na Marehemu Natepe
waliweka pingamizi kubwa sana. Pingamizi hili ndilo lililomuweka Mzee Mwinyi kwenye Urais 1985.

Ya 2005 wote tunayajua. pamoja na nguvu ya mtandao kumchafua Salum hilo halikuwa sababu muhimu sana. Sababu kubwa ni kwamba Salim hana support ya CCM kutoka Zanzibar. In other words he has no real consituency. Inasemekana kwamba karibu kura zote alizopata Salum kwenye mchakato wa Urais kwenye Halmashauri ya CCM zilitoka bara. Hata tukirudi nyuma kidogo wakati Makamu wa Rais Dr. Omar alipofariki ghafla wengi tulitegema Rais Mkapa amteue Dr. Salim (alisharudi toka OAU) kuwa makamu wake, lakini wapi? Kama angekuwa Mwalimu Nyerere angefanya lakini Mkapa hakuwa na ubavu huo.

Katika siasa za Tanzania na hasa Zanzibar, CCM kumteua Dr. Salim kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM ni kama ndoto za Alinacha! Na baada ya 2005 Salim analijua hilo.
Wakati mwingine jukwaa hili linakuwa kama klabu cha pombe! analysis zingine zinazotolewa hapa ni tepe tepe sana,kwa mfano si lazima iwe ccm au chama kingine chochote rais ajaye lazima akubalike zanzibar! vigezo vya hivi haviwezi kutupa rais bora! anayechaguliwa na rais wa jamhuri ya tanzania!

Pengine kubwa la kutizama na linalotuunganisha watanzania wote ni kama candidate anaiweza kazi! kwa maana ya uzoefu,uaminifu,hekima,ujuzi,uthabiti nk, bahati mbaya sana watanzania wengi wanaochangia hapajf wanaiona kazi hii kama rahisi tu!!! ndio maana wanasikika wengine wakisema aje kijana next time!

Lakini ukweli kabisa kwa sasa hakuna kijana iwe kwa wale walio ktk uongozi sasa au walio nje anaweza kuwa rais mzr wa tz! pengine wengi wanavutwa kwa kutaka kuiga tu, kutaka nchi zingine zenye marais vijana.kwa tz ni vigumu!kwa sababu structuire ya malezi katika familia zetu ni mbovu kabisa siku hizi!!! hazimjengi mtoto au kijana kuwa kiongozi mzuri!! zinamjenga kuwa mbinafsi,mpenda anasa,mchoyo,mbaguzi,mnafiki nk. kwa maana hiyo bado tunahitaji sana kuwa na vongozi wa umri kama wa salim,shein,mwandosya,sitta, nk kwenye nafasi ya urais na makamu ili kutunza tunu za taifa letu,AMANI,UTULIVU,KUHESHIMIANA,UPENDO nk.

Mifano ipo mingi lakin ni vzr tunapojadili watz wanaoweza kufanya hii kazi tuongozwe na sifa ya UWEZO na siyo kutanguliza uwepo wa mizengwe au cjui mtandao hiyo ni fanatism tu haina nguvu sasa hivi,lkn mwisho kabisa yupo mwenyezi Mungu nayye ana hesabu zake! our choise is not ABSOLUTE!! it can be changed!!
 
Ndio Salim alipata zahama kubwa sana 2005 na kuna sababu zake.

Tukumbuke huko nyuma Salum alituhumiwa na SMZ kushiriki mauaji ya Mzee Karume. Wakati akiwa mwakilishi UN alitakiwa aende Zanzibar kwa mahojiano na vyombo vya usalama Mwalimu Nyerere akamkingia kifua hasa Kutokana na yaliyowatokea wakina Mzee Hanga huko nyuma. Mwalimu alitaka vyombo vya usalama vya Zanzibar vifanye mahojiano na Salum hapa DAR na SMZ ikakataa. Tangu hapo katika macho ya SMZ ndugu Salim Ahmed Salim hajawahi kujisafisha kuhusu mauaji ya Mzee karume pamoja na kwamba SMZ ilikubali "yaishe". This is Salum's greatest political weakness.

Ndio maana 1985 baada ya Mzee Rashi Kawawa kukataa kumrithi Nyerere kwa sababu za kiafya pamoja na Nyerere kumtaka Salim aingie Ikulu wajumbe wa Kamati Kuu toka Zanzibar wakiongozwa na Marehemu Natepe
waliweka pingamizi kubwa sana. Pingamizi hili ndilo lililomuweka Mzee Mwinyi kwenye Urais 1985.

Ya 2005 wote tunayajua. pamoja na nguvu ya mtandao kumchafua Salum hilo halikuwa sababu muhimu sana. Sababu kubwa ni kwamba Salim hana support ya CCM kutoka Zanzibar. In other words he has no real consituency. Inasemekana kwamba karibu kura zote alizopata Salum kwenye mchakato wa Urais kwenye Halmashauri ya CCM zilitoka bara. Hata tukirudi nyuma kidogo wakati Makamu wa Rais Dr. Omar alipofariki ghafla wengi tulitegema Rais Mkapa amteue Dr. Salim (alisharudi toka OAU) kuwa makamu wake, lakini wapi? Kama angekuwa Mwalimu Nyerere angefanya lakini Mkapa hakuwa na ubavu huo.

Katika siasa za Tanzania na hasa Zanzibar, CCM kumteua Dr. Salim kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM ni kama ndoto za Alinacha! Na baada ya 2005 Salim analijua hilo.

Hongera Mkuu,uloyaandika ni kweli na hii inatuonyesha kuwa bado CCM Zanzibar ina nguvu pale wanapotaka kutikisa kibiriti .... jee karata yao ni ipi hata wasikilizwe?
 
Back
Top Bottom