Wito kwa kina dada wenzangu:- Nilidanganyika, nikatumia kanuni ya P. M. U, sasa NAJUTA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,720
155,314
Jamani PMU ni pata mimba uolewe.
Nimedanganyika mwenzenu mie, nina mimba ya miezi miwili, namwambia mheshimiwa juu ya huu mzigo, na kuanza michakato ya ndoa.
Cha kusikitisha bwana kaka ananijibu, eti mie sina sifa za kuwa mkewe, ila nina sifa za kuwa girlfriend tu.
Hivi sasa kichwa chaniuma, najiuliza NIZAE AU NITOE, sipati jibu.
 
Kwani mlikuwa mmepanga na kukubaliana mambo ya ndoa au hayo mawazo ya ndoa yamekuja baada ya jamaa kuchana nyavu?
 
Umeliona kosa lako na kulijutia lakini? lea mimba yako na mtoto atakuwa wako peke yako utoe ya nini una uhakika kwamba wewe una yai la kumpata mtoto mwingine?,mwisho nikukumbuhe kitu kimoja kuolewa si lazima,mume hatafutwi kwa PMU
 
Kubeba mimba ili uolewe...pole sana...usitoe huyo mtoto....mtunze uzae ulee....mama yako angekutoa ungekuwepo??

Usiongeze kosa juu ya kosa.... waweza shindwa kuzaa huko mbeleni!!!
 
Kwa nini ulazimishe ndoa?

Tena kwa binadamu
Kama unataka ndoa muulize mungu
Kama alivompatia adamu mke na wewe atakupatia wa ubavu wako
Pole sana
Kuzaa sio kwamba ndo utaolewa tena
Subiri mume wako toka kwa bwana
 
Kwa nini ulazimishe ndoa?

Tena kwa binadamu
Kama unataka ndoa muulize mungu
Kama alivompatia adamu mke na wewe atakupatia wa ubavu wako
Pole sana
Kuzaa sio kwamba ndo utaolewa tena
Subiri mume wako toka kwa bwana

Wewe umeokoka lini?
 
Hio mnapenda wanawake kuitumia. Hayo mambo ya kizamani.
Hata mimi kama sijapanga kukuoa ukinilitea hizo nakubali mtoto kumlea lkn kwako mchozo unaishia hapo.
 
Kwa nini ulazimishe ndoa?

Tena kwa binadamu
Kama unataka ndoa muulize mungu
Kama alivompatia adamu mke na wewe atakupatia wa ubavu wako
Pole sana
Kuzaa sio kwamba ndo utaolewa tena
Subiri mume wako toka kwa bwana
mh! smile...........!!
i wish you...............
 
Tumekuwa wapenzi kwa mwaka na miezi sasa, nikadhani nikinasa basi itakuwa rahisi kwa mwenzangu kutangaza ndoa
kazi kweli kweli, wa kukuoa wala haitaji mimba....wakati ukifika ataamua tu lile limpendezalo...lea mtoto wako Gilesi,unaweza na Mungu akusaidie!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
pole,ila kubeba mimba sio ticket ya kuolewa,pengine wewe unawaza ndoa,yeye anawaza mchezo wa baba na mama na sio kukuoa.inauma ila songa mbele na maisha yako.wanaume wengine walivyokuwa wabaya,baada ya miaka kadhaa atamuulizia mtoto wake.ila kwa sasa hataki hata kusikia uja uzito.usitoe mwaya,mtoto ana raha yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom